image

Hatma ya kinyozi maishani mwangu

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

HATIMA YA KINYOZI MAISHANI MWANGU

Baada ya muda kusubiri ndipo akaletwa kinyozi. Kinyozi alikuwa na upara, na ndevu ndefu zilizokuwa nyeusi sana na zenye afya. Nilipomwangalia vyema niligundua kuwa hakuwa ni mzee. Ijapokuwa sura yake haikuwa ni ngeni sana, lakini sikujuwa hata kidogo niliipata wapi. Sikutaka kujuwa mengi sana, nikamueleza kuwa aninyoe mnyoo wa kawaida sana, na nywele ziwe fupi. Kinyozi naye hakutaka kuchelewa akatoa vifaa vyake na kuanza kunoa kisu, ama kinyoleo chake.

 

Kinyozi alinoa kwa haraka hata nikadhani anaweza kumaliza kichwa changu ndani ya muda mchache sana. Allipomaliza kunoa akakiendea kichwa changu na kuanza kukiangalia vyema. Ghafla akaondoka na kuelekea kwenye vifaa vyake. Kisha akatoa kitu kama yai kisha akaeekeza kwenye jua kwa muda kidogo. Kisha aakaza kunieleza kuwa “siku ya leo ni mbaya sana kwako, unatakiwa unieleze unakotaka kuelekea ili nikusaidie” sikuelewa anazungumzia utumbo gani, nikamwambia aninyoe haraka.

 

Alichokifanya ni akachukuwa kisu na kuninyoa kidogo kisha akaanza tena kunieleza utumbo wake. “baba yako namfahamu sana na alikuwa hafanyikitu bila ya kunishauri, pia nakumbuka nilikuwa nikikubeba sana ulipokuwa ukimsumbua baba yako kwa kutaka safari zisizo kuhusu”. napo nikaanza kukumbuka kuwa kumbe ndio maana ninaifahamu sura yake. Lakini sikuweza kuvumilia utumbo wake aliousema maana muda unazidi kusogea halafu ameninyoa kidogo anaendelea kubwabwaja. Nilimchukia hata nikamueleza kuwa ondoka na nitaita kinyozi mwingine. Aliposikia maneno yakke basi kwa haraka akaendelea kuninyoa tena kidogo kisha akaanza kubwabwaja.

 

Nilijaribu kumdanganya kuwa nina haraka kuna mwaliko nimepewa na rafiki zangu. Nilijuta kuyasema maneno haya maana ndipo akataka tuende sote. Alining’ang’ania sana kuenda, nikamueleza afanye haraka kuninyoa nitamchukuwa. Hapo ndipo akaninyoa kwa haraka, kisha akalinganisha vyema kichwa changu. Alipomaliza nikamuelekeza sehemu aende atanikuta. Alikataa, kabisa kwa madai kuwa anataka tuende wote vinginevyo hataenda.

 

Nilichofanya nikampatia vyakula na vinywaji kisha nikamueleza atangulie huku na mimi nakwenda kutafuta matunda mazuri. Nilichokifanya nikamuelekea aende dukani kwangu, maana kuna kijiwe pale nje, hivyo lazima atawakuta watu. Yote haya nilikuwa nayafanya ili niweze kumtoroka niende kwa mwanamke yule. Nilipanga tukikubaliana nipose kabisa. Kumbe wakati ninawaza haya yeye alitambua fika kuwa yote ninamdanganya tu.

 

Alichokifanya alichukuwa vitu na kuelekea nilipomuelekeza. Na mimi kwa haraka nikatoka na kupotelea mtaani. Nilikwenda mpaka kwenye lile jumba la mzee tajiri, nilipomuona yule binti bila ya kutambuwa kumbe kinyozi alikuwa ananifatilia kwa mbali. Nikaingia ndani, sasa wakati naingia kumbe yule mwenyewe alikuwa bado yupo ikabidi nijifiche mule ndani. Ghafla nikasikia makelele. Mzee tajiri alikuwa akimpiga mtumwa wake kwa makosa aliyoyafanya. Alimpiga na kwa bahati mbaya alifariki dunia.

 

Kinyozi alikuwa akifatilia mambo yote haya kwa ukaribu japo alikuwa kwa mbali. Alitambua kuwa aliyekuwa akipigwa ni mimi, hivyo akajuwa kuwa nitakuwa nimekufa tayari. Alichokifanya alikimbia kwa haraka mpaka dukani kwangu na kuchukuwa vijana kwa wazee wote waliokuwepo pale. Wakaja kwenye jumba la tajiri na kuanza kumzogoma tajiri kwa kosa la kumuuwa mtoto wao. Yaani waliamini mimi mtoto wao nimeuliwa na tajiri.

 

Tajiri hakuwa mwenye kuyaelewa maneno yako vyema ndipo akamuomba mmoja wao aeleze kwa ufasaha hasa nini kimetokea. Ndipo kinyozi akatoka na kusema “Binti yako na mtoto wetu wanapendana, na wewe umemkamata kijana wetu leo ukampiga na kumuuwa hivyo lazma ulipe”. tajiri akawaeleza kuwa mimi hayo mambo siyajuwi na ndio kwanza hivi nina yasikia, na kama huamni ingia ndani ukamtafute kijana wako, kama ukimkuta amekufa nitalipa chochote mkitakacho na hata shingo yangu nitakupatieni”.

 

Kinyozi akatoka na kuingia ndani, akafika kwenye ukumbi ambao nipo. Nilipomuona nikaingia kwenye sanduku kubwa na kujificha. Alipoona hakuweza kuniona aliliburuta sanduku na kutokanalo nje. Nikakurupuka kwenyesanduku lile na kutaka kukimbia. Nilishangaa sana kuona nje kunakundi kubwa la watu. Nikatoa vipande vya dhahabu nilivyo navyo nilivyopanga kumpatia yule binti. Nilivirusha vipande vile vya dhahabu kwenye kundi la watu. Lengo watakapoanza kugombe dhahabu nitatoka mbio.

 

Basi mambo yakawa kama hivyo, watu wakaanza kugombe dhahabu ndipo nikatoka na kukimbia ili nisikamatwe. Ukweli ni kuwa ningekamatwa na yule mzee tajiri bila shaka angeniuwa. Nilipokuwa nakimbia nilishangaa kumuona kinyozi yupo nyuma yangu. Nilikasirika sana, lakini sikuwa na jinsi. Nilikimbia mpaka mbali sana nikakaa kupumzisha nafsi yangu. Kabla sijasimama nikajikwa kwenye jiwe na kuanguka chini Loo!loo nikavunja mguu wangu. Nilipatwa na maumivu makali sana. Nikakaa chini pembeni kidogo baada ya kujiburuza. Na kinyoz akakaa pembeni yangu. “angalia sasa kwa ujinga ulioufanya, nimekosa kukutana na mwanamke wa maisha yangu na nimevunja mguu wangu” ni maneno niliyomwambia kinyizi.

 

“hivi huini kuwa nimekuokoa kutokana na kuuliwa na tajiri” huu ndio upuuzi aliyo nijibu eti ameniokoa. Kisha akaanza kunipa huduma ya kwanza kwenye mguu wangu. Nilikaa kwake kwa muda wa siku tatu, na hata sikutaka kurudi nyumbani kwa kuhofia usalama wa familia yangu. Siku ya nne nikaandika barua ya kumtaarifu yule binti kuwa ninasafiri ila nitarudi kwa ajili yake. Kama bado atanisubiri haitachukuwa muda mrefu. Kisha nikaipiliza barua hii kwa bibi ipeleke.

 

Sikutaka tena kumuona kinyozi wala kuishi naye mji mmoja. Niliandika barua kuipatia familia yangu na kuwaeleza kuwa ninasafiri kidogo. Lengo ni kuwa mbali na kinyozi ili kutuliza nafsi yangu. Nilibeba hakiba yangu na kuja hapa baghadad, ni miezi mingi yamepita, sasa nilishangaa tena leo kumuona hapa. Moyo wangu uliumia sana nilipomuona leo. Na hii ndiyo hadithi yangu mimi na huyu kinyozi.

 

Basi muandaaji wa sherehe akamuuliza kinyozi je anayoyasema ni ya Ukweli. Kinyozi akazungumza kuwa ni kweli kabisa na asingelikuwa yeye kijana angeuliwa kabisa.kisha kinyozi akaendelea kusema “mimi si mtu wa maneno mengi kama walivyo kaka zangu, na nimeokoa maisha ya huyu kijana lakini yeye ananidharau na kuniona kuwa ni mtu muongo na mwenye maneno mengi. Mimi kaka zangi wengine ni vipofu, viziwi, wasio na mikono , na mabubu. Yote haya wameyapata kwa sababu ya midomo yao na maneno yao mengi, ngoja niwasimulie yaliyowapata kaka sangu saba, kisha ndio mtajuwa kuwa mimi si mtu wa maneno mengi, na isingelikuwa ni mimi kijana angekufa”

 

Alipomaliza kusema maneno haya akaanza kuhadithia yaliyowakuta kaka zake sita hata wakapata ulemavu kwenye viungo vyao.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 838


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Upendo uliotafsiriwa kwa michoro
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME
Soma Zaidi...

KWA NINI DIRISHA MOJA?
KWA NINI DIRISHA MOJA? Soma Zaidi...

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO
Soma Zaidi...

JARIBIO LA TATU LA A LADINI
Soma Zaidi...

UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Soma Zaidi...

Kwa nini vidole vimekatwa
HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tano wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi
Soma Zaidi...

Ndoa ya siri
NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Soma Zaidi...