Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo....

NDOA YA SIRI YAFANYIKA

Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Nikaifaa na kujipaka manukato maridadi na kuwa mtanashati ka kuelekea kwenda sala ya ijumaa. Mapema nilifika msikitini na kuanza kumuomba Mungu. Kwa furaha nia shauku nilioa nayo hata sikuweza kulala msikitini. Baada ya sala kuisha nilitoka masikitini na tayari kuelekea kwa kipenzi changu mtarajiwa.

 

 

 

Nilichukuw amashahidi wawili kwa siri, na hawa walikuwa ni wafanyabiashra wenzangu wa kutokea Baghadad. Tulipanda magari ya kuburuzwa na farasi. Tukafika katika nyumba niliyoelekezwa na tayari kugonga mlango. Mabinti wawili wengine walio wazuri sana wakafungua malango na sisi watu watatu tukaingia. Tulikutanan na ukumbi mzuri wenye malumalu za almasi. Ukuta uluojengwa vyema na kutiwa mapambo ya madini ya fedha a almasi.

 

 

 

Nikaangalia vyema nikaona mapambo yenye kuchorwa kwa lugha ya kiarabu kilicho pendeza. Tuliweza kusogea kila chumba kikiwa kina mapazia marefu yenye rangi za kupeneza sana. Mapazia yalikuwa na michirizi ya madini ya silva pamoja na mapambo ya nayoning’inia mithili ya lulu zilizohifadhiwa vyema. Niliweza kustaajabishwa na manukato ya vyumba hivi ni mazuri sana sijapatapo kuyaona. Tuliendelea hata yukafika kwenye kumbi moja kubwa sana. Hapo tukakuta kuna watu kadha aa wanaume.

 

 

 

Niliweza kuchunguza vyema ukumbi huu nikagundua umepambwa mapambo mazuri sana. Umechorwa michoro ya vippeo michoro iliweza kutiwa rangi za kijani, manjano na bluu. Hakiak niliweza kumpa sifa sana mchoraji. Katikati ya chumba kulukuwa na kiti kikubwa sana cha miguu sita. Miguu iliyopamba kwa vishikizo vya madini ya shaba, magodoro ya hariri yalikaa byema kwenye kiti hiko kikubwa.

 

 

 

Juu ya kiti mzee mkubwa alikuwa amekaa hapo. Nilimtambuwa umri wake ni kati ya 60 mpaka 70. alikuwa na ndevu nyingi na nyeupe zilizomkaa vyema. Alikuwa na sharubu nyupi na mashrafa yaliyo lala vyema. Ndevu zenye afya njema zilizotiwa hina na kufanana vyema. Mzee alivaa kanzi nadhifu yenye manukato zaidi ya watu wote tulio hudhuria. Basi tukakaribishwa vyema nikaka mimi na wenzangu. Jumla tulikuwa wtatu 9.

Bila ya kupoteza muda yule mzee akanitaja kwajina “Je wewe kijana ndiye Ibrahimu Khalidi wa Baghadad?” nilisita kidogo kujibu huku nikiwaza amelijuaje jina langu, na amejuaje kama natokea Baghadad. “ndiye mimi mzee” basi akaniambia nisogee karibu na ndipo akaniuliza maswali kadhaa na nikamjibu vyema. Basi akaniuliza “ Kijana Ibrahimu khalid umekubali kumuoa mwanangu Nurat khan”? “ hapo ndipo nilipopata kujuwa jina halisi la binti yule na kumjuwa Baba yake. “Ndio nimekubali kumuoa Nurat Khan…”

 

 

 

Baada ya hapo mbele ya mashahidi ndoa ikafungwa. Mashahidi waliweza kupatiwa dhahabu pishi tano kila mmoja na wakaruhudiwa kuondoka. Mimi nikapelekwa kwa mke wangu. Kwa hakika nilipatapo kuona mambo mengi na mazuri na ya kustaajabisha. Naomba nisielezee hasa kipengelehiki. Basi tukaelekea nyumba nyingine ambapo ndipo binti anaishi. Huko ni mbali na alipo baba yake. Na tukaendelea kumaliza taratibu za usikuwa harusi mimi na mkewangu (……taa ikazimwa…….).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 534

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani

Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 8: Aliyekatwa kidole gumba

Kojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema

Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 5: Simulizi ya samaki wa ajabu

Simulizii hii inapatikana kwenye hadhithi za HALIF LELA U LELA katika kitabu cha kwanza....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 12: Hadithi ya mfalme alikuwa kwenye kisima

Wapendwa tuendelee kuoata stori nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad

Soma Zaidi...