Navigation Menu



image

mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

mgawanyiko katika quran

imageimage MGAWANYIKO KATIKA QURAN
Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara
Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Katika Darsa hii tutaangalia migawanyiko hii.

Sura katika qurani zimegawanywa katika makundi makuu mawili:
1.sura zilizoteremshwa Makka na na huitwa Maki
2.Sura zilizoteremshwa Madina na huitwa madani

Sura hizi unaweza kuzijuwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu ambazo zimewekwa na maulamaa wa elimu za Quran. Ila kwa ufupi ni kuwa Sura za makka ni zile ambazo zimeteremshwa kabla ya mtume (s.a.w) hajamaliza hijra kufika madina na zile za madina ni zile ambazo zimeshushwa wakati mtume (s.a.w) amesha hama kwenda madina.

Utofauti wa sura hizi ni kuwa nyingi katika sura zilizoshushwa Maka ni fupi na Maudhui yake yamejikita sana katika kuboresha imani. Na zile za Madina zina sifa ya kuwa ndefu na maudhui zake nyingi zimekuwa zikizungumzia hukumu na sheria.

Pia qurani nzima imegawanywa katika vipande vipande kama ifuatavyo
1.Juzuu 30
2.Surah 114
3.Rukuu(paragraph)
4.Aya
5.Manzil

Aya ni umoja na wingi wake ni Ayat. Ni vigumu kufasiri neno Aya kwa kiswahili ila kwa ufupi unaweza kusema ni sentesi ijapokuwa maana hii ni tofauti kidogo ila angalau inaleta maana. Aya katika Qurani zipo 6236. Na aya ndani ya Qurani inaweza kutengenezwa na mkusanyiko wa maneno au herufi. Pia aya inaweza kuwa herufu mojatu na ndo maana ni tofauti na neno sentensi kwa kiswahili.

Sura katika qurani zipo 114 na sura zote zimeanzwa na basmala isipokuwa sura ya 9 surat trauba yenyewe haina basmala. Kuna sababu nyingi zinatolewa na na wajuzi katika elimu za Quran kuelezea kwa nini sura hii haijaanzwa na basmala. Ila kwa ufupi ni kuwa hakukupatikaniwa dalili ya kufanya hivyo kutoka kwa mtume(s.a.w). Tutazungumzia zaidi mas-ala hii katika asbab-nuzul. Halikadhalika basmala kwenye qurani zipo 114 kuna sura moja ina basmala 2 nayo ni surat an-namli ambayo ni sura ya 27. Sura kwenye qurani zimepangiliwa kuanzia 1 mpaka 114. Ila mpangilio huu sio kulingana na kushuka kwao.

Rukuu ni mgawanyiko mwengine. Kwa kiswahili rukuu ni aya. Rukuu wingi wake ni rukuu’at na huweza kutengenezwa na muunganiko wa aya nyingi ambazo zote zinazungumzia maudhui moja. Katika qurani kuna rukuu 558. Alama ya rukuu ni herufi ع kubwa. Alama hii ina sehemu kuu 3 juu kati na chini.
1.juu huwekwa namba ya rukuu kuwa ni ya ngapi kwenye sura
2.Kati huwekwa namba za aya zilizomo kwenye hiyo rukuu
3.Huwekwa namba ya rukuu kuwa ni ya ngapi kwenye Quran

Juzu zipo 30 katika qurani yote. Hii ni rahisi kwa watu wanaotaka kumaliza kusoa qurani katika mwezi mmoja yaani ndani ya sikun 30. Kwa mashafu za kuhifadhisha qurani kila juzu inakuwa na kurasa 10 isipokuwa zujuu ‘Amma ambayo ndo juzuu ya 30 yenyewe ina kurasa zaidi.

Manzil wingi wake ni manaazil. Qurani imegawanywa katika manazil saba 7. Hii huwezesha urahisi kwa wanaotaka kumaliza kusoma qurani ndani ya wiki moja yaani siku saba 7. Manaazili huandikwa namba zake nyingi ya ukingo wa kurasa ya mashaf.
1.Manzil 01 huanzia sura ya 1 hadi ya 4
2.Manzil 02 huanzia sura ya 5 hadi ya 9
3.Manzil 03 huanzia sura ya 10 hadi ya 16
4.Manzil 04 huanzia sura ya 17 hadi 25
5.Manzil 05 huanzia sura ya 26 hadi 36
6.Manzil 06 huanzia sura ya 37 hadi 49
7.Manzil 07 huanzia sura ya 50 hadi 114


                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1126


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Swala ya Kuomba Toba (tawbah) na namna ya kuiswali
Soma Zaidi...

maana ya swala kilugha na kisheria
Soma Zaidi...

Siku ya Taqwiya na kusimama Arafa
5. Soma Zaidi...

Haya ndio matendo ya hija
Soma Zaidi...

Lengo la swala
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Soma Zaidi...

Kuamini siku ya mwiho: Pia utajifunza kuhusu maisha ya barzakh (kaburini), siku ya qiyama
Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)
Soma Zaidi...