Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.....
MALIPO YA WEMA NI WEMA
Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Hapa Zubeida akawa anajiulia kuwa ni nani huyu anakuja? Aua ni yule mchumba wake? Maswali haya hayakupata amjibu. Baada ya muda kupita akatokea binti mmoja mreembi kama mwezi uliokamilika umbo lake. Binti yule akamsogelea Zubeidah na kupiga goti mbele yake na kuukamata mkono wa Zubeidah na kuubusu kisha akamwambia “ NI YAPI MALIPO YA WEMA? KWA HAKIKA NI WEMA TU”.
Lilikuwa ni swali ambalo halihitaji majibu kutoka kwa Zubeidah. Kwa malipo ya wema ni wema, Zubeida akamuuliza “ni nani wewe ni ni nani mimi na nimefuka vipi hapa?. Yule mrembo akaanza kutoa kisa chake. Kuwa yenye ni mtoto wa mkuu mfalme wa majini ambaye alionana naye hapo mwanzo. Alipokiuwa matembezima jana akiwa amejibadili katika umbo la nge alipokuwa nakimbizwa na adui wake aliyekuwa katika umbo la kunguru alimsaidia kwa kumuuwa adui wake kunguru. Hivyo yule nge alikuwa ni huyu mtoto wa mfalme. Kwa ufupo ni kuwa Zubeidah amemuokoa mtoto wa mfalme katika kizingiti za kifo kuuliwa na adui wake na huu ni wema mabao analipwa.
Basi yule mrembo akamwambia Zubeida kuwa ndugu zako walipokutumbukiza baharini nilikuwepo kwenye jahazi lenu kwa nia ya kuku;inda mpaka ufikapo kwenu. Hivyo nilikuokoa kwenuye ajali ile na sikuweza kumuokoa mchumba wako, kwa hilo naomba unisamehe sana. Hata hivyo baba yangu anaweza kukupa chochote utakacho kiseme utapata, na hata ukitaka utaishi hapa na mimi. Ila kuhusu ndugu zako kwa hakika sitaweza kuwasamehe katu. Nitawapa adhabu kubwa sana nai ningewauwa ila kwa kuhofia chozi lako siwezi kufanya hivyo.
Basi Zubeidah akaitwa na mfalem wa majini yule na kuulizwa nini ameamua kati ya yale aloelezwa na binti mafalme. Zubeidah akachagua kurudishwa nyumbani kwao na hakuhitajia chochote. Basi binti mafalme akampa unywele wake na kumwambia ukiwa na shida na mimi choma nywele hii kwa hakika nitakuja hapo kwa haraka zaidi. Basi kufumba na kufumbua Zubeidah akajikuta yupo nyumbani kwake na mlangoni wamekaa mbwa wawili na kuangalia pembeni akakuta bahasha ambayo imewekwa mlangoni. Kufungua bahasha ile akakuta ndani kuna barua iloandika\wa “Kutoka kwa Binti Mfalme wa majini ya majini na Nchi kavu kwenda kwa Zubeidah mwana wa tajiri mpotea njia mwenye kusalitiwa. Ama baada ya salamu napenda kukutaarifu kuwa hao mbwa unaowaona mlangoni kwako ni ndugu zako na hiyo ndio adhabu niloichagua. Watabaki hivyo kwa muda wa miaka 10 na utakuwa ukiwapiga fimbo za mijeledi 300 kwa kila mmoja na kila siku. Na kama hautafanya hivyo watakufa siku inayofata. Ama kuhusu mali zako zote nimeziokowa na zipo stoo. Hata hivyo baba yangu amekujengea nyumba karibu jirani na mji wa Mfalme mwadilifu Harun Rashidi mfalme wa Baghdah. Huko uende na ukakae na ndugu zako hao. Usisahau kufanya nilichokwambia Zubeidah.”
Hivyo Zubeidah akachukuwa mali zake na kuhamia katika nyumba ile aloambiwa mjini Baghdad na ndugu zake. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mbwa wakawa wanatoa machozi mengi sana na hata mfalme akawa anatoa machozi. Hivyo hii ndi sababu ya mimi kuwaadhibu mbwa hawa kila siku yalikuwa ni maneno ya Zubeidah. Mfalme baada ya kusikiliza hadithi hii akamgeukia Amina aliyekuwa na alama na makovu kwenye mwili wake na mumwambia aeleze hadithi yake, nae akaanza kama ifuatavyo;-
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 09:05:50 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 104
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 13: Wageni wa Baraka kujongea
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 10: Hadithi ya Ndoto ya binti mgonjwa wa mfalme
Skmulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 19: Kinyozi
Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabi cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 7: Hadithi ya safari ya majibu juu ya maswali mawili
Wapendwa wasomaji na wasikilizaji wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tuendelee kusikiliza hadithi zetu mzuri na za kusisimua.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP4 Part 5: Hadithi ya pili ya mtoto chongo wa mfalme
Hadithi za HALIF LELA U LELA huwa zina muendelezo na hadidhi hii ni muondelezo wa kisa cha pili cha mtoto chongo wa mfamle ambayo imetoka ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 3: Aladini akiwa na binti wa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 1: Hadithi ya safari saba za Sinbad
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini akiwa hatiani
Muendelezo.... Soma Zaidi...