(c)Vipawa vya Mwanaadamu

Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine.

(c)Vipawa vya Mwanaadamu<

(c)Vipawa vya Mwanaadamu


Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Mwanaadamu anatofautiana sana na viumbe wengine, hasa katika suala la kufuata utaratibu wa maisha, kutokana na vipawa alivyotunukiwa na Muumba wake ambavyo hatuvioni kwa viumbe wengine.


Vipawa hivi ni:
-Akili na fahamu ya hali ya juu ambayo humwezesha kuwaza, kufikiri na kutafakari juu ya yeye mwenyewe na mazingira yake.
-Utambuzi wa binafsi (self consciousness) ambao humuwezesha mwanaadamu kufahamu mambo mbali mbali, kutambua mambo na kuyahusisha, kuyachambua, kuyalinganisha, n.k.



-Elimu (uwezo wa kujielimisha na kuelimika) ambayo humuwezesha mwanaadamu kufahamu mambo mbali mbali na kumuwezesha kutenda kwa ufanisi na kuwa na hadhi ya juu kuliko viumbe vyote.


-Huria (uhuru wa kuamua na kutenda atakavyo) - humuwezesha mwanaadamu kufuata utaratibu wa maisha anaoutaka.



Vipawa hivi vyote kwa pamoja humtofautisha sana mwanaadamu na viumbe vingine. Humpa uwezo mkubwa na kumfanya auangalie ulimwengu na umbile lake pamoja na vyote vilivyomo kwa mtazamo wenye kutofautiana mno na ule wa viumbe wengine.


Kwa mfano, kutokana na utambuzi binafsi (self consciousness) mwanaadam anatambua uhusiano wake na watu wa familia yake.


Kuna baba, mama, dada, kaka, mke, watoto na ndugu wengine ambao anapaswa kushirikiana nao mpaka kufa.



Hapa lazima mwanaadam aamue mwendo atakaoufuata ili kuwa na uhusiano unaostahiki baina yake na watu hawa.


Pia mwanaadamu ana uhusiano na watu wasio hesabika ulimwenguni, wengine ni majirani zake, wengine marafiki wengine ni maadui zake. Kuna wenye haki juu yake na wako wenye haki zake. Pia mwanaadamu ana uhusiano na viumbe vingine vyenye uhai na visivyo na uhai.


Kwa ujumla vyote hivi vipo kwa kumsaidia yeye lakini mwanaadamu anapaswa aamue namna ya kuvitumia kwa manufaa yake yeye mwenyewe na wale wanaomzunguka.



Hivyo, ni dhahiri kuwa ni lazima mwanaadamu awe na njia iliyojenga mwenendo wake juu ya namna atakavyoshirikiana na wanaadamu wenziwe na viumbe vyote vinavyomzunguka kwa sababu katika hali halisi ya maumbile jambo hili la uhusiano haliendeshwi na silka (instinct) kama ilivyo kwa viumbe wengine. Njia hii inayojenga mwenendo baina yake na mazingira yake ndio dini yake - njia yake ya maisha.



Pia mwanadamu ameumbwa katika namna ambayo hawezi kujitosheleza mwenye. Kwa namna moja au nyingine ni mwenye kuwategemea wanaadam wenziwe na viumbe vingine. Hivyo utaona kwamba mwanaadam hawezi kuishi bila ya kuwa na maingiliano na wanaadamu wenzake, viumbe vingine na mazingira yake yote kwa ujumla.


Kutokana na sababu hiyo basi utaona kuwa kila mwanaadamu anafuata utaratibu wa maisha (dini) ambao hujenga uhusiano wa maisha baina yake na mazingira yake.


Suala lingine ni mwanaadamu kuwa na akili ya hali ya juu kuliko viumbe vingine vyote katika ardhi hii. Hatusemi kuwa wanyama hawana akili kabisa lakini sio katika daraja ya juu kama ilivyo akili ya wanaadamu.


Kwao wao hitajio muhimu ni silka inayowawezesha kuishi na kuzaana na akili kama wanayo si hitajio kubwa kama lile la silka.


Kazi yake ni kuwawezesha kutambua mahitajio yao ambayo ni lazima wayafuate ili waweze kuishi na kuzaana.



Swali ni kwamba kwa nini mwanaadamu ana akili zaidi kuliko viumbe vingine (wanyama)? Kwa kweli hakuna sababu nyingine isipokuwa ni kumuwezesha mwaanadam kutambua njia ya maisha inayomfahamisha na kumuelekeza kwenye lengo la maisha yake hapa duniani.


Mwanaadamu atakapoacha kutumia akili yake kwa kazi hii atakuwa hana tofauti na mnyama katika kuendesha maisha yake ya kila siku na wakati mwingine atakuwa na mwenendo mchafu zaidi kuliko ule wa mnyama kama Qur-an inavyotutanabahisha:


Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam - wengi katika majini na watu (kwa sababu hii). Nyoyo (akili) wanazo lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi.


(7:179).
Kwa hiyo, mwanaadamu ana akili ya juu kuliko jamii ya viumbe vingine ili aweze kuamua ni njia gani ya maisha inayostahiki kufuatwa.


Hivyo, kutokana na vipawa alivyonavyo, mwanaadamu hujisaili maswali kama: Nini chanzo cha ulimwengu na nini lengo la kuwepo dunia na uhai wa mwanaadamu na ni vipi mwanadamu aishi ili afikie lengo hili? Maswali haya ni lazima yapatiwe majibu ili maisha yaweze kuwa na maana na muelekeo.


Majibu yatakayotolewa ndio yatakayokuwa msingi wa dini ya mwenye kutoa majibu hayo.



Kwa mfano kama mtu atatoa jawabu kuwa chanzo cha ulimwengu ni bahati nasibu (chance creation) yaani hauna muumbaji na uhai ikiwa ni pamoja na maisha ya mwanaadamu hauna lengo, basi mtu huyo atayajenga maisha yake juu ya msingi kwamba hakuna Mungu


. Hivyo njia yake ya maisha au dini yake itakuwa ya kikafiri.



Kwa ujumla vipawa hivi vya hali ya juu alivyotunukiwa mwanaadamu, kuliko viumbe wengine humlazimisha mwanaadamu kufungika katika mfumo wa maisha ya kijamii katika kuendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku katika uchumi, siasa, utamaduni, na kadhalika. Mfumo huo wa maisha utakuwa ndio dini yake.



Kwa mtazamo wa Uislamu tumeona kuwa dini ni utaratibu au mfumo wa maisha anaofuata binaadamu, katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii.



Hivyo kwa vyovyote vile binaadamu katika kuendesha maisha yake ya kila siku atakuwa anafuata dini moja au nyingine.


Akifuata mfumo wa maisha aliouweka Mwenyezi Mungu, ambao ni sawa na mfumo wa maisha unaofuatwa na maumbile yote (Qur-an 3:83) atakuwa anafuata Dini ya Kiislamu - dini ya kujisalimisha kwa Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha.


Binaadamu akiamua kufuata mifumo ya maisha iliyojengwa kwa kanuni na sheria zilizowekwa na watu, zinazopingana na kanuni na sheria za Allah (s.w) atakuwa anafuata dini za Kikafiri - Mifumo ya maisha inayopingana na mfumo wa maisha aliouweka Allah (s.w).



Hivyo katika kuishi hapa duniani watu wanagawanyika katika makundi makuu mawili - kundi la Waislamu wanaoufuata mfumo wa maisha aliouweka Allah (s.w) na kundi la Makafiri


wanaofuata mifumo ya maisha waliyoibuni watu kama inavyobainika katika Qur-an:-


'Yeye ndiye aliyekuumbeni (nyote). Wengine wenu ni Makafiri na wengine wenu ni Waislamu. Na Mwenyezi Mungu anayaona (yote) mnayoyafanya.' (64:2)




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 283


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa
Soma Zaidi...

dharura
14. Soma Zaidi...

Bani Israil Kuabudu Ndama
Wakati Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Adam(a.s) na Mkewe Katika Pepo
Adam(a. Soma Zaidi...

Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu
Kuchunga'au kutekeleza'ahadi'ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat Al-Asr
Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...

HADITHI YA TUNDA EPO
Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya vitani
Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)
Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema. Soma Zaidi...

Kuwa na mwenye haya, na faida zake
24. Soma Zaidi...