Hadithi ya mvuvi na jini

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA MVUVI NA JINI

Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja. Alikuwa anavuwa kwa kutumia nyavu ya kutupa. Alijiwekea sheria ya kutupa nyavu mara nne kwa siku.

 

Alitoka sikumoja asubuhi, akatupa nyavu yake mara ya kwanza na asiambulie kitu. Akarudi nyumbani na kurudi baada ya muda, akatupa nyavu yake na akaambulia mauchavu. Akatupa mara ya tatau akaambulia mauchafu bila ya samaki. Na hapo nyavu yake alikuwa imeharibiwa hivyo akaishona na kuiweka tayari kutupa mara ya mwisho. Mara hii alipotupa aliambukia kuvua lichiupa la shaba lenye mfuniko wa silva.

 

Kwa kutaka kujuwa kilichomo mule akaamua kuofunguwa chupa ile. Akaanza kuitowa kifuniko. Ghafta akaona moshi mkubwa unatoka kwenye ile chupa. Moshi ukajikusanya angani kama kiwingu na punde tu kukatokea jini kubwa sana. “chaguwa mwenyewe kifo cha kukuuwa” ni sauti ya kushangaza ya jini lile. Mvuvi akashngaa kusikia anaambiwa achaguwe kifo.

 

“nimefanya nini mkuu? Na wewe ni nani? Na umetoka wapi?”. Ni fgurushi la maswali ya mvuvi kuliuliza lile jini.

 

“Mimi ni jini nilikuwa nimefungiwa kwenye chupa hii na mkuu wangu, na wewe ndo umenifungulia”. Ni maneno ya jini

Mkuvu akamuuliza “sasa kama nimekufungulia ulipokuwa umefungu ina maana nimekutendea wema , haya mbona unataka kuniuwa”?

 

“nilifanya kosa na mkuu wangu akanifungia humu, miaka mia moja kwa kwanza niliahidi atakaye nifungulia nitampa utajiri mkubwa. Mika ile ikapita na sikupata wa kunifungulia. Miaka nia ya pili nikaahidi atakaye nifungulia nitampa thamani kubwa ya duniani, pia hakutokea wa kunifungulia. Miaka mia ta tatun nikaahidi atakaye nifungulia nitamfanya mfalme na nimpa anachotaka kwa kila siku. Pia miaka hii ikapita bila ya kufunguliwa. Baada ya hapo nikaahidi kuwa atakaye nifungulia nitamuuwa ila nitampa nafasi ya kuchagywa kifo atakachotaka. Hivyo wewe ndo umekuja kunifungulia, chaguwa kifo gani unataka ufe”.

 

Mvuvi akamwambia hule jini, “mimi siamini kama umetoka humu kwe nye chupa. Umeingiaje humu wewe mkubwa hivyo kwenye kichupa kidogo hiki?. Hebu ingia nikuone ndo nitaamini”.

 

Yule jini akajirudisha kwenye jhali ya moshi na akaingia kwenye ile chupa. “umeona sasa nilivyoingia?, nipo kwenye chupa sasa, umeamini?” ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Mvuvi baada ya pale kwa haraka zaidi akachukuwa kifuniko na akaifunga chupa. “sasa nitakurudisha kulekule baharini ulikokuwa.” ni maneno ya mvuvi akimwambia jini.

 

Jini akajitahidi atoke lakini akashindwa ikabidi amwambie mvuvi “ naomba nifungulie, nitakupa utajiri ukunifungulia” mvuvi kwa sauti kubwa akamjibu “hapana siwezi kukutowa usije ukawa umenidanganya. Nitakutupa baharini na nitaweka tangazo hapa ili atakaye ivua chupa ajuwe kuna jini airudishe”.

 

Jini likaanza kujitetea kwa saiti ya kinyonge “nakuomba, nakuahidi pia unifungulie, nitakupa utajiri”. Mvuvi kwa sauti ya busara akamjibu “naogopa yasije yakanikuta yaliyompata tabibu wa mfalme.” “ni yapi hayo yaliyompata tabibu?” ni swali la jini kumuuliza mvuvu. Mvuvi akaanza kusimulia hadithi ya tabibu kama ifuatavyo;-

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1797

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

SAFARI YA SITA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Soma Zaidi...
Safari ya saba ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
TONGE LA MWISHO

Download kitabu Hiki Bofya hapa KWISHA KWA CHAKULA Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MVUVI NA JINI

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MVUVI NA JINI Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja.

Soma Zaidi...
SAFARI YA TATU YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao.

Soma Zaidi...
Kisa Cha mfugaji na mkewe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Kutokana nyani mpaka kuwa chongo

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...