Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....
USULUHISHAJI WA WALODHULUMIWA.
Basi baada ya kusikiliza hadithi hizi mfalme akaanza usuluhishi na kumwambia Zubeidah achome huo unywele ili amuite jini binti mfalme. Basi Zubeidah akauchoma huo unywele na baada ya punde akaja jini yule na mfalme akataka msamaha kwa mabinti walogeuzwa mbwa, basi akawambwagia maji na wakageuka kuwa watu. Pia bint mfalme akazungumza kuwa alomfanyia unyama Amina ni mwanao mwenyewe ewe mfalme ni kuwa mtoto wako alimpenda Amina na kumposa na ndoa aliifanya kwa siri na hatimaye mambo yakawa hivyo. Basi jini akaondoka.
Mfalme akamuita mwanae na kumuuliza yalotokea na akamjibu kama mambo yalivyo elezwa. Basi akatoa amri mrejee mkewe na kisha Zubeidah ana dada zake akawaozesha kwa wale machongo watatu na yeye mwenyewe mfalme akamuoa Sadie. Inasemekana ndoa zao zilikuwa ni za upendo wa hali ya juu na hakukutokea ugomvi mpaka Allah akapitisha amri yake.
Baada ya Schehra-zade kumaliza kusimulia hadithi hii Dinar-zade alifurahi sana. Lakini furaha hii haikumzidi sultani. Hapo Schehra-zade akamwambia basi hadithi hii haifiki hadithi ya Sinbad mwenda baharini. Sultani akuliza ni kipi kilompata sinbad mwenda baharini hata hadithi yake ikawa nzuri hivyo? Hapo Schehra-zade akaanza kusimulia hadithi hii;-
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 18: Binti wa pili mwimba mashahiri mwenye makovu
Mwendelezo wa hadithi kutoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA......
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Mtumwa wa mfalme na mawaziri
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha tatu.....
Soma Zaidi...