HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU

HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU

HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU


HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU



Aladini alipofika kwake alikuwa na mawazo sana, maana ilibakia kidogo aingie majaribuni. Aladini sasa alikuwa na mawazo kuwa muda wowote asipokuwa makini anaweza kupoteza kila kitu. Kwa mawazo yote aliamua akalale. Katu usingizi hakuweza kupata hata lepe la usingizi. Aladini akiwa kwenye fikra na mawazo haya ghafla aliwaza kile kitabu. Aladini alifikiri hasa ni nini chanzo cha lile pango na ni kitu gani kimeandikwa kwenye pango lile. Aladini akapatwa na hamu kubwa ya kusoma, ijapokuwa Aladini hakukulia katika mazingira ya kupenda kusoma. Aladini alifikiri ili aweze kuelewa vyema akaoge. Pia huenda alikwenda kuoga kwa sababu Aladini aliamini kuwa kitabu kile kitakuwa ni kitabu kitukufu hivyo si vyema kukigusa bila hata kuoge.


Baada ya kumaliza usafi wa mwili Aladini akakamata kitabu akiwa yupo kitandani kwake. Hata mkewake alishangazwa sana na tabia ya mumewe leo kusoma. Kwa hakupatapo kumuona akisoma hata. Gamba a juu la kitabu lilikuwa ni la ngozi iliyokunnwa vyema. Gamba la juu lilikuwa ni chakavu na halikuweza kuonyesha chochote katika picha wala maandisi. Lakini mshangao mkubwa ni pale Aladini alipofunua ukurasa wa kwanza wa kitabu ambapo alikuta picha ya pete aliyovaa, mshumaa wa ajabu, yule ndege wa ajabu, vile vijiwe vya pangoni, vile vijiko pamoja na kit kama yai. Lakini kitu hiki kumeandiwa juu na nyuki kadhaa wa dhahabu. Picha hizi hazikuwa na majina. Hapa Aladini akaanza kupatwa na mshangao na kuanza kufikiri kuwa huwenda mambo yote aliyokutana naye yalishatabiriwa kwenye kitabu hiki.


Aladini alizidiwa na ushawishi na madukuduku. Aladini hakuridhishwa na zile picha alitaka sasa kuona nini maana ya picha zile. Ndipo akafunguwa ukurasa unaofata. Loo! Aladini alistaajabu zaidi kuona kuna mchoro wa sura yake, mkewe, baba yake na pia kulikuwa na sura mbili za watu ambazo ni ngeni sana kwa Aladini. Watu hawa alikuwa ni babau yake na mchawi wa pili. Aladini alianza sasa kuamini kuwa kitabu kile kuna familia yake, hivyo kuna uwezekana wa uhusikaji wake katika pango lile. Chini ya ukurasa huu kulikuwa na maandishi ya lugha asiyoijuwa. Lakini maandishi hayo yalifanana sana na maandishi ya majini.


Ukurasa uliofuata ulikuwa na rangi nyeusi tupu na maandishi ya rangi nyeusi yaliyoweza kuonekana kwa mbali sana, kama vile jongoo kwenye usiku wa kiza. Maandishi yaliweza kusomeka kwa mbali sana. Aladini akabaki kukodoa mimacho tuu. Baada ya kutazama kwa muda mrefu maandishi yale yakaanza kubadilika taratiibu kuwa meupe na kuanza kusomeka vyema. Mambo haya yalimshangaza sana Aladini. Muda wote Aladini alikuwa akisoma kitabu akiwa amelala kichalichali. Basi akajigeuza upande wa kulia. Wakati anajigeuza kwa bahati mbaya alikifunga kitabu. Alipokuja kukifungua kila alichokisoma na kukiona kwenye kitabu kile hakikuweza kuonekana tena. Zilibaki kurasa tupu. Dah aladini alistaajabu sana, na alitambuwa kuwa hakuna kinachobakia kwenye kitabu hiki baada ya kukisoma.


Kwa kuwa Aladini hakuweza kusoma yale maandishi yaliyokuwa yakisomeka baada ya kukodoa macho kwa muda maandishi yakaanza kurudi tena. Maandishi hayakuwa mengi sana ila yalisomeka kama ifuatavyo


โ€œSalamu nyingi zikufikie mchaguliwa wetu ewe Aladini, bila s haka ndiwe unayesoma hiki kitabu kwa sasa. Kwani asingeweza yeyote kusoma ila wewe. Siri nzito ya familia yako na pango ili inapatikana humu. Tumekilinda kitabu hiki kwa miaka zaidi ya 85 sasa, na baada yako hakuna atayeweza kuisoma katu, kwani maandishi tutakuwa tumeshayachukuwa. Kumbuka siri za kwenye kitabu hiki hutamueleza yeyote. Tambua pia kuwa kurasa zijazo utatakiwa kufumba macho ndio uweze kusoma kitabu hiki. Hakikisha upo peke yako katika sehemu tulivu, mwisho ninakutakia mafanikio mema na binti mfalmeโ€


Aladini sasa maswali mengi yakazidi kuzunguka kichwani mwake hasa pale alipotakiwa mafanikio mema yeye na binti Mfalme. Inamaana maisha ya Aladini yalishaandikw akuwa atamuoa binti Mfalme. Aladini alijaribu kufungua kurasa zijazo lakini hakuona maandishi. Alijaribu kukodoa macho kwa muda mrefu lakini wapi. Aladini sasa akawaza kuwa njia pekee ya kuendelea kusoma kitabu kile ni kufumba macho na kuwa katika sehemu nzuri na tulivu. Aladini akafikiri kuwa chumba cha stoo ambapo kulikuwa kukitoka mwangaza hajawahi kuingia, wala kuchunguza mwangaza ule ulitokea wapi. Aladini akawaza kule ndio sehemu pekee iliyo tulivu ambapo hatoweza kusumbuliwa katu.


Aladini akabeba kitabu chake na kuelekea kwenye chumba kile. Loo! Harufu nzuri ya marashi yaliyonukia vyema ilimkaribisha. Aladini alistaajabishwa kuona kuwa chumba kile kina vijiwe vinavyotoa mwangaza kama vya kule pangoni. Vijiwe vilikuwa kwenye kaboksi kadogo ka vioo. Chini ya kiboksi kulikuwa na karatasi iliyoandika โ€œzawadi kwako Aladini mjukuu wanguโ€. Aladini alikuta kwenye chumba kile kuna kiti kikubwa kizuri sana. Kiti kilichofanana na cha mfalme. Aladini alikaa pale na kujiandaa tayari kwa kusoma ujumbe wa siri kwenye kitabu cha maajabu.

๐Ÿ“„ Download Post hii
Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 598

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono
Hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono

Soma Zaidi...
Siri ya wageni wale inafichuka
Siri ya wageni wale inafichuka

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Siri ya wageni wale
Siri ya wageni wale

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu
Hadithi ya tabibu

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA TABIBU: Tambua ewe Sultani mwadilifu kuwa mimi nimezaliwa katika familia ya wachamungu waabuduji wanaofata mila za kiyahudi.

Soma Zaidi...
Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Hadithi iliyosimuliwa na tabibu

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME
KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME

Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani.

Soma Zaidi...