Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini

Muendelezo....

HATMA YA NURDINI NCHINI KWAKE.

Baada ya mfalme kuondoka pale ndani zilipita siku tatu bila hata kuongea na mte yeyote yule. Jambo hili lilileta taharuki kubwa sana. Hatimaye siku ya nne na mapema mfalme akaonekana kwenye baraza la asubuhi. Akiwana barua yake mkononi alionekana kuhoji baadhi ya walinzi. Alikuwa akihoji ni kitu gani kilitokea kwa Nurdini na wapi alipo. Majibu aliyopatiwa huwenda hayakumfurahisha kwa sababu uso wake haukuonekana kufurahia kabisa. Moja kwa moja alikwenda kuketi kwenye kiti chake cha kifalme. Kilikuwa ni kiti kirefu chenye vishikizo vya dhahabu, vilalio vya hariri iliyo laini vyema. Ijapokuwa kiti kilikuwa ni kizuri na lakini mfamle hakuwa na raha kabisa.

 

 

 

"nimepokea barua kutoka kwa Haru Rashid wa Baghadad ananitaka nijivuwe madaraka kwa amani ili nimkabidhi Nurdini kijana wa hayati waziri wangu mzee Farid". Yalikuwa ni maneno ya mfalme yaliyoonekana kumstaajabisha kila mtu aliyekuwepo pale ndani ya ukumbi ule. Hapo zamani mfalme wa nchi hii hupata uthibitisho wa kuendelea na madaraka ama kuyawacha kutoka Baghadad.

 

 

 

Ni kuwa wakati fulani nchi hii ilivamiwa na majeshi kutoka meneo ya India. Hivyo mfalme wa Baghadadi akiwa anatokea Maka kuhiji aliweza kuokoa nchi hii dhidi ya jeshi la wahindi. Tokea hapo wakaweka mkataba kuwa mchi hii mfalme hatakuwa halali mfapa athibitishwe na mfalme Harun Rashid wa Baghdad. Mkataba huu utaendelea kuwa hai mpaka pale ambapo Mfalme Harun Rashid atakapofariki.

 

 

 

Sasa kabla ya mfalme huyu walisha pita wafalme watatu nyuma. Mzee Farid pia alikuwa katika orodha ya kuwa Mfalme lakini alikatwa kutokana na upole wake. Hivyo kwa mkataba walioweka mfalme wa Baghadad ataweza kumuachisha madaraka mfalme wa nchi hiyo endapo hataridhishwa na utendaji wake kama kunyanyasa wananchi ama kupuuza majukumu yake. Hivyo basi kwa barua aliyoleta Nurdini inamaana mfalme huyu anatakiwa ajivue na Nurdini awe mfalme mpya.

 

 

 

Baada ya majadiliano marefu sana mawaziri walionekana kutokukubaliana na maamuzi hayo. Nusu walikuwa wanataka mfalme wao aendelee, kiongozi wa kundi hili alikuwa ni Masoud. Na nusu nyingine ilitaka mfalme akubali kuachia madaraka na kiongozi wa kudni hili walikuwa na rafiki na jamaa wa mzee Farid. Mwisho Masoud alitowa hitimisho kwa kusema "kwanza barua yenyewe haipo sahihi, ilipaswa iletwe na waziri ama kiongozi yeyote kutoka serikalini kwake, sasa haiwezekani Nurdini alete barua hii, mimi naona nurdini ni muongo, ameghushi barua hii hivyo akamatwe kisha auliwe"

 

 

 

Yalikuwa ni maamuzi magumu lakini mfalme alikubaliana nayo. Mfalnme akaruhusu Nurdini akamatwe atiwe kwenye gereza lililo madhubuti sana . swala la kumuuwa hakutaka lifanyike mpaka ainarishe ulinzi kwanza maana kunaweza kukatokea vita kutokana kupuuza barua ile endapo itakuwa ni ya kweli. Masoud ijapokuwa alisisitiza nurdini auliwe lakini hakuwa na pingamizi kwa maamuzi ya mfalme wake.

 

 

 

Siku arobaini sasa zimepita toka Nurdini aondoke baghadad. Siku hiyo mfalme alipita kwenye nyumba ambapo mke wa Nurdjini yupo. Alimkuta anaimba mashairi ambayo yalikuwa ni kuilaumu nafsi yake kwa kumuachia mune wake kipenzi kuondoka peke yake. Mfalme alisikitishwa sana pia akaijona yupo makosani. Ikabidi aitishe mkutano kidogo kuhusu barua yake aliyoituma. Katika mkutano wakakubaliana liondoke jeshi la watu 3000 kajini lisiibgie nchini likae nje ya mji ama mipakani, kisha waziri wawili akiwepo Jafari waingie kwa mfalme wa nchi ile ili kufuatilia barua ya mfalme Harun rashid. Endapo mfalme ataipinga jeshi linatakiwa limtoe kwa nguvu.

 

 

 

Katika msafara huu mke wa Nurdini pia likuwepo. Wakatoka kuelekea huko. Siku ya tatu wanaingin, kumbe na kule mfalme aliitaka kumuuwa Nurdini. Taarifa za jeshi la wa tu 3000 zikamfikia mfalme na wakati huo mawaziri wa mfalme harun rashid wanaingia. Mfalme Muhammad ibn Suleiman hakuwa na njia nyingine ya kuema barua ni feki. Hivyo ikabidi akabidhi madaraka kwa amani kabisa kwa Nurdini.

 

 

 

Kutoka hapo Nurdini akawa ndio mfalme mpya wa nchi hii. Mahusiano mazuri ya nchi mbili hizi yalitanuka na kuchanua vyema. Wananchi waliweza kusafiri na kushirikiana kibiashara kati ya nchi mbili hizi. Uongozi wa Nurdini ulipenda sana kwani hakuweza kuwabaguwa wanyonge. Kwa masaada wa mke wake aliyekuwa na akili na busara kubwa Nurdini alibadilika sana na kutoka Nurdini mzembe kuwa Nurdini bora sana.

Huu ndio mwisho wa hadithi hii. Ahsante sana kwa kuwa mvumilivu tukutane hadithi ya Badrudini, bila sjaka utaipenda zaidi kuiko hii.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa image Tarehe 2024-09-10 15:05:13 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 168


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 1: Muuaji ni nani?
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 5: Safari ya kwenda nyumbani
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 3: Simulizi ya kuingia kwa wageni
Simulizii hii ya kuwasili kwa wageni inapatikana ndani kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... moja kwa moja tusikilize kisa hichi.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 10: Jumba la Aladini
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 2:  Simulizi ya tabibu wa mfalme
Simulizi ni nzuri sana maana zinafundisha na hazibagui mkubwa wala mdogo... tusikilize na kusoma kisa cha tabibu wa mfalme....kutoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 15: Baba tajiri na kifo chake
Muendelezo....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 8: Hadithi ya kisiwa cha uokozi
Simulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP4  Part 5: Hadithi ya pili ya mtoto chongo wa mfalme
Hadithi za HALIF LELA U LELA huwa zina muendelezo na hadidhi hii ni muondelezo wa kisa cha pili cha mtoto chongo wa mfamle ambayo imetoka ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 10: Hadithi ya Ndoto ya binti mgonjwa wa mfalme
Skmulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 12: Dirisha moja kwanini????
Muendelezo.... Soma Zaidi...