image

Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?

Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?

Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?


Hakika dini mbele ya Allah ni Uislamu...” (3:19)


“Basi uelekeze uso wako katika Dini iliyo ya haki kabla ya kufika hiyo siku isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu; siku hiyo watatengana (Waumini wende Peponi na Makafiri wende Motoni).” (30:43)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa pamoja na kuwepo dini nyingi (mifumo mingi ya maisha) hapa ulimwenguni dini ya Haki anayoiridhia Allah (s.w) ni Uislamu.


Hivyo Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa na watu kwa sababu zifuatazo:
Kwanza, ndio dini ya kweli na ya uhakika kwa sababu imefumwa na Allah (s.w) aliye mjuzi wa kila kitu. Allah (s.w) ndiye aliyemuumba binaadamu kwa lengo maalumu, na hivyo ndiye pekee anayestahiki kumuwekea utaratibu wa maisha utakaomuwezesha kufikia lengo la kuumbwa kwake kwa wepesi.


Tunakumbushwa katika Qur-an:



“Litukuze jina la Mola w ako aliye Mtukufu. Aliyeumba (kila kitu na) kukitengeneza na akakikadiria (kila kimoja lengo lake) na akakiongoza (kufikia lengo hilo).” (87:1-3)
Dini nyingine zote wanazofuata watu ni dini za upotofu kwa sababu zinabuniwa na wanaadamu wasio na ujuzi wala uwezo wa kazi hiyo.


Mifumo yao ya maisha imefumwa kwa dhana wakiongozwa na matashi ya nafsi zao.


Tujihadhari na wazushi hawa wa dini kama Allah (s.w) anavyotuasa:


“Na kama ukiwatii wengi katika (hawa) waliomo ulimwenguni watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu.


Hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kuzua (tu basi).” (6:116)
Pili, Uislamu ndio mfumo wa maisha pekee unaolandana na umbile la binaadamu na maumbile yote yaliyomzunguka.


Yaani kanuni na sheria zilizowekwa na Uislamu zinakwenda sambamba na kanuni na sheria zinazofuatwa na maumbile yote, kwani mtunzi wake ni yule yule mmoja, Allah (s.w). Ni kwa msingi huu, Allah (s.w) anatanabahisha watu:



“Je, (watu) wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo mbinguni na ardhini kimejisalimisha kwake kipende kisipende?...” (3:83)


“Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa saw a ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu.Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mw enyezi Mungu.


Hiyo ndio dini iliyo ya Haki lakini watu wengi hawajui. ” (30:30).



Hivyo kwa kuwa Uislamu ni dini ya maumbile, ndio pekee inayoweza kuiongoza jamii kwa uadilifu na kuleta furaha na amani ya kweli.



Tatu, ndio dini pekee inayofuatwa na walimwengu wote wa sehemu zote na wa nyakati zote. Mitume wote wa Mwenyezi Mungu kuanzia Adam (a.s) mpaka kuishia kwa Muhammad (s.a.w), wamefundisha na kufuata dini moja- Uislamu-kama tunavyokumbu shwa katika aya zifuatazo:


“Amekupeni sheria ya dini ile ile aliyomuusia Nuhu, na Tuliyokufunulia wewe na Tuliyowausia Ibra him na Mussa na Issa, kwamba simamisheni dini (Uislamu) wala msifarikiane kwayo...” (42:13)



“Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki (kupiganiw a). Yeye amekuchagueni (muwe umma ulio bora). Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini


. (Nayo dini hii) ni mila ya baba yenu Ibrahimu; yeye (Mw enyezi Mungu) alikuiteni Waislamu tangu (katika vitabu vya zamani) huko; na ka tika (Qur-an) h ii p ia (mum eitw a jin a h ilo) ili awe Mtume shahidi juu yenu na nyinyi muwe mashahidi juu ya watu (waliotangulia)...” (22:78).



Pia Uislamu ni dini isiyoruhusu ubaguzi wa aina yoyote kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:


“Enyi w atu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kw a
(yule) mwanamume (mmoja, Adam) na (yule yule)
mwanamke (mmoja, Hawwa). Na tumekufanyieni
mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi).
Hakika aheshimiw aye sana miongoni mwenu mbele
45


ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye ha bari (za mambo yote).” (49:1 3)
Nne, Uislamu ni utaratibu wa maisha uliokamilika.


Uislamu unamuelekeza binaadamu namna ya kuendesha kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na ya kijamii. Uislamu umeweka utaratibu unaozingatia watu kama walivyo. Kwa kutambua kuwa mtu anakamilika kwa kuwa na mwili na roho, Uislamu umeweka utaratibu wa kuustawisha mwili na roho.


Uislamu umetuwekea kanuni na sheria zinazotuwezesha kujenga afya zetu na kukuza utu (ucha Mungu) wetu.


Pia, kwa kutambua kuwa watu ni viumbe wanaotakiwa waishi kijamii (social beings) na kutegemeana, Uislamu umetoa mwongozo na kuweka kanuni na sheria ambazo humuwezesha kila mtu binafsi na jamii kwa ujumla kuishi maisha ya furaha na amani.


Uislamu umeweka mifumo ya kijamii kama vile siasa, uchumi, utamaduni, na kadhalika juu ya misingi ya haki na Uadilifu.
Tano, ni dini pekee inayomuongoza binaadamu namna ya kumiliki hisia zake.


Uislamu unatuelekeza, tufanyeje tunapokuwa katika furaha kubwa.


Kwa mfano Uislamu unatuelekeza kuwa tunapokuwa na sherehe, tule na kunywa vilivyo vizuri na halali lakini tusifanye israfu na tumtaje na kumsifu Allah (s.w) kwa wingi.


Pia Uislamu unatuelekeza la kufanya pindi tunapofikwa na jambo la kutuhuzunisha sana. Kwa mfano, Uislamu unatuelekeza kuwa tunapofikwa na msiba wa aina yoyote, tusubiri na tuone kuwa,hilo lililotokea ni katika Qadar ya Allah (s.w), kama tunavyokumbu shwa katika aya zifuatazo:


“Na Tutakutieni katika msuko suko wa hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri (2 :155)



Ambao uwapatapo msiba husema: Hakika Sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea”.(2:155-156)


“Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujaumba. Kwa yakini hilo ni sahali kwa Mwenyezi Mungu.


Ili msihuzunike sana juu ya kitu kilichokupoteeni, w ala msifurahi sana kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye” (57:22-23)
Sita, Uislamu ni dini ya haki kama inavyobainika katika Qu r-an.


“Yeye (Allah (s.w) ndiye aliyemleta Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili aijaalie (dini hii) kushinda dini zote ijapokuwa watachukia washirikina” (9:33)
Dini ya haki hapa ina maana kuu mbili; maana ya kwanza ni kuwa Uislamu ni dini ya Allah (s.w), mjuzi na mwenye Hikima.


Allah (s.w) ndiye anayestahiki kuwaundia binaadamu dini kwa kuwa ndiye aliyewaumba kwa lengo maalumu na kwa hiyo ndiye mwenye haki pekee ya kuwawekea wanaadamu utaratibu wa maisha na kuuambatanisha na mwongozo utakaowawezesha kufikia kwa ufanisi lengo hilo.



Maana ya pili ni kuwa Uislamu ni dini ya kusimamia haki za binaadamu katika jamii kwa uadilifu kuliko dini yoyote ile. Mitume na Vitabu vya Allah (s.w) vimeshushwa ili kuwafundisha watu uadilifu na kuwaamuru wasimamishe uadilifu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


“Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. Na tumekiteremsha (tumekiumba) chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu ajulishe anayemnusuru na Mitume yake na hali ya kuwa hawamuoni Mwenyezi Mungu. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu mwenye kushinda.” (5 7:25).


Katika aya hii tunajifunza kuwa silaha zinatokana na chuma na aina nyingine za madini, nani zana zinazotakaiwa zitumiwe na waumini ili kusimamisha haki na uadilifu katika jamii. Katika aya nyingi za Qur-an waumini wa Kiislamu wameamrishwa kupigana na madhalimu ili kuhakikisha haki inapatikana katika jamii kwa kila raia kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Basi nawapigane katika njia ya Mwenyezi Mungu wale wanaouza maisha (yao) ya dunia kwa (kununua) ya Akhera. Na anayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauawa au akashinda, tutampa ujira mkuu (4:74).


Na mna nini hampigani katika njia ya Mwenyezi Mungu na (katika kuwaokoa) wale walio dhaifu - katika wanaume na wanawake na watoto - ambao husema: “Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe tuna mlinzi anaetoka kwako. ” (4:75)



Wale walioamini wanapigana katika njia ya Mw enyezi Mungu, lakini waliokufuru wanapigana katika njia ya ( Twaghuut). Basi piganeni na marafiki w a Shetani. Hakika hila za Shetani ni dhaifu. (4:76)
Saba, Uislamu ni mfumo wa maisha pekee ulioweka utaratibu wa kumbakisha binaadamu katika maadili ya utu.


Uislamu umemuwekea binaadamu ibada maalumu zenye lengo la kumtakasa na kumuwezesha kuwa na maadili mema yatakayopelekea kujenga mazingira ya furaha na amani katika jamii.


Ibada hizi maalumu ni Swala, Zakat, Saum, Hija, n.k. Namna ibada hizi zinavyofanya kazi katika kumbakisha binaadamu katika maadili ya utu imefafanuliwa vyema katika kitabu cha pili (Nguzo za Uislamu).



Sababu hizi tano za msingi, zatosha kuwa vigezo vya kumfanya mtu achague Uislamu kuwa utaratibu pekee wa maisha wa kufuata katika kuendea kila kipengele cha maisha yake. Dini zote zilizoundwa na watu, zimekosa kabisa sifa hizi na ni zenye kumhasirisha binaadamu katika maisha ya dunia na akhera.


Na hata mazingira yetu yanathibisha hili.


“Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake.Naye akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa) (3:85).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1482


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu) Soma Zaidi...

Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia
Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia. Soma Zaidi...

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?
Soma Zaidi...

Maana ya kumuamini mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao
Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s. Soma Zaidi...

Maana ya Kuamini Siku ya Mwisho
Soma Zaidi...

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu). Soma Zaidi...

Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira? Soma Zaidi...

Sababu za kutokubalika kwa vitabu vilivyotumwa kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu zama hizi
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاَللَّهِ وَالْيَوْمِ... Soma Zaidi...