8.Tikiti (watermelon). Tunda hili pia ni katika matunda yenye vitamin C na A kwa wingi. Tafiti za kisayansi pia zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidant ambazo ni pamoja na lycopene, carotenoid na cucurbitacin E. Hizi husaidia katika kuzuia mwili usipate saratani au kupunguza athari za saratani. Tikiti husaidia katika kupata choo kwa urahisi.

Antioxidant zilizopo kwenye tunda hili husaidia kuzuia saratani ya mfumo wa mmengenyo wa chakula na kuota kwa vimbe ambazo ni viashiria vya saratani. Lycopene husaidia katika kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa zina uwezo wa kupunguza cholesterol na shinikizo la damu. Katika matunda yote tikiti linajulikana kuwa ndio tunda lenye maji mengi. Lina asilimia 92% ya maji.

Ndani ya tikiti kuna virutubisho kama vitamini C, Vitamin A, vitamini B1, B5, na B6. pia kuna madini ya potassium, magnesium. Vitamin C ni antioxidant ambayo husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli kutokana na mionzi. Ndni ya tikiti kuna carotenoid hizi ni chembechembe ambazo mwili huweza kuzibadilisha na kuwa Vitamini A. pia chembecheme ziitwazo lycopene hizi ndizo zinazolipa tikiti rangi nyekundu. Chembechembe hizi zinafaida chingi za kiafya mwilini.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa tikiti lina chembechembe ambazo husaidia kuatika kupunguza athari za ugonjwa wa saratani. Mingoni mwa chembechembe hizo ni lycopene. Kitaalamu hizi huitwa anti-cancer. Hizi hupunguza athari za saratani kwa kuwa hupunguza uzalishaji wa IGF (Insulin-like Growth Factor) hii ni aina ya protini ambayo hutumika katika uzalishaji wa seli yaani cell division. Wataalamu wa sayansi wanaeleza kuwa IGF ina mahusiano makubwa na ugonjwa wa saratani. Pia ndani ya tikiti kuna cucurbitacin Eb hii husaidia katika kuzuia uotaji wa uvimbe wa saratani (growth of tumor).

Tikiti husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya moyo kama vile kiharusi, shambulio la moyo na presha. Tafiti zinaonesha kuwa lycopene husaidia katika kupunguza kiwango cha cholesterol na kupunguza shinikizo la damu.pia lycopene husaidia katika kupunguza unene wa ukuta wa mishipa ya artery (mishipa mikubwa ya damu). pia tikiti lina citrulline, ambazo ni amino acid hizi husaidia katika kutanua mishipa ya damu hivyo kupunguza presha (yaani shinikizo la damu). pia vitamini na madini mengine tulotaja huko juu ambayo yamo kwenye tunda hili husaidia katika afya ya moyo. Kama vitamini A, B6 na C pia madini ya magnesium na potassium.

Tikiti ni tunda safi kwa afya ya ngozi na nywele. Uwepo wa vitamini A na C kwenye tunda hili kunalifanya tunda hili liwe muhimu katika nyanya hizi za ubora wa ngozi na nywele. Vitamin C husaidia mwili wako kutengeneza collagen, hizi ni protini ambazo hizi huweza kufanya ngozi yako iwe laini na rahisi kukunyika na kuzifanya nywele zako ziwe na afya na mathubuti. Pia vitamin A kusaidia katika kutengenezwaji wa seli mwilini hivyo husaidia katika ukuaji wa nywele. Bila ya vitamini A ngozi yako itaonekana kavu na isiyo ya kawaida. Vitamini A na C husaidia katika kuzuia ngozi yako kuungua na jua.