Zaituni (olive).
Ni katika matunda yaliyojulikana toka zama za zamani sana. Tunda hili lina kiwango kikubwa cha cha vitamini E na madini ya copper na calcium. Pia tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidantan ambayo husaidia katika kuimarisha afya ya moyo na ini na pia husasidia katika kuzuia uvimbe.

Pia tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya zaituni yana oleic acid yaani asidi ya oleik ambayo husaidia katika kuimarisha afya ya moyo pamojha na kuzuia kupata saratani. Pia tafiti zinaonesha kuwa tunda hili lina chembechembe ambayo husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa osteoporosis. Huu i ugonjwa wa unaowapata sana wazee, na huathiri mifupa na kuifanya dhaifu.