Kukatwa mkono na kuurithi utajiri

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

KUKATWA MKONO NA KURITHI UTAJIRI

Basi niliweza kulala kwa mke wangu siku ile na asubuhi nilimuashia kipande 1000 vya dhahabu na kuondoka kuelekea dukani. Jioni niaenda tena kwa mkewangu nikalala na asubuhi jikamuachia vipande 1000 vya dhahabu na kuondoka. Niliweza kufanya hivi kwa muda hata nikafiisika mali yangu yote ikiisha. Nikiwa sina kitu, huku nikiamini kama nitaenda mikono mikavu nitaingia aibu katika familia ya kitajiri.

 

Nikiwa na mawazo kama hayo mara nikaona sehemumoja kuna msongamano wa watu. Nikasogea karibu nakukuta kuna watu wanapigana. Katika kusogea zaidi mara bikaona mama mmoja ameweka vipande vingi vya dhahabu kwenye kikapu chake kisha amefunika kwa kanga kuukuu. Basi nikasema leo ninaiba nipate kumliwaza mke wangu. Nilisogea karibu na kuingiza fumba la kwanz ana kutoa vipande kama kumi.

 

Nikaingiza tena mkono na kupata vipande 5 nikajisemea hivi vinatosha. Wakati nataka kuondoka yule mama akashibuka na kuniona. Hapo akaniitia kuwa ni mwizi na haikupita muda nikawekwa mbaroni. Nilijitetea na ndipo nikapelekwa kwa kadhi. Nikasachiwa na kukutwa na vipande vya dhahabu. Basi kadhi akahukumu nikatwe kiganja cha mkono kwa mujibu wa sheria za kiislamu.

 

Nilikatwa mkono na kupoteza fahamu. Kuja kushituka nipo sehemu ya mbali nimetupwa. Niliweza kujikongoja hata nikafika kwa mke wangu. Nikaufunga mkono wangu ili asiuone. Niliishia kulala na kumueleza kuwa ninaumwa. Kilipokuja chakula nilikulwa kwa moko wa kushoto. Kitebdo hiki kilimuuuma sana ndipo akataka kuona nini kipi kwenye mkono wangu wa kulia. Nilimueleza kuwa nina jipu ila hakutaka kuniamini.

 

Alinifungua na ndipo akaanza kuli sana. Basi nikamueleze akila kilichotokea bila hata kuficha kuwa kwa ajili yake nilikusudia kuiba na nikaiba ila nikakamatwa na kukatwa kiganja cha kulia. Basi alilia sana kisha akasema “ kwa ajili yangu umekatwa mkono, ulidhani nimekupenea pesa” basi akaagiza aletewe mashahidi wawili ndipo walipokuwa akawaambia washuhudiie kuwa mali za ke zote ni za kwangu, alioroshesha mali nyingi sana, mashamba na majumba mengi yaliyopo mjini. Alipo maliza kuoroshesha akaweza muhuri wake na hati ile ya makubalian ikapelekwa kwa baba mkwe naye akaikubali.

 

Kila kitu kilivyokuwa sawa aliwalipa mashaihidi na kisha akanichukuwa mpaka kwenye stoo. Huko nikakuta kuna mamia ya masanduku yaliyojaa dhahabu na fedha nyingi. Sanduku moja lilifumikwa kitambaa cha kijani na kuandikiwa kwa lugha ya kiarabu cha asili. Sikuweza kutambua maana yake. Ndip akanieleza kuwa kumeandikwa “kwa kipenzi changu” akanieleza fungua. Loo! Nilipofungua nilikuta vipande vyote vya dhahavu nilivyompa vipo pale kama vilivyo.

 

Akanieleza kuwa Mwenyezi Mungu amekurudishia mali yako na kukupa ziada, na kukupa mke mwema. Hapo nilimkumbatia mke wangu na kumbusu katikati ya paji lake. Mmhmmmh….(rahaaa). basi nilianza kuendeleza mali za mkewangu tukiwa pamoja. Tuliweza kuishi mika 10 na kubahatika mtoto mmoja wa kike. Miaka mitatu iliyopita mkewang aliumwa na kufariki.

 

Hivyo kwa ubize niliyokuwa nao ndipo hata nikashindwa kuchukuwa pesa yangu iliyo kwako. Na hii ndio hadithi yangu ya kukatwa mkono. Usidhani nilikula kwa mkono wa shoto kwa kupenda ama majigambo. Baada ya kijana mtanashati kumaliza kuzimulia kisha chake akanieleza kuwa, je ungependa yuende wote Baghadad kibiashara?. nami nikakubali.

 

Wiki ilofata ndipo tuakaanza safari ya kuja Baghadad. Tulifanya bishara na muda wa kurudi ulipofika mwenzangu alirudi ila mimi nikamueleza kuwa nitaendelea kuishi hapa. Akanieleza nitakaporudi Misri nimpe taarifa maana binti yake atakuwa amefikia kuolewa, hivyo angependa niwe mkwe wake.

 

Basi niliweza kuishi hapa Baghadad ni mpaka yakatokea haya yaliyotokea leo. Kijana mlevi aliyvyomaliza kusimulia akamwambia mfalme “Je! Hadithi hii si yenye kustaajabisha kuliko hadithi ya kifo cha mtoa burudani wako?” hapa mfalme akasema hapana bado haijafikia kuweza kuachiwa huru wauhumiwa wa kesi hii. Hapo mjakazi wa Mfalme akaja mbele na usema, nina hadithi ya yaliyotokea kumuhusu huyu aliyekufa, haya yalitokea jana. Naomba nisimulie kama itakuwa na uzito zaidi ya kisa hiki ninaomba watuhumiwa wawachwe huru. Hapo mjakazi wa mfalme akaanza kusimulia hadithi ifuatayo



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 975


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya tano, baada ya bibi kuachana na mke mdogo wa mfalme alienda kwa kijana wa kiume wa mfalme na kuona udhaifu wake kwamba anapenda sana mali. Soma Zaidi...

Safari ya tatu ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Safari ya kwanza ya sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tano wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hatima ya kijana mchonganishi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

TAMBUA FAIDA NA ATHARI ZA MICHEZO
POSti hii inahusu kwenye michezo na burudani.michezo ni kile kitu ambacho unakifanya kwa ajili ya kujifuraisha wewe mwenyewe.pia na watu waliokuzunguka.tukiangalia michezo anaweza kucheza mtu yeyeto yule kwa sababu michezo haina ubaguzi. Soma Zaidi...