Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito



KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO




Hili ni swali ambalo wengi ya wajawazito wanajiulizaga. Kwa ufupi hakuna shida yeyote kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito, bila kujali hatua ya ujauzito. Unaweza kuzungumza na daktari kuhusu swala hili, ila usiwe na shaka kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa endapo mwanamke akifika kileleni akiwa katika ujauzito ni jambo jema kwa afya yake na afya ya mtoto na afya ya ujauzito. Najuwa maneno haya machache hayawezi kumaliza kiu ya maswali yako. Sasa hebu tuone mabo kadhaa.



1.Kwa baadhi ya wanawake wanapata maumivu wanaposhiriki tendo hili wakiwa wajawazito. Yes hii huweza kutokea kwani kzunguruko wa damu umeongezeka maeneo ya chini na kufanya maeneo hayo yawe na hisia nyingi sana. Hii inaweza kuleta hali ya kuumia kwa mjamzito wakati wa kuingia kwa uume. Wajitahidi wakati wa tendo hili kutumia muda mwingi kujiandaa, pia spidi upungue, na tendo lisifanyike kwa nguvu kama siku za kawaida.



2.Kuna baadhi ya wanawake wanajikuta uke wao umepunguza hali ya kubana yaani wanahisi unabwebwea. Ukweli ni kuwa kutokana na ongezeko la majimaji mwanamke anaweza kuhisi kuwa ule mnato na msuguano aliouzoea haupo. Hali hii inaweza kuwapunguzia hamu ya tendo baadhi ya wanawake.



3.Kwa baadhi ya wanawake majimaji yanakuwa mengi kiasi cha kuhisi kumkosesha raha mwenziwake. Hii hutokea baada ya msisimko kuzidi ama kwa sababu kuna mabdiliko ya homoni. Kama hali ni hii hakuna budi kuvumiliana.



4.Mkao wowte unaweza kutumika maadamu hautakandamiza tumbo la mama. Hapa wawe makini sana hasa ujauzito ukiwa mkubwa wasijelibana tumbo. Mkao wa ubavu ubavu na inayofanana na namna hiyo inaweza kuwa ni mizuri. Zungumza na daktari atakupa maelekezo vyema



5.Je kushiriki tendo kunaweza kusababisha ujauzito kutoka? Hapana si kweli kabisa. Ujauzito hauwezi kutoka eti kwa kushiriki tendo la ndoa.



6.Baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa mjamzito anaweza kuona damu ama kutokwa na damu. Hii pia sio tatizo. Ila kama itakuwa inatoka kwa wingi vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.



7.Kwa baadhi ya wanwake inafikia wakati hahisi chochote anaposhiriki tendo na anakosa hamu kabisa ya kushiriki. Hili sio tatizo kubwa anaweza kumuona daktari kwa maelezo zaidi.



8.Kama atahisi dalili zifuatazo ni vyema kumuona daktari:
A.Maumivu makali zaidi yasiyovumilika
B.Damu nyingi
C.Kushindwa kupumuwa vyema





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 616


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-