HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.

HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME


Download kitabu Hiki Bofya hapa

HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.

Juwa ewe mwenye kuja kwa jina la Habili kwa cheo cha mchanja kuni kuwa mimi ni mtoto wa mfalme niliyetambulika kwa uzuri na hta mawaziri na watoto wa wafalme wakawa wanagombana kwa kutaka kunipata kuwa mke wao. Ugovi huu ulikuwa mkali hata ukaingiliwa na viumbe visivyo onekana navyo vikataka kunioa nao ni maini waliombali na rehema za Mwenyezi mungu.

Nyumbani kwetu kulikuwana kisima kilichoaminika kuwa ni cha muda mrefu kisichopungua umri wa miaka 150. katika kisima hiki kijana wa kijini alichikuwa madaraka ya kutawala majini waliopo kwenye kisima kile. Siku ile nilikwenda kuchota maji kisimani pale nikiwa kichwa changu kipo wazi kinyume na maamrisho ya dini yetu. Bila ya kutambua unywele wangu mmoja uliangukia kwenyekisima kile na kumganda kiongozi mpya a majini alipokuwa akipewa majukumu.

Nilirudi nikiwa na mabadiliko katika kichwa changu hata ndoo ya maji niliiona n nzito sana kuibeba hivyo nikatumia mikono yangu kubeba maji yale. Siku ile sikupata usingizi kwa maumivu ya kichwa na nilipopata usingizi nilshituka kwa ndoto za kutisha nilizokuwa ninazipata. Sikujuwa chanzo cha matatizo haya yote. Ilipofika asubuhi nilimueleza baba yangu ju ya maumivu ya kichwa changu. Baba alimwita daktari wetu na kuanza kunitibia. Kwa muda wa siku 5 sikupata nafuu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yakinizidia.

Kwa muda wa miezi waganga na madaktari wote walishindwa kutibu ugonjwa wangu. Ilifikia hali kuwa mbaya hata nikawa sinafahamu juu ya niayofanya, unaweza kusema nilikuwa mkichaa ambaye akili zinaingia na kutoka. Hali hii ilimpa baba yangu wakati mgumu hata akafikiri ni maradhi yaliyosababishwa na wale wachumba wliokuwa wakinigombania. Habari za ugonjwa wangu zilienea nchi nzima na kila mtaalamu wa tiba alikuja kujaribu bahati yake kwani donge nono liliahidiwa kwa atakayenitibu.

Miezi sita ilifika na habari za ugonjwa wangu zikaenea nchi za majirani. Baba alifikia hatua akatangaza kwa yeyote aatakayenitibu ataniozesha nae. Jambo hili lilisababisha hata wataalamu wa ta kutoka nchi za jirani wa lengo la kunioa pindi wakifanikiwa kunitibu. Bila ya mafanikio yeyote juu ya ugonjwa wangu ijapokuwa wapo walofaniukiwa kunipa nafuu lakini haichukui muda kabla ya ugonjwa kunizidia.

Siku niliota ndoto ya kushangaza. Ndoto hii nilipomwambia baba alijaribu kuwauliza wataalamu wenye kujuwa tafsiri za ndoto. Basi akaja mtaalamu na akaniambia nimueleze ndoto ile bila hata ya kuacha hata sehemu ndogo. Basi nilikaa kimya kwa muda kisha nikakusanya mawazo yangu na kuanza kumuelezea ndoto yangu kama ifuatavyo;-


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 859

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Safari ya nne ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
KIAPO CHA SULTANI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KIAPO CHA SULTANI.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mke na kasuku

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA KISIWA CHA MAWE YANAYOLIA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA.

Soma Zaidi...
SAFARI YA TATU YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa.

Soma Zaidi...
Alif lela u lela 1

Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa.

Soma Zaidi...
KISIWA CHA UOKOZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli.

Soma Zaidi...