image

Dua sehemu ya 04

Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua

Dua sehemu ya 04

BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU.
Hizi ni dua ambazo zimekusanya mambo ya duniani na akhera. Yaani muombaji dua hizi atanufaika kwa mambo ya kidunia na akhera. Dua hizi ni zenye kujibiwa na hazichagui muda. Nidua ambazo zinaombwa wakati wowote ule. Hizi ni dua ambazo Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa akizipenda sana kuzitumia.

1.Dua ya kuomba kheri duniani na akhera. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa akioma sana dua hii “ALLAHUMMA RABBANAA AATINAA FII DUNIYAA HASANA WAFIL-AAKHIRAT HASANA WAQINAA ‘ADHAABAN-NAARI” (amesimulia Bukhari,Muslim na Abuu Daud).

2.Dua za kutaka maghafira (msamaha). Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم akiomba dua hii “ALLAHUMMA IGHFIR LII KHATWII-ATII, WAJAHLII, WAISRAAFII FII-AMRII, WAMAA ANTA A’ALAMU BIHI MINNII. ALLAHUMMA IGH-FIR LII JUDDII, WAHAZLII, WAKHATWAII, WA’AMDII, WAKULLA DHALIKA ‘INDII. ALLAHUMMA IGH-FIRLII MAA QADDAMTU, WAMAA AKHARTU, WAMAA ASRARTU, WAMAA A’ALANTU, WAMAA ANTA A’ALAMU BIHI MINNII. WA ANTAL-MUAKHIRU, WAANTA ‘ALAA KULLI SHAI-IN QADIIR” (amepokea Bukhari).

3.Dua ya kuomba rehma na rizki. Amesimulia Sa’ad رضىالله عنه kuwa alikuja mtu mmoja kwa Mtume akamwambia ewe mtume nijulishe maneno niwe ninayasema. Mtume akamwambia sema “LAA ILAAHA ILLA LLAHU WAHDAHU LAA SHARIKA LAHU. ALLAHU AKBARU KABIIRAA WAL-HAMDU LILLAHI KATHIIRAA WASUBHAANA LLAHI RABBIL-’ALAMIINA LAAHAULA WALAA QUWATA ILLAA BILLAHIL-’AZIZIL-HAKIIM” akasema Mtu yule kumwambia mtume صلّي الله عليه وسلّم “maneno haya ni kwa ajili ya Allah je! Ni yapi yatakuwa kwa ajili yangu? Mtume صلّي الله عليه وسلّم akamwambia sema “ALLAHUMMA IGH-FIR LII WARHAMNII, WAHDINII WARZUQNII” (amepokea muslim).

4.Dua ya kujikinga na upotovu. Amesimulia Ibn ‘Abas رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa akisema “ALLAHUMMA LAKA ASLAMTU, WABIKA AAMANTU, WA’ALAIKA TAWAKALTU, WAILAIKA ANABTU WABIKA KHAASWAMTU. ALLAHUMMA INNII A’UDHUBIKA BI’IZZATIKA LAA ILAAHA ILLA ANTA AN TUDHWILLANII ANTAL-HAYUL-LADHII LAA YAMUUTU WALJINNU WAL-INSU YAMUUTUUNA”. (amepokea Muslim).

5.Dua ya kutaka hifadha kwa Allah katika mambo ya dunia na akhera. Amesimulia Ibn ‘Abas رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم akiomba dua (hii): “RABBI A’INNII WALA TU’IN ‘ALAIYA WANSURNII WALAA TANSUR ‘ALAIYA WAMKUR LII WALAA TAMKUR ‘ALAIYA WAHDINII WAYASIRIL-HUDAA LII WANSURNII ‘ALAA MAN YUGH-NII ‘ALAIYA. RABBI IJ’ALNII SHAKRAA LAKA DHAKAARAA WAHAABAA LAKA MUTWAWAA LAKA MUKHBITAN ILAIKA AWAHAN MUNIIBAA. RABBI TAQABBAL TAUBATII WAGH-SIL HAUBATII WAJIB DA’AWATII WATHABIT HAJATII WASADID LISAANII WAHADI QALBII WASLUL SAKHIIMATI SWADRII”. (amepokea Tirmidh na Abuu daud kwa isnad sahihi).

6.Dua ya wakati wa kulala na kuamka.amesimulia Abuu Dhar رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم pindi anapotaka kulala usiku huweka mkono wake chini ya kitefute chake kisha husema “BISMIKALLAHUMMA AHYAA WA AMUT” na anapoamka husema “ALHAMDU LILLAHI LADHII AHYAANAA BA’ADA MAA AMAATANAA WAILAIHN-NUSHUUR”. (amepokea Ahmad Bukhari na musmlim).

7.Dua wakati wa kuvaa nguo. Amesimulia Ibn Sa’id رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapovaa nguo au kanzu au msuli au kilemba husema “ALLAHUMMA INNII AS-ALUKA MIN KHAIRIHI WAKHAIR MAA HUWA LAHU WA A’UDHUBIKA MIN SHARI WASHARI MAA HUWA LAHU”

8.Dua wakati wa kutoka nyumbani. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم Mwenyekusema pindi anapoingia nyumbani kwake “BISMILLAHI TAWAKALTU ‘ALAA LLAHI WALAA HAULA WALAA QUWATA ILLAA BILLAH” huambia “umetoshelezewa, umeongozwa na umekingwa na shetani” (amepokea Abuu Daud n Tirmidh).

9.Dua wakati wa kuingia nyumbani amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa Mtume alimwabia “ewe kijana changu utakapoingia kwa ahalizako (nyumbani kwako) salimia (yaani toa salamu ‘ASALAAMU ‘ALYKUM WARAHMATUL-LLAHI WABARAKAATUH’) itakuwa ni baraka kwako na kwa ahalizako”. (amepokea Tirmidh).

10.Dua ya wakati wa kuingia chooni. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapoingia chooni husema “BISMILLAHI ALLAHIMMA INNII A’UDHUBIKA MINALKHUBUTH WALKHABAAITHI”. (amepokea Bukhari Muslim).

11.Dua wakati wa kutoka chooni. Amesimulia ibn ‘Umar رضىالله عنه kuwa alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapotoka chooni husema “GHUFRAANAKA ALHAMDU LILLAHI LLADHII ADH HABA ‘ANNIL-ADHA WA’AF ‘ANNI” (amepokea Tirmidh na Abuu Daud).

ADHKARI MBALIMBALI NA DUA Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari. Tutajifunza pia na faida zake kama Mtume صلّي الله عليه وسلّم alivyozungumza na masahaba zake.

1.amesema Mtume"‏ أَفْضَلُ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ ‏"‏ “bora ya dhikir ni kusema Lā ilāha illallāh na bora ya dua ni kusema Al-ḥamdulillāh” (amepokea Tirmidh).

2.Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَا مِنْ عَبْدٍ يَقُولُ فِي صَبَاحِ كُلِّ يَوْمٍ وَمَسَاءِ كُلِّ لَيْلَةٍ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الأَرْضِ وَلاَ فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ فَيَضُرُّهُ شَيْءٌ ‏" “Mja yeyote atakayesema ‘Bismillāh, alladhi lā yaḍurru ma`a ismihi shai'un fil-arḍi wa lā fis-samā', wa huwas-Samī`ul `Alīm’ mara tatu kila asubuhi na jioni hatadhuriwa na kitu chochote” (Amepokea Tirmidh).

3.mtume amesema "‏ مَنْ قَالَ حِينَ يُمْسِي رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا وَبِالإِسْلاَمِ دِينًا وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُرْضِيَهُ ‏"‏ “Mwenye kusema jioni ‘Raḍītu billāhi rabban wabil-Islāmi dīnan wa bi-Muḥammadin nabiyyan’ itakuwa ni haki kwa Allah kumridhia” (Amepokea tirmidh).

4.Mtume alimwambia al-baraa IBN ‘Aazib kuwa “أَلاَ أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ تَقُولُهَا إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَإِنْ مُتَّ مِنْ لَيْلَتِكَ مُتَّ عَلَى الْفِطْرَةِ وَإِنْ أَصْبَحْتَ أَصْبَحْتَ وَقَدْ أَصَبْتَ خَيْرًا تَقُولُ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ لاَ مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ ‏"‏ ‏ “je nikufundishe maneno utakayoyasema pindi atakapoliendea tandiko lako (kulala) na kama utakufa utakufa katika fitrah (uislamu) na ukiamka asubhi utakuwa umepambaukiwa katika kheri? Utasema ‘'Allāhumma innī aslamtu nafsī ilaika wa wajjahtu wajhī ilaika, wa fawwaḍtu amrī ilaika, raghbatan wa rahbatan ilaika wa alja'tu ẓahrī ilaika, lā malja'a [wa lā manjā] minka illā ilaik. Āmantu bikitābikal-ladhī anzalta wa binabiyyikal-ladhī arsalt’ (Amepokea Tirmidh).



         › WhatsApp ‹ Whatsapp





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 364


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

DUA YA MUUMINI NA DUA YA KAFIRI
DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI. Soma Zaidi...

Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana
12. Soma Zaidi...

DUA 41 - 50
41. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa salamu katika uislamu
MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu Soma Zaidi...

Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo
Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu. Soma Zaidi...

DUA ZA WAKATI WA HASIRA
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA. Soma Zaidi...

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 42: Ewe Mwana Wa Adam, Utakaponiomba Na Kuweka Matumaini Kwangu Basi Nitakusamehe
Soma Zaidi...

KUKUSANYIKA KATIKA DUA
KUKUSANYIKA KATIKA DUA. Soma Zaidi...

NAMNA AMBAZO DUA HUJIBIWA
NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA. Soma Zaidi...

kuwa muaminifu na kuchunga Amana
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Soma Zaidi...

Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 2: Ujio wa Jibril kwa Mtume (s.a.w)
Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy Soma Zaidi...