Familia mpya baada ya harusi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI:

Aladini akiwa mbele ya mfalme alionekana kuwa ni mtoto mtiifu sana na ni wa kipekee anayestahiki kuwa mkwe wa Mfalme. Hali hii ilimfanya mfalme kuridhika sana na chaguo lake na maamuzi. Mfalme alihisi kuwa waziri alikuwa akimpeleka mbali hasa kutaka kumuozesha mwanaye kwa kumchafulia aladini. Japo mfalme alikuwa na mambo anataka kuyafahamu kuhusu Aladini amepata wapi utajiri ule, na ni nani hasa. Mfalme aliamini kuwa ipo siku Aladini atamueleza yeye mwenyewe ama ipo siku atakuja kutambua. Basi kwa bashasha na mapenzi Mfalme akasalimiana na mkwe wake pamoja na mwanaye kipenzi.

 

Watatu hawa wakakaa kwenye viti hali ya kuangaliana. Viti vilivyopambwa vyema katikati ya bostani la Mfalme ndani ya ikulu. Viti vilikuwa juu ya yasi za kijani sana kwa ubichi, zilipendeza mno. Maua mazuri yenye rangu za kuvutia. Bostani lilijawa na harufu nzuri ya maua na wadudu walioonekana kupendezesha sana wakiwa wanakula nta ya maua. Nyuki wakubwa wa rangi ya njano utadhani ni dhahabu zilizokuwa zikipepea. Nyuki hawa walimkumbusha sana Aladini alipokuwa pangoni. Mfalme alikuwa muda wote mwenye furaha alipomuangalia Aladini mkwe wake. Binti Mfalme alipatwa na wivu kuona sasa mapenzi ya baba yanahamia kwa Aladini. Baba hamuangalii tena mwanaye kwa upendo kama zamani. Ila aliamua kupotezea kwani alianimi Aladini ni mwe tu kwa vyovyote vile.

 

Wajakazi waliovalia vyema walikuja mbele na kuweka vyakula laini kwa ajili ya kufungulia kinywa. Ukimya ulitawala kwa muda huku Aladini akiangalia kwenye mjengo ulioonekana ni mgeni kwenye mji. Wajakazi walipomaliza kutenge vyakula binti Mfalme akahakikisha kila kitu kipo salama kwa ajili ya Mume wake kipenzi. Mjakazi mkuu wa Mfalme aliyeonekana kuwa na sura nzuri na umbo la kuvutia, naye alikuja kuhakikisha usalama wa chakula cha mfalme. Wote waliwakaribisha mabosi wao na tayari kula.

 

Wakiwa tayari kula mfalme alivunja ukimya uliotawala kwa muda mrefu. “aladini mwanangu, karibu sana, na kuwa huru” “ahsante sana baba, nimefurahi sana, pia ninafuraha zaidi kuwa na mwanao” “mmh mume wangu, mpkaka unitaje” “hahaaa mwanangu kutajwa si ndio upendo” “mmmh Ahsante sana mume wangu kipenzi” “nafurahi sana kama wanangu mnapendana hivyo “Ahasante sana baba” yalikuwa ni mazungumzo machache kati ya watatu hawa.

 

Walianza kuzungumza mazungumzo ya hapa na pale, huku wakiendelea kula, na kukisifia chakula. Binti mfalme alionekana mvivu sana wakula huku akitumia muda mwingi kumuangalia Aladini jinsi anavyokata matonge. Aladini alitambua hilo na alihitaji wamtambue kuwa katika kula hanaga uvivu. Wakiendelea kula Aladini alimueleza Mfalme kuwa jumba Analoliona ni jumba lake hivyo anatarajia leo kuhamia yeye na mkewake kwenye jumba lao.

Mfalme alishikwa na taharuki na mshangao mkubwa, kuona kuwa Aladini si tu ni mtanashati bali pia ni kijana Tajiri. Basi waliendelea kuzungumza kisha Aladini na mkewake wakaondoka waende kujiandaaa kwenda kuona nyumba yao mpya. Mama Aladini alishawai kwenda kuhakikisha kuwa mambo yote yapo safi, mama alikwenda kuhakikisha kuwa vitanda na thamani za ndani vipo sawa. Mama alistaajabishw akuona jumba lote lipo sawa kasoro dirisha moja tu. Mama alijuwa lamda vifaa vya yjenzi vilikwisha. Alichokifanya ni kwenda mjini kutafuta mafundi kwa gharama yeyote kutengeneza dirisha. Lakini Loo! Walishindwa kabisa. Mwishowe mama aladini aliwaruhusu mafundi waondoke na akawalipa kwa uchache kutokana na kazi waliofanya.

 

Msafara mkubwa wa Aladini na mkewake ukaanza kuondoka. Mfalme aliahidi atakuja siku itakayofata, alimsisitiza binti yake aishi salama na mume wake. Aladini akiwa kwenye gari la kuburuzwa na farasi gari lililopambwa kwa vipambio vilivyo vizuri sana na magodoro malaini. Ndani aladini na mkewake walikuwemo. Farasi waliowapanda wallionekana kuwa wamenona sana na waliopendeza. Walikuwa na viatu vigumu vya rangi sawa. Msafara huu ulifatiwa na kundi la wajakazi wa kiume na kike. Inafikia idadi yao watu 52, wote wakiwa katika mavazi mazuri kama vule wanakwenda kumpokea mgeni wa thamani.

 

Msafara kila ulipopita mjini watu hawakuwacha kumtaja Aladini huku wakitaja hasa utajiri wake. Aladini alipata kutajwa zaidi hata kuliko mfalme. Mama Aladini alipopata habari kuwa Aladini sasa anakuja alipanga watu wake tayari kuwakaribisha kwenye jumba kubwa la kifahari. Hakika Aladini alikuwa ni tajiri hasa, utajiri usiowezakufananishwa katika historia ya nchi. Utajiri ambao chanzo chake haujulikani ijapokuwa pia mwisho wake upo matatani kwani kila mtu alianza kutafuta siri ya mafanikioa ya Aladini. Sambamba na watu hawa waziri mkuu ndiye aliyekuwa adui mkubwa wa Aladini. Alisafiri hasa kwa lengo la kujuwa undani wa ladini na namna ya kumpindua.

 

Baada ya mwendo wa muda msafara ukafika kwenye jumba la Aldini. Aladini mwenyewe alistaajabu kwa uzuri wa jumba lake. Ijapokuwa aliona jumba lile kwenye maono lakini hakuamini kama litakuwa zuri kisi hiko. Aladini alikaribishwa na dirisha moja amablo halikuweza kumaliziwa. Aladini alifurahi kweli, maana alitambuwa kuwa alifanya hivi kwa makusudi. Kundi kubwa lilionekana kustaajabu sana kwani katika mji kusikngeweza kupatikana fundi aliye hodari. Jumba lilikuwa zuri hata kama utaanza kulielezea katu hutamaliza



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1050


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Mtoto wa Tajiri na maskini ( sehemu ya kwanza)
Post hii inahusu hadithi fupi tu kuhusu mtoto wa tajiri na maskini, palikuwepo na watoto wawili mmoja akiwa mtoto wa tajiri na mwingine wa maskini. Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)
Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini. Soma Zaidi...

Siri ya kifo yafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani. Soma Zaidi...

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Safari ya tatu ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya. Soma Zaidi...

Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...

Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara. Soma Zaidi...