image

Historia ya zamani

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

HISTORIA YA ZAMANI

Wale wazee wawili ulioowaona mmoja ndiye babu yako mzaa mama yako. Na mzee mwingine bila shaka unamfahamu kuwa ndiye mchawi uliyemsababishia kifo chake. Hawa wawili walikuwa marafiki sana. Waliiishi kaka mazingira ya kumtambuwa Mwenyezi mungu. Siku zote walikuwa ni watenda ibada. Siku zote walitii amri kutoka kwa wakubwa, na walikuwa ni wachapa kazi. Walipendelea kula kwa majasho yao. Urafiki wao ulidumu zoka wakiwa watoto hata walipokuwa ni watu wazima. Waliweza kuishi kwa amani na upendo na familia zao.

 

Jambo moja liliwasumbuwa kwa muda mrefu nalo ni kukosa utajiri. Mzee seifu alikuwa akimshawishi mzee Aladini ili waweze kwenda kwa waganga wapae utajiri. Kwa muda mrefu hatimaye mzee Aladini akashawishika na akakubali kwenda kwa mganga kwa sharti la kuwa wasikubali sharti lolote lakmuasi Mungu. Basi walianza kwa waganga lakini masharti yalikuwa ni yale yale ambayo ya kumuasi Mungu na kufanya sirki. Ila walifika kwa mganga mmoja aliyewaeleza kuwa watatakiwa walipie pesa wakabidhiwe pete na mshumaa. Hivyo vitawapa utajiri kwa haraka sana ila sharti moja tu wanatakiwa watoe sadaka ya kuchinja ng’ombe na kutoa nyama kwa watu bila ya sharti lolote.

 

Wazee hawa walikubali sharti hili. Basi wakajiandaa na kuchanga pesa na kumlipa mganga, wakatoa sadaka kama walivyoahidi na kukabidiwa mshumaa na pete. Mzee Aladini alipewa mshumaa na mzee sefy alipewa pete. Wakapewa maelezo namna ya kutumia vitu hivi. Basi mzee sefu haraka sana akaanza kutumia pete yake vyema na kuiamrisha mambo mengi na ya kiutajiri. Mzee sefu aliweza kuwa tajiri haraka sana hata watu wote wakaanza kumshangaa.

 

Kwa upande wake mzee Aladini akaenda mbali sana na kuanza kutengeneza lile pango. Hapo babu akamchukuwa tena Aladini hadi kwenye pango. Pale wakaanza kumuona mzee Aladini wakati huo kila alichofanya. Mzee aladini alikaa kwenye pango kwa nje na kumuomba mungu dua na kutaka kuwa utajiri wote wa mshumaa ule uje kuwanufaisha familia yake. Katika maombi yale mzee Aladini alithubut kuomba kuwa angepeda familia yake ijekuwa ni familia ya kifalme, na huu ndio utajiri hasa mzee Aladii alioutaka.

 

Mzee Aladini akiwa kwenye maombi jini wa mshumaa alitokea na kumueleza kuwa atahakikisha kuwa aliyoyataka mzee Aladini yanakuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Jini wa mshumaa akashukuwa karatasi ngumu ya ngozi na kuandika vitu flani kisha akaweka chini, sura ya binti mfalme ikatokea, na sura ya mfalme ikatokea. Hapo akamuhakikishia kuwa huyu ni Mfalme atakayekuwepo enzi hizo mjukuu wako Aladini atakapopata akii ya kuishi na familia. Ha huyu ndiye mfalme atakayeungana na ukoo wako.

 

Hapo jini wa mshumaa na mzee Aladini wakaanza kudisaini kila kitu kwa ajili ya maisha ya ukoo wa Aladini. Wakaweka kila kitu tayari ndani ya pango. Yaani kila ambacho Aladini alikiona kwenye pango kiliwekwa kwa sababu maalumu na kwa ajili yake na ukoo wake. Nyuki walioonekana ni wa dhahabu waliwekwa kwa ajiliya kuinda mafuta ya mshumaa, yale mauwa na miti ya matunda ya madini ilikuwa ni utajiri wa zamani sana uliohifadhiwa kwnye mapango toka Mfalme Suleimani alipofariki. Utajiri huu ilibidi uhifadhiwe ili ujeleta manufaa kwa vizazi vijavyo. Jini wa mshumaa alikuwa ni miongoni majini waliohudhuria mkutano uliopitisha wazo hilo, hivyo naye akabeba utajiri kuuhifadhi. Basi babu akaanza kumueleza Aladini maana ya kila kilichopo kwenye lile pango na jinsi atakavyoweza kutumia.

 

Baada ya kupata maelezo babu alimchukuwa Aladini na kumrudisha kwa mzee seif. Huku mzee seif utajiri wake uliongezeka na kuwa mkubwa. Baada ya masiki kadhaa akaanza kuwa mjeuri na asimkumbuke tena mwenyezi mungu. Alikuwa na kibri na dharau sana. Hata rafiki yake hakumkumbuka tena. Ilitokea siku moja akatoa kashifa na kumtuka na mzee mmoja, hali ile ilimfanya apate laana. Ilipofika usiku jini wa pete akamtokea na kumueleza kuwa hawezi tena kuendelea kuanya kazi, kwani amepigwa marufuku na jini wa mshumaa. Maana ni mkubwa kuliko yeye. Basi toka siku hiyo utajiri wa mzee sefu ukaanza kuporomoja.

 

Mzee Aladini hakuchukuwa muda mrefu aakanza kuumwa. Mzee sefu alikuwa akimuomba amkabidhi mshumaa lakini alikataa katu. Mzee Aldini akamueleza jini wa mshumaa ahakikishe analinda pango vyema. Mzee Aladini aliacha mtoto wa kike tu ambaye hakufahamu chochote kuhusu pango lile. Mzee Aladini alifariki dunia. Baada ya kufariki mzee Sefu alihangaika sana kujuwa wapi mshumaa umewekwa. Siu moja alishangaa kuona ukuwa jini wa pete alimjia. Na hapoa akamueleza kilakitu na namna ya kuingia kwenye pango.

 

Alimueleza kuwa hatoweza kuingia mwenyewe, ni lazima ampate Mjukuu wa mzee Aladini ama kijana ambaye hajajuwa mwanamke. Na anatakiwa afie pangoni na asishike kitu kingine ama kuiba chochote. Utajiri wa mzee Seifu uliporomoka na kuisha ijapokuwa jini wa pete alikuwa akija lakini hakuweza kumsaidia kupa utajiri kwa chochote. Pete sasa iliweza kumsaidia kujuwa wapi pangolilipo basi. Aliendelea kutafuta vijana wa kuingia pangoni bila mafanikio. Mzee seifu alibaki kuwa masikini tena na akahama mji kwa kuhofia udhalilifu. Na akaanza kujifunza uchawi huku akisaidiwa na pete yake mara moja moja.

 

Maisha yaliendelea hata binti wa mzee Aladini akaolewa na Mzee Mustapfa. Na baadaye aakazaliwa Aladini. Mzee Seif alipata habari za kuzaliwa Mjukuu wa mzee Aladini. Alifurahi maana alijuwa ni yeye tu ndiye anayefahamu siri ile ya pangoni; na hapo ndipo mambo yale yalipoanza utokea. Babu aliendelea kumsimulia mambo mengi na akamuelekeza pia yalipo mampango mengine ya utajiri. Alimueleza kuwa kwenye kabati ndani ya pango kuna ramani a kuyafikia mapango hayo. Mzee akampeleka Aladini maeneo balimbali kisha akamrudisha kwenye ule uwanja.

 

Aladini alipofika kwenye uwanja akaanza kuona kiza kianaanza kuingia kidogo kidgo kama mlango umafungwa na hatimaye kiza kinene. Anafumbua maho ypo kwenye kiti na kile kitabu hanacho tena. Ilikuwa ni usiku wa manane. Alipofika ndani kwake alimkuta mke wake analia sana. Alidhani mumewe amepatwa na ajali ana amepotea maana si kawaida kuchelewa ivi. Aladini hakumficah mkewe kitu akamueleza kila kitu na mkewe akaridhika. Wakalala na maeisha mengine yakaendelea





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1382


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

UGENI WA DHATI
Soma Zaidi...

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI
Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEMA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI
Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaa wa tatu
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi mwenyewe
Soma Zaidi...

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaka wa pili
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...