image

Siri ya wageni wale inafichuka

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA

Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Tulikuwa ni marafiki sana tukiwa katika umri wa miaka 7 mapka 18. baba yako alikuwa ni mchamungu toka alipokuwa mdogo. Alipata malezi mema sana. Na mimi nilivutiwa nikawa nirafiki yangu sana. Tulikuwa tukifanya ibada pamoja na karibia mambo yetu yote. Wakati nilipohama Misri kuja Yemeni niliweka ahadi na baba yako kuwa nikipata mtoto wa kike ataolewa na mtoto wake na akiwa wa kiume atauoa wako, na tulimuomba Mungu atutofaitishie watoto wetu, yaani akiwa wangu wakike wake wa kiume ama wake wa kike wangu awe wa kiume.

 

Miaka mingi ilipita hata tukasahau ahadi zetu. Mimi nilichelewa kupata mtoto na hata yeye. Hata hivi miaka yapata 17 iliyopita nikajiwa na wageni wa ajabu, kisha akataja kisha kama kile kilichomtokea baba. Kisha akaenelea kusema. Wageni wale walikuwa si watu wa kawaida. Ni wajumbe waliotumwa kuja kutukumbusha ahadi zetu na kutupatia habari njema za kaupa watoto. Siku ya mwisho walipoondoka wageni wale walinieleza kuwa mtoto wako atao;ewa na mtoto wa rafiki yako kaam ahadi. Atakuja mwenyewe, na utamjuaje wakaniachia pete hii iliyokufikia. Walinieleza kuwa pete hii ikifika mikononi mwako katu haitaondoka.

 

Wakanieleza kuwa sifa zako utakuwa ni muuza viatu. Hivyo binti yangu anayemsaidia kazi mke wangu nilimuagiza aje kwako kuuliza viatu kama walivyonieleza wageni wale sifa za viatu. Nikamueleza kama utamuona mtu aliyebadilika utambue huyo ni mtu ninaye mtafuta. Mwambie aje kwangu. Sasa nilikuwa na ugomvi na matajiri wenzangu waliotaka kumuoa binti yangu, niliwakatalia sana, na ndipo wakapanga njama ya mumuua.

 

Bila ya kutambua wakamuua yule mfanyakazi wangu wakidhani ndiye binti yangu. Baada ya tukio lile kutokea na pete kupotea bikajua kuwa pete imesafika kwa mwenyewe, maana wageni wale walinieleza katu ete isingeweza kuibiwa, ila itamfikia mwenyewe. Baada ya kumaliza kuzungumza akaniambia kuwa nisiendelee tena kuwatafuta wageni wale katu sitawaona. Akamuita binti wake nije nimuone.

 

Akaja binti mmoja akafunua sura yake. Nilihisi kama nimepigwa shoti kwenye mwili wangu. Ghafla joto likapanda, nilistaajabu kabisha kuona kuwa kumbe duniani kuana mabinti warembo kiasi kile. Nilijisemea kuwa wale waliotaka kumuoa hawakukosea katu. Kwa kweli binti alikuwa ni mzuri sana. Kisha mzee akasema “mwanangu nitakuozesha binti yangu bure ila kwa sharti kuwa uwe ni kama mwanangu”

 

Nilikubali na ndipo nikaozeshwa. Nilimuoa mke wangu nikiwa sina mkono mmoja. Bada ya harusi niliishi na mke wangu kwa muda wa miaka 5. kumbe kulikuwa na watu wananifanyia uaduni. Na ndipo wakanifanyia uchawi nikapata jini hili lililokuwa likinisumbua. Tulipata sifa zako ndipo tukaja Baghadad kupata matibabu. Ha hii ndio hadithi ya kukatwa mkono wangu.

 

Baada ya tabibu kusimulia hadithi hii akamuelekea Sulatani na kumuuliza “Je! Sultani hadithi hii haiwezi kuwa nzito kama kifo cha mtoa burudani?” mfalme akajibu angalau ila bado. Kama haitahadithiwa hadithi nyingine iatakayoshinda hii, wote mtapoteza vichwa vyenu. Basi hapo Mshona nguo akaja mbele na kusema “ Mtukufu nitasimulia kisa kilichomtokea huyu marehemu jana,kitakuwa ni cha kushangaza zaidi kuliko hadithi za wenzangu waliotangulia kusimulia. Akaanza kusimulia kama ifuatavyo           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1137


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya mjakazi wa Mfalme
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Soma Zaidi...

JARIBIO LA TATU LA A LADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza
Soma Zaidi...

ALADINI NA BINTI WA MFALME.
ALADINI NA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ujio wa wageni wa baraka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Historia ya pango, aladini na kitabu
Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi mwenyewe
Soma Zaidi...