Simulizi za Hadithi EP 8 Part 3: Kijana mchonganishi
Muendelezo....
HATIMA YA KIJANA MCHONGANISHI
Mansur akaondoka haraka akiwa na majozi sana huku akiwaza nitampata wapi kijana huyu. Mansur alijisemea, Mungu aliyeniokoa na janga la kwanza ataniokoa na hili la pili. Mansuri alipofika kwake aliwaeleza kla kitu, na akabakia kwake kwa siku tatu bila kwenda kokote. Manzur ilipofika siku ya tatu akajiwa na mjumbe kutoka kwa khalifa kuwa anahitajika akiwa na muhalifu ama ajiandae kwa kifo. Mansur akaanza kuagana na famiia yake na kuacha usia.
Kabla ya kuondoka mwanae mdogo aliyekuwa akimpenda sana alikuja kumkumbatia baba yake kama ishara ya kuagana. Mansur wakati akimkumbatia mwanaye alihisi ugumu kwenye tumbo la mwanaye. Akamuuliza ameweka nini. Mtoto akajibu kuwa nimeweka tunda epo nimepewa na Manyakazi wetu, alikuwa hataki kunipa eti amemnyang’anya mtoto wa watu ambaye baba yake amekwenda mbali kununua maepo matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabu.
Mansur aliposikia habari hii alifurahi sana na kusema ssa nimeokoka. Hapo akamchukuwa mfanyakazi wake na kwenda naye kwa khalifa. Kijana akaulizwa na kukirikonsa. Khalifa akaagiza habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na ihifadhiwe kwenye kumbukumbu ya nyaraka za kushangaza na kutisha. Kisha waziri Mansur akasema ewe khlifa ninakiri kuwa mfanyakazi wangu amepatwa na hatia. Ila ninakuomba kuwa nitakusimulia kisa cha kushangaza zaidi ya hiki, na endapo utakirikuwa kimeshangaza zaidi naomba iwe fidia umuache huru mfanyakazi wangu.
Khalifa alikubaliana na maneno haya na hapo Mansur akaanza kusimulia hadithi ya Badrudin.
Tukutane kitabu cha tatu hadithi ya badrudin
Huu ndio mwisho wa kitabu cha pili hadithi za Alif lela u lela. Usiwache kuwa nasi tukutane kitabu cha tatu. Kama unahitajikitabu cha kwanza na pili wasiliana
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu
Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza....
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.....
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 5 Part 7: Sehemu ya nne ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.....
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 1 Part 1: Simulizi ya kiapo cha Sultan
Simulizi hii inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadidhi za HALIF LELA U LELA.
Soma Zaidi...