image

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: KIFO CHA DAMU

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: KIFO CHA DAMU

Kifo cha damu

by Rajabu Athuman

KIFO CHA DAMU

KITABU CHA PILI,
HADITHI ZA ALIF LELA U LELA
UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA.
Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Mfalme huyu alikuwa na watoro wawili ambao ni Shahariyar na Shahzaman. Watoto hawa walikuwa mahodari na walifahamika sana. Alipofariki baba yao mtoto mkubwa alitawala kiti cha baba yake kuanzia makao makuu na mdogo wake akaendelea kutawala maeneo ya Samarqand.


Baada ya kutengena kwa muda ndugu wawili hawa walipanga kukutana. Makutano yao yalifanikiwa kupangwa na hatimaye wakakutana. Katika wakati kama huu wa kukutana kwa ndugu wawili hawa kulitokea hali za kusalitiwa na wakezao. Shahariyar alikuwa na mkewake aliyempenda sana na hakuamini kuwa inaweza kutokea siku akasalitiwa na mkewe. Baada ya usaliti huu aliamini kuwa hakuna tena mwanamke mkweli duniani kote. Hivyo akaweka nadhiri ya kuoa mke mpya aliye kigori na kumuuwa kila ifikapo asubuhi.


Kiapo hiki cha Sultani huyu kilikuwa kweli na alikuwa akifanya hivyo yaani anaowa jioni na asubuhi anauwa. Hali ilikuwa ngumu kiasi kwamba watu wakawa wanawakimbiza mabinti zao mjini. Sifa zote nzuri za Sultani huyu zikaanza kuwa mbaya kwa kitendo chake cha kuuwa watoto wa kike. Kazi yote ya kutafuta mabinti wa kuolewa na mfalme pamoja na kazi ya kutekeleza ahadi ya mfalme kuwauwa mabinti hawa alipewa mmoja katika mawaziri wa Sultani huyu.


Sultani huyu alikuwa na mabinti wawili ambao ni Schehrazade na Dinarzade. Mabinti hawa walikuwa ni wazuri sana na walipendana na hata hivyo walipata upendo mkubwa sana kutoka kwa mbaba yao. Schehrazade ambaye ndiye mkubwa alikuwa ni mrembo zaidi na alikuwa na taaluma mbalimbali na alikuwa na elimu za mambo mengi hata ya kisayanzi na masimulizi ya fasihi. Watu wa nchi hii waliamini kuwa uzuri alonao Schehrazade anafaa kuilewa na mfalme au mtoto wa mfalne na si mtu mwingine.


Sikumoja katika mazungumzo ya kifamilia kati ya waziri na watoto wake Schehrezade alitowa ombi la kushangaza kwa baba yake na kumwambia kuwa anatakakukomesha tabia ya mfalme ya kuuwa mabinti hivyo anataka siku ifiataya aolewe yeye. Waziri alishangaa na kumuonya mwanae lakini hakusikia. Akajaribu kumtisha na akamsimulia hadithi ya mfugaji na mkewe lakini msmamo wake hauku badilika. Basi harusi ikafanyika na Shehrazadw akapanga mpago na Dinarzade juu ya kutaka kukomesha tabia ya Sultani.


Usiku nyumbani kwa mfalme Dinarzade alisikika akimuamsha dadayake Schehrazade ambaye anatarajiwa kuuliwa ifikap asubuhi. Dinarzade alimwambia dada yake apigie hadithi nzuri iwe kama ndio mazungumzo ya kuagana. Schehrazade aluimtaka idhini mfalme na kukubaliwa. Akaanza kumsimulia hadithi ya mfanya biashara na jini. Masimulizi ya hadithi hii yalionekana kumvutia na Sultani pia. Schehrazade kwa ufundi wake wa kusimulia hadithi aliikata hadithi hii na kumwambia Sultani akimuongeza siku zaidi ya kuishi ataimaliza.


Sultani alimpa siku zaidi Schehrazade ili amalizie hadithi zake. Utamu uliendelea kumpanda Sultani na kila siku hadithi zilikuwa zinaishia patamu. Hivyo Schehrazade akaendelea kupata muda zaidi wa kuishi. Dada huyu alisimulia hadithi ya mvuvi na jini, hadithi ya chongo watatu na mabinti wa baghadad na nyinginezo hata akafikia kwenye hadithi ya Sinbad. Dada huyu alipomaliza hadithi hii akabakiwa na kuelezea yalotokea kwa mtoto wa Sinbad.


Basi siku ilofata baada ya kuisha kwa hadithi ya Sinbad Scheherazade akaanza kusimulia kilichotokea kwa mtoto wa Sinbad alozaliwa na bint โ€˜Aisha mtoto wa mfalme. Scheherazade akamueleza kuwa atahaya ya msimulia hadithi nzuri zaidi ya ile a mtoto wa Sinbad. Hapo Sulltani akamwambia asimulie hiyo hadithi nzuri zaidi ya mtoto wa Sinbad. Hapo Scheherazade akaanza kusimulia hadithi ifuatayo.


KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SUKLTAN.
Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Kijana huyu alizoeleka sana na mfalme kiasi kwamba mfalme hakuwea kumkosa hata kwa siku moja. Siku moja kijana huyu akiwa kwenye dimbwi kubwa la mawazo alitembea maeneo kadhaa katika mji huu na akakutana na Mshona nguo. Alikaa sana kwenye eneo hili nje ya ofisi ya mshona nguo.


Muda wa kufunga ofisi ulipofika mshonanguo alimchukuwa kijana huyu na kwenda naye nyumbani kwa lengo la kufurahi nae na kula chakula. Alipofika nyumbani mkewake alimpokea kwa ukarimu kijana huya. Na kwa ufundi na uwezo wa kutoa burudani alio nao kijana huyu aliweza kuchangamsha nyumba hii. Mke wa mshonaji alianza kuandaa chakula kizuri sana na nyama ya samaki. Aliandaa ndizi na vyakula vizurivizuri kwa ajili ya mgeni wao.


Huku burudani zikiendelea mke wa mshonaji aliendelea kupika. Mshonaji alikwenda kuchukuwa vinywaji kadhaa na kuvileta pale nyumbani kwao. Muda wa chakula ulipofika walikusanyika na kuanza kula. Katika kufanya manyonjo na furaha mke wa mshonaji akachukuwa nofu la nyama na kuliiweka kwenye mdomo wa kijana yule na kumwambia meza. Kijana alimeza na kwa bahati mbaya kwenye nofu lile kulikuwa na mwiba mkubwa sana. Mwiba ule ukamkaba kijana yule na kupoteza maifahamu.


Mshonaji baada ya kuangalia hali ile akagunduwa kuwa kijana amekufa. Kuona hivyo akaogopa sana maana ataambiwa amemuuwa kijana wa watu. Wakashauriana na mkewake nini wafanye. Baada ya muda wakaamuwa kumchukuwa marehemu waendenae kwa tabibu ili wamuachie msala wote tabibu. Hali ikawa hivyo na wakambeba hadi mlangoni kwa tabibu kisha wakamlaza pale.


Waligonga hodi akatoka kijana wakamueleza amuite abibu harakwa kuna mgonjwa ana hali mbaya. Alipoingia ndani yule mtto kwenda muita tabibu mshonaji na mkewe wakakimbia. Tabibu alitoka na kiza cha usiku ule na akamkanyaga huyo aloambiwa mgonjwa. Ikawa tabibu akafikiri yeye ndo alomuuwa mgonjwa. Akanza kushauriana na familia yake wajue namna ya kujinusuru na janga lile. Mke wake akamshauri mumewe kwa kumwambia kuwa wamueke kwenye ukuta wa jirani yao.


Jirani yao alikuwa ni muuza nyama hivyo kulikuwa na wezi wanakuja kuiba nyamma pale kwake. Hivyo walifikiria huenda akampiga na kujuwa amemuuwa yeye. Basi wakamfunga kamba karehemu yule na kumpenyeza kwa nje ya nyumba yao kupitia paani. Aliposimama sawa kwenye ukuta wa jirani yao kwa nyuma wakaitowa kamba ile. Ilipofika usiku sana yule muuza nyama alirudi nyumbani na alipoona mtu kasimama kwenye ukuta wake akajuwa ni mwizi amekuja. Hivyo akachukuwa fimbo kubwa na kuanza kumtandika sawasawa. Hatimaye mtu yule alianguka na alipomgusa akahisi ameshakufa.


Kwa woga akafikkiria kuwa ameuwa mtu. Akaanza kushauriana na familia yake namna ya kujinusuru na mkasa huu.wakaamuwa wambebe maiti yule kisha wakamsimamishe kwenye moja ya kuta za sokoni, huenda akakumbana na walinzi wakampiga na hapo itakuwa ameuliwa mwizi na esi itaishia hapo. Wakafanya hivyo na baada ya muda mmoja katika walevi akapita eneo lile na alipoona mtu kajibanza akajuwa ni wale watu wanaomnyemelea siku zote na kumuibia pindi akilewa.


Mlevi yule alinyata pale karibu na kumpiga chupa ya mgongoni mtu yule. Hatiumaye kwa pigo moja la mlevi mtu yule akaangunga na m;evi kuangalia vile akajuwa kuwa ameuwa. Palepale walinzi walifika na kumkamata mlevi yule kwa kosa la kuuwa mtu. Basi kesi ile ikapelekwa kwa kadhi ili hukumu itolewe, na hukumu ikapita kuwa mlevi ni muuwaji hivyo naye auliwe. Mlevia akapelekwa katika uwanja wa mauaji na kuwekwa tayari kuuliwa.


Wakati hukumu inataka kupitishwa ghafla akatokea yule muuza nyama na kusema โ€œewe ndugu hakimu tafadhali niuwe mimi kwani ndiye nilomuuwa huyo kijana na si huyo mleviโ€ basi pale pale akaondolewa mlevi na muuza nyama akatiwa kitanzi tayari kwa kuchinjwa. Kabla hajachinjwa akatokea tabitu na kusema yeye ndiye muuwaji hivyo achinjwe yeye. Na alipotaka kuchinjwa tabibu alikuja mshona charahani na kusema yeye ndiye muuwaji halisi na wote hawa hawahusiki. Kitanzi kilipokuwa kwa mshona charahani. Kabla ya kufanya zoezi hakimu akaanza kushauriana na wenzie nini wafanye maana muuwaji halisi hawamjui.


NANI MUUWAJI?
Mfalme alipoamka alitaka kumuona kijana wake lakini asimuone. Akauliza habari za kijana yule na akaelezwa kuwa amefariki lakini muuwaji hajulikani, mpaka sasa kuna wauwaji wanne na kila mmoja anadai yeye ndio muuwaji halisi. Mfalme akaamrisha wote waitwe na waje mbele yake na amtafute muuwaji halisi wa kijana wake yeye mwenyewe.


Mfalme aliogopa sana asije fanya kosa kama lile alolifanya kwenye kesi ya kifo cha mtoto kwenye ndoo ya maji ambapo mtu asiye na hatia aliuliwa. Walinzi wa mfalme wakamuuliza kwani ni kitu gani kilitokea kuhusu kesi ya mtoto huyu. Akawasimulia kwa ufupi habari hii kuwa alikiwepo mama mmoja aliyekuwa na mtoto anayeanza kusimama dede. Pale ndani palikuwepo na mfanya kazi wao. Mtoto yule alizoeshwa kuogeshwa kwenye ndoo ya maji na mama yake a alikuwa akifurahia sana anapotiwa kwenye ndoo ya maji.


Siku moja mama yule alipata safari ya ghafla na kumuacha mtoto wake kwa jirani maana mfanyakazi hakuwepo alikwenda kuchota maji mbali kidogo. Mtoto yule akiwa kwa jirani alitoroka na kyurudi kwao. Na kwa kuwa milango ilikuwa wazi aliingia ndani na kukuta ndoo za maji zipo wazi. Mtoto yule akaingia kwenye ndoo zile na kupitiwa na usingizi. Dada mchota maji alipokuja hakuangalia vizuri kwenye ndoo akajaza maji na kuondoka kwa haraka ili akawahi foleni ya maji.


Mtoto mule kwenye ndoo alipiga kelele na kayanywa maji zaidi na hatimaye akapoteza maisha. Akaja dada wa kazi na kujaza ndoo ile kisha akaifung bila ya kuangalia nddani. Akazipandanisha ndoo kama tatu. Mama aliporudi alimtafuta mtoto kwa jirani bila ya mafanikio. Juhudi za kumtafuta ziliendelea ndani ya siku tatu bila hata kufanikiwa. Majirani wakamuonea huruma mwenzao na wakaamua kumpikia apate kula, wengine wakaanza kufua nguo zake na kudeki nyumba maana ndani ya siku tatu hakukuwa kukipikwa wala kufagiliwa wala kudekiwa.


Maji yalipobakia ndoo moja wakamkuta mtoto amshakufa kwenye maji. Mama yule kwa hasira alimpeleka mfanyakazi wa hakimu na hatimaye mfanyakazi akauliwa kwa kosa la kumuuwa mtoto kwenye maji na kumficha na ndoo. Kumbe mfanya kazi hana hatia maana ni mama aliyemzoesha mwanae kuingia kwenye ndoo na nikosa la jirani kutomuangalia vizuri mtoto. Kosa la mfanyakazi kuweka maji bila ya uangalifu. Hivyo nahofia kesi hii isijekuwa na mfanano na hii. Basi kwa haraka akaagiza waletwe wat wote wanaohusika mbele yake.


Watu wote wakapelekwa kwa mfalme pamoja na maiti wao. Falme akaanza kuuliza mmoja mmoja ataje amemuuwa vipi. Hapo mlevi akasema namna ambavyo tukio limetokea, kisha muuza nyama akaeleza tukio lilivyotokea kwa upande wake kisha tabibu kisha mshona nguo. Baada ya kiusikia maelezo ya kushangaza mfalme akaamuru habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Kisaha mfalme akauliza je kuna mwenye hadithi inayoshangaza zaidi ya hii ya kijana wangu huyu? Hapo mlevi akasema yeye ana hadithi ya kushangaza zaidi ya hii. Na akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-Pata kitabu Chetu Bofya hapa           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 412


Download our Apps
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰2 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰3 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO. Soma Zaidi...

SAFARI YA TANO YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TANO YA SINBAD Baada ya watu kukusanyika siku ilofata sinbad akaanza kusimulia stori ya safari yake ya tano. Soma Zaidi...

Safari saba za sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Soma Zaidi...

HADITHI YA MVUVI NA JINI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MVUVI NA JINI Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja. Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

TONGE LA MWISHO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KWISHA KWA CHAKULA Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Soma Zaidi...

Ndani ya pango la makaburi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...