image

Kwisha kwa chakula

Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad

KWISHA KWA CHAKULA

Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Tulianza kuwazika mpaka wenzangu wote wakaisha hata nikamzika mwenzeu wa mwisho pekeangu na kubakia mimi tu. Nikiwa na mkate mmoja tu wa ngano ulobakia nikaaza kulia na kijuta kuwa bora nisingesafiri. Nilikata tamaa na nguvu ziliniishia nikajua sasa ndo nakufa mimi. Wakati nilipokuwa nimekaa pale niliona ndege akinywa maji ya kale kajimto. Nilitamani nimuuwe ndege yule nipate chakula.

 

Nilianza kumvizia ndege yule na hata nikamrushia jiwe, na kwa kiwewe ndege yule akaingia kwenye lile pango ambalo kale kajimto kamepotelea. Nilimsubiri nje ya pango ili atoke lakini hakuweza kutoka hata ikafika jioni. Nikala kipande cha mkate na kubakiwa na kipande kimoja. Ilipofika asubuhi nikapata akili luwa kama yule ndege hakuweza kutoka kwenye [pango lile kutakuwa na mabo makuu mawili yanaweza kutokea, moja huenda ameliwa au ametokea nje ya pango sehemu nyingine. Hapo nikajipa matumaini kuwa mto huu utakuwa umetokea eneo jingine.

 

Basi nikaanza kuunganisha mabao kisha nikajilaza kifudifudi na kukusanya mali za dhahabu, almasi na mali nyinginezo za madini katika eneo lile na kulweka mabao yangu kwenye mto ule ambao ulinichukuwa na kupotea nami kwneye pango. Niliweza kupitishwa sehemu nyembembe sana ambapo niliumia sana. Nilimaliza kipande cha mkate wangu hata nikawa sina chochote. Nikawa nawaz anaweza kufa humu kabla hata sijaliona jua. Kwa njaa na mawazo na maumivu ya kugongwa nilipoteza fahamu na nisijue kinachoendelea kwenye mto ule.

 

Nilipokija kuzinduka nikakuta nimezungukwa na watu wengi sana na ni wakubwa zaidi. Wakawa wananiuliza mimi ni nani na nimefika vipi pale kwenye eneo lile. Kabla sijaeleza chochote kwani sikuwa na uwezo wa kusema hivyo nikaomba wanipatie chakula na maji. Nikapewa na kuanza kuridhisha tumbo langu hata nikashiba na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nikawaeleza habari yangu na walishangaa sana. Wakaamuwa kunipeleka kwa mfalme wao ili apate kujuwa yalonikuta.

 

Walinichukuwa mimi na mabao yangu yale na mali zangu na ku nipeleka kwa mfalme wao wa kisiwa hiki kiitwache Serendib. Kwa heshima na taadhima nikamsalimia mfalme na kumueleza kila kilchotokea bila hata ya kuficha. Mfalme alishangaa sana na kuniona nimezaliwa na nyota ya ajali inayoambatana na uokovu. Mfalme akamumu habari yangu iandikwe kwa maandishi ya dhahabu na iwekwe kwenye hifadhi ya kifalme kwa vizazi vijavyo.

 

Nilikaa pale Serendib kwa muda wa mwezi mmoja na nikamuomba ruhusa mfalme niweze kurudi nyumbani. Alikubali na kunipatia malinyingi kisha akanipatia barua ili nikampe Sultan Harun Rashid wa Baghadad. Barua ilikuwa imeeandikwa kwenye karatasi cha bluu zilizotengenezwa na ngozi ya nyok. Maadhishi yalikuwa ni ya dhahabu yaliyochovywa na mafuta ya misk. Mfalme pia alinipatia zawadi nyingi sana kwa ajili ya familia yangu na kwa ajili ya Sultani Harun Rashi. Barua ilikuwa na lengo la kuomba urafiki kati ya vuiongozi wawili hawa.

 

Nilisafiri kwa amani hata nikafika kwenye bandari ya Balsora na kufika nyumbani na mali mengi sana. Niliwaeleza ndugu zangu yalonikuta na safari hii nikaadidi kuwa sasa sitosafiri tena kibiashara. Siku ilofuata nikaongozana na familia yangu na kuelekea kwa Sultan kwenda mpatia barua yake. Sultani alifurahi sana na alipenda zawadi alopewa. [ia aliniuliza habari nyingi kuhusu mfalme wa Balsora na kumridhisha maswali yake. Nikaondoka na kurudi kwangu. Baada ya hapa nikaanza kutengeneza maisha yangu na sikutaka tena kusafiri majini.

 

Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii ya safari hyake ya sita Sinbad alimpatia Sinbad wa nchikavu pesa kiasi kadhaa kama fidia ya kupoteza muda wake na kumsikiliza. Watu wakatawanyika pale na akamuahidi Sinbada awahi kesho ili asikilize kilichotokea kwenye safari yake yta saba na kwa nini alivunja ahadi yake mara hii.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-09 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 994


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Wanyama ambao hutolewa zaka
(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo. Soma Zaidi...

HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME. Soma Zaidi...

HADITHI YA KHALID MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID. Soma Zaidi...

KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME. Soma Zaidi...

JINI NA MFANYABIASHARA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA. Soma Zaidi...

Alif lela u lela: utangulizi
Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Soma Zaidi...

Hadithi ya waziri aliyeadhibiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

TONGE LA MWISHO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KWISHA KWA CHAKULA Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: KIFO CHA DAMU
Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...

KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO. Soma Zaidi...