Muendelezo.....
UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Aladini alifumba macho kama vile mtu aliyelala, baada ya muda wa sekunde kadhaa kiza kinene zaidi ya kufumba macho. Aladini akiwa kizani kwa mbali anaona kama vile mlango unafunguliwa na hatimaye mwanga unaonekana. Aladini sasa ni kama yupo kwenye uwanja, matukio yote anayaona kwa macho yake mawili. Hii ni historia iliyotokea zamani sana na ikahifadhiwa kwenye kitabu hiki katika njia isiyo ya kawaida.
Vwazee wawili ambao walifahamiana vyema kwa urafiki walikuwa wakitoka kwenye nyumba moja kubwa. Aladini aliweza kuitambu nyumba hii ni Msikiti kutokana na umbile lake. Mzee mmoja alifahamika kwa jina Seif na Aladini aliweza kuitambua sura ile ila hakujuwa vyema ni wapi ameijuwa sua ile. Wazee wale walionekana ni wacheshi sana na walikuwa wakiitana kwa majina yao ya utoto. Mzee mmoja aliitwa Aladini na mwingine aliitwaSeif. Aladini aliaanza sas uwa na hamu ya kutaka kelewa zaidi ni kwa nini mzee seif aliweza kuijuwa sura yake lakini hakumbuki wapi ameona na ni kwa nini mzee mwingie alikuwa na jina sawa na lake.
Aladini akiwa katia hali kama hiyo ya kuwaza huku akiwasindikiza wazee wale ghafla alitokea mzee mwingine ambaye alionekana kuwa ni mwenye busara. Mzee yule akamwambia Aladini “karibu kijana kwenye uwanja wa kumbukumbu. Hapa utaweza kukumbuka kila kitu ulichosahamu ama kilichotokea zamani na kikiwa na mahusiano na wewe.” nitawezaje? “nipo kwa ajili ya kazi hiyo na ni miaka 100 sasa nafanya kazi katika kitabu cha historia ya ajabu” ni itabu gani hiko babu” “ si kitabu kimoja ni mamia ya vitabu vilivyowekwa kwenye mapango ya utajiri, tangia enzi za mfalme suleimani” haya yalikuwa ni mazungumzo machache kati ya babu na Aladini.
Kisha Aladini akamuomba babu amsimulie sasa kila kitu kuhusu anayoayaona na aliyopata kuyasikia. Pale babau akakaa mbele ya Aladini kufumba na kufumbua babu na Aladini wakawa wapo nyuma ya wale wazee wawili. Babu akaanza kumsimulia kwa kukueleza kila kitu. Hadithi ilikuwa kama ifuatavyo:
HISTORIA YA ZAMANI
Wale wazee wawili ulioowaona mmoja ndiye babu yako mzaa mama yako. Na mzee mwingine bila shaka unamfahamu kuwa ndiye mchawi uliyemsababishia kifo chake. Hawa wawili walikuwa marafiki sana. Waliiishi kaka mazingira ya kumtambuwa Mwenyezi mungu. Siku zote walikuwa ni watenda ibada. Siku zote walitii amri kutoka kwa wakubwa, na walikuwa ni wachapa kazi. Walipendelea kula kwa majasho yao. Urafiki wao ulidumu zoka wakiwa watoto hata walipokuwa ni watu wazima. Waliweza kuishi kwa amani na upendo na familia zao.
Jambo moja liliwasumbuwa kwa muda mrefu nalo ni kukosa utajiri. Mzee seifu alikuwa akimshawishi mzee Aladini ili waweze kwenda kwa waganga wapae utajiri. Kwa muda mrefu hatimaye mzee Aladini akashawishika na akakubali kwenda kwa mganga kwa sharti la kuwa wasikubali sharti lolote lakmuasi Mungu. Basi walianza kwa waganga lakini masharti yalikuwa ni yale yale ambayo ya kumuasi Mungu na kufanya sirki. Ila walifika kwa mganga mmoja aliyewaeleza kuwa watatakiwa walipie pesa wakabidhiwe pete na mshumaa. Hivyo vitawapa utajiri kwa haraka sana ila sharti moja tu wanatakiwa watoe sadaka ya kuchinja ng’ombe na kutoa nyama kwa watu bila ya sharti lolote.
Wazee hawa walikubali sharti hili. Basi wakajiandaa na kuchanga pesa na kumlipa mganga, wakatoa sadaka kama walivyoahidi na kukabidiwa mshumaa na pete. Mzee Aladini alipewa mshumaa na mzee sefy alipewa pete. Wakapewa maelezo namna ya kutumia vitu hivi. Basi mzee sefu haraka sana akaanza kutumia pete yake vyema na kuiamrisha mambo mengi na ya kiutajiri. Mzee sefu aliweza kuwa tajiri haraka sana hata watu wote wakaanza kumshangaa.
Kwa upande wake mzee Aladini akaenda mbali sana na kuanza kutengeneza lile pango. Hapo babu akamchukuwa tena Aladini hadi kwenye pango. Pale wakaanza kumuona mzee Aladini wakati huo kila alichofanya. Mzee aladini alikaa kwenye pango kwa nje na kumuomba mungu dua na kutaka kuwa utajiri wote wa mshumaa ule uje kuwanufaisha familia yake. Katika maombi yale mzee Aladini alithubut kuomba kuwa angepeda familia yake ijekuwa ni familia ya kifalme, na huu ndio utajiri hasa mzee Aladii alioutaka.
Mzee Aladini akiwa kwenye maombi jini wa mshumaa alitokea na kumueleza kuwa atahakikisha kuwa aliyoyataka mzee Aladini yanakuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Jini wa mshumaa akashukuwa karatasi ngumu ya ngozi na kuandika vitu flani kisha akaweka chini, sura ya binti mfalme ikatokea, na sura ya mfalme ikatokea. Hapo akamuhakikishia kuwa huyu ni Mfalme atakayekuwepo enzi hizo mjukuu wako Aladini atakapopata akii ya kuishi na familia. Ha huyu ndiye mfalme atakayeungana na ukoo wako.
Hapo jini wa mshumaa na mzee Aladini wakaanza kudisaini kila kitu kwa ajili ya maisha ya ukoo wa Aladini. Wakaweka kila kitu tayari ndani ya pango. Yaani kila ambacho Aladini alikiona kwenye pango kiliwekwa kwa sababu maalumu na kwa ajili yake na ukoo wake. Nyuki walioonekana ni wa dhahabu waliwekwa kwa ajiliya kuinda mafuta ya mshumaa, yale mauwa na miti ya matunda ya madini ilikuwa ni utajiri wa zamani sana uliohifadhiwa kwnye mapango toka Mfalme Suleimani alipofariki. Utajiri huu ilibidi uhifadhiwe ili ujeleta manufaa kwa vizazi vijavyo. Jini wa mshumaa alikuwa ni miongoni majini waliohudhuria mkutano uliopitisha wazo hilo, hivyo naye akabeba utajiri kuuhifadhi. Basi babu akaanza kumueleza Aladini maana ya kila kilichopo kwenye lile pango na jinsi atakavyoweza kutumia.
Baada ya kupata maelezo babu alimchukuwa Aladini na kumrudisha kwa mzee seif. Huku mzee seif utajiri wake uliongezeka na kuwa mkubwa. Baada ya masiki kadhaa akaanza kuwa mjeuri na asimkumbuke tena mwenyezi mungu. Alikuwa na kibri na dharau sana. Hata rafiki yake hakumkumbuka tena. Ilitokea siku moja akatoa kashifa na kumtuka na mzee mmoja, hali ile ilimfanya apate laana. Ilipofika usiku jini wa pete akamtokea na kumueleza kuwa hawezi tena kuendelea kuanya kazi, kwani amepigwa marufuku na jini wa mshumaa. Maana ni mkubwa kuliko yeye. Basi toka siku hiyo utajiri wa mzee sefu ukaanza kuporomoja.
Mzee Aladini hakuchukuwa muda mrefu aakanza kuumwa. Mzee sefu alikuwa akimuomba amkabidhi mshumaa lakini alikataa katu. Mzee Aldini akamueleza jini wa mshumaa ahakikishe analinda pango vyema. Mzee Aladini aliacha mtoto wa kike tu ambaye hakufahamu chochote kuhusu pango lile. Mzee Aladini alifariki dunia. Baada ya kufariki mzee Sefu alihangaika sana kujuwa wapi mshumaa umewekwa. Siu moja alishangaa kuona ukuwa jini wa pete alimjia. Na hapoa akamueleza kilakitu na namna ya kuingia kwenye pango.
Alimueleza kuwa hatoweza kuingia mwenyewe, ni lazima ampate Mjukuu wa mzee Aladini ama kijana ambaye hajajuwa mwanamke. Na anatakiwa afie pangoni na asishike kitu kingine ama kuiba chochote. Utajiri wa mzee Seifu uliporomoka na kuisha ijapokuwa jini wa pete alikuwa akija lakini hakuweza kumsaidia kupa utajiri kwa chochote. Pete sasa iliweza kumsaidia kujuwa wapi pangolilipo basi. Aliendelea kutafuta vijana wa kuingia pangoni bila mafanikio. Mzee seifu alibaki kuwa masikini tena na akahama mji kwa kuhofia udhalilifu. Na akaanza kujifunza uchawi huku akisaidiwa na pete yake mara moja moja.
Maisha yaliendelea hata binti wa mzee Aladini akaolewa na Mzee Mustapfa. Na baadaye aakazaliwa Aladini. Mzee Seif alipata habari za kuzaliwa Mjukuu wa mzee Aladini. Alifurahi maana alijuwa ni yeye tu ndiye anayefahamu siri ile ya pangoni; na hapo ndipo mambo yale yalipoanza utokea. Babu aliendelea kumsimulia mambo mengi na akamuelekeza pia yalipo mampango mengine ya utajiri. Alimueleza kuwa kwenye kabati ndani ya pango kuna ramani a kuyafikia mapango hayo. Mzee akampeleka Aladini maeneo balimbali kisha akamrudisha kwenye ule uwanja.
Aladini alipofika kwenye uwanja akaanza kuona kiza kianaanza kuingia kidogo kidgo kama mlango umafungwa na hatimaye kiza kinene. Anafumbua maho ypo kwenye kiti na kile kitabu hanacho tena. Ilikuwa ni usiku wa manane. Alipofika ndani kwake alimkuta mke wake analia sana. Alidhani mumewe amepatwa na ajali ana amepotea maana si kawaida kuchelewa ivi. Aladini hakumficah mkewe kitu akamueleza kila kitu na mkewe akaridhika. Wakalala na maeisha mengine yakaendelea.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:50:34 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 164
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Madrasa kiganjani
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 11: Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..
Karibuni tuendelee kusimuliana stori za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza, stori nzuri sana na za kuvutia zimeandaliwa kwaajili ya kujifunza na kujiburudisha pia..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 6: Hadithi ya ugeni wa dhati
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 16: Kitabu cha ajabu
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 15: Hadithi ya safari ya Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.
Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 4: Ndoa ya kwanza
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 27: Kaka wa sita wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...