Wafuatao ni baadhi ya wale waliodai utume wakati Mtume (s.a.w) akiwepo na baada yake.
Aswad Aus:
Alijitangazia Utume wakati wa Mtume (s.a.w) na aliuawa kwa amri ya Mtume mwenyewe.
Musailama (Al-kadhaab)Alijitangazia Utume wakati wa Abubakari (Khalifa wa kwanza wa Mtume (s.a.w). Waislamu walimpiga vita na kumuua.
Bah au ’lla Alijitokeza huko Iran katika karne ya 19 na aliuawa na Waisalmu.
Mirza Gulam Ahmed
Alizaliwa huko India katika kitongoji cha Kadiani katika karne ya 19. Japo alilindwa na serikali ya Kikoloni ya Kiingereza, alipigwa vita na Waislamu kwa maneno na kalamu mpaka uwongo wake ukawa dhahiri kwa waislamu pamoja na kutumia kwake Qur-an hii wanayoifuata Waislamu.
Pia kwa kukosekana mtu aliyekuja na kitabu cha mwongozo kinachofanana na Qur’an angalau kwa mbali, inazidi kutudhibitishia kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ni Mtume wa mwisho na Qur’an ni ujumbe wa mwisho wa Allah (s.w) utakaobakia mpaka mwisho wa ulimwengu.
Maana ya Kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila s iku.