image

Simulizi za Hadithi EP7  Part 17: Jaribio la tatu kwa Aladini

Muendelezo....

 

JARIBIO LA TATU LA A LADINI

 

 

 

Baada ya yule mchawi na waziri kushindwa kufanikisha wazo lao, sasa mchawi aliamua kuanza kutafuta mbinu mbadala. Mcawi alitambua kuwa endapo ataweza kumiliki kitu chochote kutoka kwenye lile pango ataweza kufanikisha mpango wake wa kulipiza kisasi cha kaka yake. Mchawi yule akaenda mjini kwa bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Hawiya. Hawiya alikuwa ni bibi mchamungu sana ambaye alikuwa akiwaombea watu dua na kukubaliwa maombi yake. Watu wa mjini waliamini kuwa Hawiya ni mwanamke aliye karibu na mungu sana. Kwa maana hiyo mchawi akaenda kwa hawiya na mumuuwa, kisha akachukuwa sura yake.

 

 

Kwa sura ya Hawiya Mchawi aliweza kufika nyumbani kwa Aladini. Alivizia wakati ambao Aladini hakuwepo nyumbani. Alipofika akajifanya anaombea watu dua na hatimaye akataka kuombea nyumba ya Aladini na familia yake. Mke wa Aladini alifurahi sana kumuona bi Hawiya na alipenda aiombee nymba na ndoa yao iwe na upendo endelevu. Bila ya kufahamu kinachoendlea kuwa yule sio hawiya. Mchawi akiwa katika sura ya hawiya akaanza kuomba dua. Aliweza kutumia nguvu za kichawi kuwashawishi watu kuwa kweli yeye ni Hawiya Mchamungu. Aliweza kutumia viini macho na kuonyesha miujiza mikubwa.

 

 

Wakati anamuombea Binti Mfalme mchawi alitumia mazingaombwe na kumfanya binti mfalme aone mambo ya baadaye. Akiwa katika hali hiyo binti Mfalme alimuona Aladini akiwa katika mavazi meume sana, huku ameongozana na kundi la watu. Alipochunguza kwa umakini aligunduwa kuwa Aladini anakwenda kuoa mke wa pili. Moyo wa binti Mfalme uliruka kwa wivu na hasira. Alipokuja kushituka kumbe alikuwa anaota. Uchawi uliweza kufanya kazi vyema na sasa binti mfalme alianza kupata wasiwasi kuwa ipo siku Aladini ataoa.

 

 

Mchawi akaanza kuingiza maneno hapo hapo, “inaonekana huna amani na ndoa yako, kuwa mumeo ataoa kke wapili, nitakusaidia kitu kumsahaulisha hizo fikra kabisa” nitashukuru sana jamani mamaangu” “usijali mwanangu nitakusaidia, ila sharti ni moja tu” ni lipi hilo mama kipenzi” “upate mafuta ya mshumaa wa kale, mafuta hayo yamehifadhiwa kwenye pango la ajabu kwenye yai la ajabu pia ni lazima ayalete mumeo mafuta hayo” mama yakipatikana nitafanikiwa kweli maana nampenda sana mumewangu Aladini” “ndio nakuhakikkishia utafanikiwa kabisa”. haya yalikuwa ni mazungumzo ya Hawiya na binti Mfalme.

 

 

Basi binti Mfalme akampatia chumba bi Hawiya awezekukaa pale kwa muda wa siku tatu mpaka mafuta yatakapopatikana. Aladini siku hiyo alirudi jioni na hakuwa na muda wa kukagua ndani. Usiku alipata chakula na kupumzika. Bint Mfalme akaanza kuzungumza maneno matamu kwa mumewe. Lengo lake ni kumvutavuta ili aweze kumletea mafuta ya ajabu. Katika mazungumzo ndipo akayataja afuta ya ajabu na akahitaji aletewe na yeye ayajuwe. Aladini aliposikia hivyo alitambua kuwa hapa kuna kitu. Hakutaka kumchafulia fikra mkewe, hivyoa akamuahidi kumtekelezea haja yake. Binti mfalme siku iyo alilala na furaha sana.

 

 

Ilipofika asubuhi Aladini alianza kufanya uchunguzi wake. Na akagunduwa kuwa kuna mwanamke mgeni amelala hapa ndani. Kwa kutumia mshumaa wake Aladini aliweza kutambuwa kuwa huyu ni yule mchawi. Aladini alicukuwa upanga wake na kwenda kumkata kichwa chake mchawi. Na hapo hadithi ya mchawi ikaisha. Waziri alipozipata habari hizi alirudi kwa Aladini kuomba msamaha. Aladini aliakubali kumsamehe waziri kwani hakuna ubaya wowote aliyomfanyia zaidi ya kushirikiana na mchawi.

 

 

Baad ya matukio haya Aladini alitambuwa kuwa ipo siku atatokea mchawi mwingine ama jini aliye mkubwa kuliko yule wa mshumaa. Na ataweza kumnyang’anya mali ama kuzipeleka kwenye mikono mibaya. Aladini aliamini njia pekee ni kuzudisha mali alizo nazo kwa wenyewe koo za majini. Aladini alimuita jini wa mshumaa na kumueleza wazo hiyo naye akakubaliana. Aladin alitumia mshumaa kwa mara ya mwiho kuwa na stoo ya madini mengi yenye thamani, dhahabu, ilijaa chumba kizima, Almasi na madini mengine mazuri. Kisha alilima shamba kubwa na kuweka wafanyakazi. Aladini alifanya mambo kadhaa kama vitega uchumi vyake. Kwani alianza kuiandaa kuishi maisha ya amani bila ya kuwa na pete wala mshumaa.

 

 

Aladini alipojirishisha kila kitu akamakabidhi jini wa mshumaa pete na mshumaa. Ijapokuwa jini wa mshumaa hakutaka kutengana na Aladini ila hakuwa na budi, na aliahidi kumsaidia Aladini muda wowote atakapokuwa na shida. Alipata kumueleza naman ya kukutana naye.baada ya makabidhiano hayo Aladini alilala kwa Amani siku hiyo. Ilipofika asubuhi alikwenda pangoni kushuhudia kilichoendela. Loo hakukuta kitu zaidi ya msitu. Hapo Aladini alihisi amani maana anakwenda kuishi maisha a kujitegemea.

 

 

Aladini aliweza kuishi vyema na familia yake. Baadaye akamhamisha mama yake wakae pamoja. Urafiki wa mama Aladini na Mfalme uliongezeka wakawa kama kaka na dada. Baada ya miaka kadhaa mfalme alifarika baada ya kushuhudia wajukuu wawili watoto wa Aladini mmoja wa kike na wa kiume. Wakike aliitwa Hawila na wa kiume aliitwa Mustapha. Alipofariki mfalme Aladini alichukuwa nafasi kama mtoto wa kiume wa Mfalme. Hakika nchi ilipata kiongozi bora mwenye upendo. Aliweza kutuma mali yake mwenyewe kwa ajili ya maisha ya watu wa nchi yake. Hakika historia haitamsahau Aladini.

 

 

Mpaka kufika hapa Dinarzade akamaliza Hadithi ya Aladini. Kweli mfalme Shaharia aliyekuwa akisikiliza masimulizi haya kati ya Dinarzade na Shahrazade aliweza kufarujika sana. Ni mwaka sasa umefika bila hadithi kukoma. Mfamle amesahau kabisa kama alikuwa akiwauwa mabinti. Kisha Dinarzade akaanza kusimulia hadithi ya tunda tufaha (epo)





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:51:26 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 43


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 14: Wageni
Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 8 Part 1: Hadithi ya tunda
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.
Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 17: Siri ya wageni yafichuka
Muendelezo........ Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 16: Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 3: Mlevi asimuliwa hadithi
Muendelezo wa simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 18: Hadithi ya fundi cherehani
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 3: Uokozi kwenye kisiwa
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 10: Jumba la Aladini
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 6: Sehemu ya tatu ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa sehemu ya tatu ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...