Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?
Mimba ya namna hii kitaalamu hufahamika kama ectopic pregnancy. Je hii ni mimba gani? Hii ni mimba ambayo yai lililorutubishwa linaendelea kukuwa nje ya mji wa mimba (uterus). mimba inaweza kukuwa sehemu yeyote kwenye tumbo ila nje ya mji wa mimba. Kwa asilimia kama 90% mimba hukuwa kwenye mirija ya falopia. Hii ni mimba hatari sana na inahitaji uangalizi wa haraka sana, kwani inaweza kuhatarisha maisha ya mama. Inakadiriwa kuwa mimba za namna hii huchukuwa kati ya asilimia 1 mpaka 2 ya miba zote.
Kwa nini mimba hii ni hatari?
1.Mimba inatkuwa nje ya mji wa mimba hivyo haiwezekani mtoto kupona
2.Inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ama sehemu ilipokuwa.
3.Inaweza kusababisha ulemavu kwa mama endapo itachelewa kuonekana
4.Kwa asilimia 30 mimba hii haina dalili hii ni hatari zaidi.
5.Inaweza kusababisha uvujaji wa damu kwa kiasi ikubwa
6.Inaweza kusababisha mwanamke kuhitajiwa kufanyiwa upasuaji kamma tiba.
Sababu za kutokea mimba hii
Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa asilimia 30 ya mimba hizi hazina dalili. Lakini kwa kiasi kikubwa mimba hizi huwa na dalili. Tafiti zinaonyesha kuwa dalili zake hutokea kabla ya wiki ya 10. Sasa hapa nitakutajia baadhi tu ya dalili za mimba hii:-
1.Maumivu ya tumbo upande mmoja wa nyonga.
2.Maumivu ya mabega
3.Kutokwa na damu kwenye uke.
4.Maumivu ya nyonga.
5.Mvurugiko wa tumbo na kutapika
6.Maumivu ya upande mmoja wa mwili.
7.Kizunguzungu na uchovu
8.Maumivu ya mabega, shingo na mkundu.
Sababu za kutokea kwa mimba hii.
1.Kuwa na maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID
2.Uvutaji wa sigara
3.Kama una umri wa miaka 35 na kuendelea
4.Kama unatumia madawa ya kuivisha mayai
5.Kama ulishapata ujauzito huu hapo mwanzo upo uwezekano kuja kupata tena
6.Kama ulifanyiwa upasuaji kwenye mirija ya falopia
7.Kama una tatizo la endometriosis
8.Baadhi ya njia za kuthibiti uzazi mfano, IUD
Nini tena yapasa kujuwa?
1.Ujauzito uliotungia njea haurithiwi yaani kama mama aliwahikupata ujauzito huu hali hii hairithiwi.
2.Kutoka kwa ujauzito sio sababu ya kupata mimba hii
3.Kutoa ujauzito pia hakuna mahusianao na ujauzito huu
4.Mazoezi na michezo pia hihusiani na kutokea kwa ujauzito huu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kufunga kizazi kwa wanawake.
Soma Zaidi...Hali ya ujauzito huanza kutabirika Mara tu ya kujamiana, pia chemikali (hormon) za mwili huanza mchakato wa kuongeza na kupunguza utendaji kazi wa kemikali hizo mfano.follical stimulating hormon (FSH) na lutenazing hormon kuivisha yai tayari kwa kutengen
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kwa mjamzito huweza kuanaa kuonekana mwanzoni kabisa mwaujauzito, ndani ya mwezi mmoja. Ikabidi si dalili pekee ya kuwa ni mjamzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna unavyoweza kumtambua mtoto mwenye Ugonjwa wa Nimonia na tiba anayopaswa kupata mtoto mwenye Nimonia
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi
Soma Zaidi...Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
Soma Zaidi...Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...