Safari ya sita ya Sinbad

Safari ya sita ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad

SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Walipokusanyika watu wote akaanza kusimulia kuhusu safari yake ya sita. Nilipookoka na safari ya tano sikutamani tena kusafiri kwa njia ile. Hali hii haikudumu kwa muda mpaka nilipoamua kufanya safari ya mwisho kwani nilikuwa uymri umeshakwenda sana. Nikaamini kuwa faida nitakayoipata safari hii sitafanya safari nyingine yeyote ya majini. Basi nilianza kujiandaa kwa ajili ya safari hii. Hata hivyo maandalizi yalichukuwa muda kwani umri ulikuwa umeshakuwa mkubwa. Baada ya maandalizi safari ikaanza.

 

Safari hii ilikuwa mbaya sana, maana hata hatukuweza kupata siku mzima iliyo salama. Mara tuu baada ya kuanza safari kwa muda wa masaa kama nane kwa makadirio upepo uliharibika na kuwa mkali sana. Jahazi lilikuwa likipelekwa tusukokujuwa kwa muda wa siku tano. Siku ya sita upepo ulitulia katika sehemu ambayo hata hatuijui kabisa. Nahodha baada ya kuangalia zaidi eneo hili alilitukusanya karibu na akatuambia kuwa hapa tulipo tupo katika mkondo hatari sana baharini na hakuna jahazi lililokuja mkondo huu na kupona.

Ghafla maji yaendayo kwa kasi yakatuchukuwa na kutupeleka kwenye ufukwe wa kisiwa tusichokijua. Tulipofika pale nahodha akatuambia tuchuke sisi na mizigo yetu kisha akagawa chakula tulicho nacho sawa kwa sawa kwa kila mtu. Kisha akatuambia kuwa hapa tulipo hakuna upepo unaotoka kuelekea kokote. Maji yote yanavutwa kuelekea hapa. Na eneo hili kama mnavyoona lina mlima huu ambapo hata ukipanda sauti haitafika popote wala kusikiwa na mtu.

 

Kisha akatuambia kuwa hakuna yeyote atakuja kutuakoaa hapa hivyo maisha ya mtu kuishi yatategemea kuisha kwa chakula chake. Wakati anazungumza maneno yale mimi nilikuwa nawaza yalonikuta kule kwenye mapango. Basi hali ikawa hivyo kwa hakika hakuna pa kutokea. Nilizunguka kuangalia eneo li;le nikagunguwa kuwa kuna mto ambao umetokea mlimani kisha ukakunja bila ya kuingua baharini ukarudi upande wa bondeni kudogo pembeni mwa ufukwe na ukapotelea kwenye pango ililo jembaba

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views: 2316

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 web hosting     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Hadithi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya mke na kasuku

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo.

Soma Zaidi...
SAFARI YA PILI YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA PILI YA SINBAD Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi.

Soma Zaidi...
SAFARI YA KWANZA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA KWANZA YA SINBAD Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid.

Soma Zaidi...
SAFARI YA SITA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Soma Zaidi...