Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 4: Kilema mtanashati asiye na mkono

Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.....

HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO

Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Nilipokuwa mdogo nilisikia wafanyabiashara wakitoa sifa kemkem kuhusu miji ya misri na uzuri wake. Walikuwa wakisifia jinsi mto Nile unavyokwenda kwa kasi na kupendezesha macho. Majumba makubwa ya wafalme na mafarao wa Misri. Hawakuacha kusifia uzuri wa masoko na mabinti wa Misri.

 

 

 

Basi wakati alipofariki baba yangu mimi nikawa ndiye msimamizi wa mali zake. Katika familia yetu nilikuwa peke yangu yaani sikuwa na mama wa la baba na nilizaliwa peke yangu. Basi niliendelea kukuza biashara aliyoiacha baba yangu. Na ilikuwa ni kuuza kanzu pamoja na nguo za kike. Nilikuwa nikiuza vitamaa vya kujifunika kwa wanawake ambavyo vimechovywa na dhahabu pamoja na kuwekewa haririri.

 

 

 

Watu walipenda sana aina za mavazi nilizokuwa nikiuza.nilibahatika kupata wateja wa jumala na rejareja. Sifa za nguo zangu zilienea bara la arabu hata zikafika Misri. Niliweza kupata wateja wa kike na kiume. Niliongeza ujuzi wa kuchovya nguo zangu na marashi pamoja na mafuta ya miski. Kwa hakika hazikuisha kunukia katu.

 

 

 

Sikumoja walipata kunijia wafanyabiashara wa kutokea misri. Walikuwa wakitoa sifa nyingi sana. Hata nikavutiwa na mimi kwenda Misri. Nikaanza kuwauliza maswali kuhusu bidhaa na naman aya soo lilivyo. Nikaandaa bidhaa zangu na kujiandaa kwa safari kuelekea Misri. Baada ya maandalizi kukamilika nikatoka na Ngamia wangu tulipia maeneo mbalimbali yakiyo ya kuvutia. Tulivuka bahari ya na kuingia Misri. Nikatafuta nyumba ya wageni na kulala nikiwa mimi na wafanyakazi wangu.

 

 

 

Ilipoofika asubuhi nikaanza kuchunguza mjini vyema na kutafuta eneo salama kwa biashara. Katika pirika nikakutana na meya wa Mji na kumuelezea shida yangu. Hapo akanielekeza kwa wafanyabishara wadogo. Basi nikaingia mkataba na wafanyabishara wadogo kwa makubaliano kuwa watauza bishaa zangu kisha nitakuwa ninkikusanya mapato kila siku ya alhamisi. Pia nitakuwa nikiwalipa kulingana na faida kwa kiasi maalumu. Wafanya bishara wengi wa Misri huwa wanatumia njia hii.

 

 

 

Basi nikawa kila alhamisi nakwenda kufuatailia mapato yangu na kisha ninawapatia ujira wao. Nikawa naagiza bidhaa kwa jumla kutokea maeneo mbalimbali kisha ninawapatia wauzaji. Kwa hakika Misri kulikuwa kukinipatia faida kuliko Baghadad. Nilifanya hivi kwa muda wa miezi 2 na nusu.

 

 

 

Sikumoja nilikaa dukani kwa wauzaji wangu nikiwa ninakunywa tangawizi iliyotokea china. Akaja msichana mmoja wa makamo kati ya miaka 21 mpaka 25. alikuwa amefunika sura yake, kama ilivyo tamaduni kwa waislamu. Kwa muonekana anaonekana ni msichana kutoka familia ya kitajiri. Basi alisogea mpaka pale nilipokaa na akakaa pembeni yangu. Hapo ndipo nilipopata kusikia sauti yake na harufu ya manukato yake. Hakika sijapatapo kupata harufu nzuri kama ile. Kwa muda huo aliweza kuteka fikra zangu na moyo wangu hata nisiweze kuhisi ladha ya tangawizi niliokuwa nikinywa.

 

 

 

Nilibakia mdomo waki nikiwa na maswali mengi, huyu ni nani, anataka nini hapa, ni mafuta gani amepaka, ni kwa nini amekuja kukaa karibu na mimi. Mmmmhhh sikutaka kumuuliza kwa kuhofia kuondoka kwake. Baada ya muda akaanza kuulizia bei za vitambaa vya ushungi, ambao una michirizi ya dhahabu nyekundu na mapambo ya hariri. Aliagizia vitu vya thamani sana hata nikafikiri atakuwa ni mtoto wa Mfalme.

 

 

 

Baada ya kuagiza akataka aruhusiwe achukuwe bidhaa kisha pesa atamuagiza mtu ailete. Yule muuzaji akakataa na kumueleza kuwa hawezi kufanya hivyo maana leo mmiliki wa bishara yupo. Nilipata kuyasikia vyema mazungumzo hayo. Yule binti alikasirika na kurudisha bidhaa zile na akasema “kwa hakika biashara yako haijali hadhi za watu”. maneno yale yalinichoma sana.

 

 

 

Basi kwa sauti ya upole nikamuita na kumwambia chukuwa hiyo bidhaa uliyoitaka kwani mimi ndiye mmiliki. Ukipenda utarudisha pesa usipopenda pia itakuwa ni sadaka yangu kwako. Maneno haya niliyasema bila ya kufikiri gharama ya bidhaa zile. Yule bint alinisogelea na kunieleza “Mungu akubariki kwa hisani yako, Naomba akupe afya njema ujekuwa mume wangu”. maneno haya yalikuwa ni kama msumari wa mshangao uliokita kwenye moyo wangu.

 

 

 

Nikamsogelea zaidi ni kumwambia ningepata japo kuona sura yako. Basi akasogea zaidi na kufunua kidogo kitambaa kilichoziba sura yake. Nilibaki kukodoa mimacho, hakika sijapatapo kuona uzuri huo kwa mwanadamu. Macho ya kuvutia yaliyozungukwa na nyusi nzuri zilizo nyeusi sana. Ngozi iliyo laini iliyokaa vyema kwenye shavu la binti huyo. Kwa haraka binti alishusha kitambaa na kupotelea njiani.

 

 

 

Sikumuuliza jina lake na hata wapi anakaa. Nilijuta sana maana nilitamani niwe ninamuona kila muda, kila saa, kila wakati. Nikamuuliza muuzaji wangu kuhusu taarifa za binti yule, naye hakuwa akifahamu jambo lolote. Siku hiyo sikupata hata lepe la usingizi, maana sura ya binti ilikuwa ikinijia usiku kucha. Nilitambua kuwa moyo wangu amekwenda nao wote.

 

    






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 10:55:23 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 111


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 1: Kisa cha mvuvi na jini
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA .... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 8: Simulizi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Muendelezo wa hadithi ya mtoto wa mfalme mwenye chongo katika hadithi ya HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu
Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 23: Kaka wa pili wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hadithi ya Nurdini Mtoto wa Waziri
Hii ni hadithi ya kitabu cha tatu cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 1: Muuaji ni nani?
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili ..... Soma Zaidi...