picha

Hatima ya kijana mchonganishi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

HATIMA YA KIJANA MCHONGANISHI

Mansur akaondoka haraka akiwa na majozi sana huku akiwaza nitampata wapi kijana huyu. Mansur alijisemea, Mungu aliyeniokoa na janga la kwanza ataniokoa na hili la pili. Mansuri alipofika kwake aliwaeleza kla kitu, na akabakia kwake kwa siku tatu bila kwenda kokote. Manzur ilipofika siku ya tatu akajiwa na mjumbe kutoka kwa khalifa kuwa anahitajika akiwa na muhalifu ama ajiandae kwa kifo. Mansur akaanza kuagana na famiia yake na kuacha usia.

 

Kabla ya kuondoka mwanae mdogo aliyekuwa akimpenda sana alikuja kumkumbatia baba yake kama ishara ya kuagana. Mansur wakati akimkumbatia mwanaye alihisi ugumu kwenye tumbo la mwanaye. Akamuuliza ameweka nini. Mtoto akajibu kuwa nimeweka tunda epo nimepewa na Manyakazi wetu, alikuwa hataki kunipa eti amemnyang’anya mtoto wa watu ambaye baba yake amekwenda mbali kununua maepo matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabu.

 

Mansur aliposikia habari hii alifurahi sana na kusema ssa nimeokoka. Hapo akamchukuwa mfanyakazi wake na kwenda naye kwa khalifa. Kijana akaulizwa na kukirikonsa. Khalifa akaagiza habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na ihifadhiwe kwenye kumbukumbu ya nyaraka za kushangaza na kutisha. Kisha waziri Mansur akasema ewe khlifa ninakiri kuwa mfanyakazi wangu amepatwa na hatia. Ila ninakuomba kuwa nitakusimulia kisa cha kushangaza zaidi ya hiki, na endapo utakirikuwa kimeshangaza zaidi naomba iwe fidia umuache huru mfanyakazi wangu.

 

Khalifa alikubaliana na maneno haya na hapo Mansur akaanza kusimulia hadithi ya Nurdini.

 

Tukutane kitabu cha tatu hadithi ya Nurdin

 

Huu ndio mwisho wa kitabu cha pili hadithi za Alif lela u lela. Usiwache kuwa nasi tukutane kitabu cha tatu. Kama unahitajikitabu cha kwanza na pili wasiliana nasi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF Views 2123

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 web hosting     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

KIFO CHA AJABU

Download kitabu Hiki Bofya hapa KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN.

Soma Zaidi...
Kwanini vidole gumba vilikatwa

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y

Soma Zaidi...
Alif lela ulela

Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...