Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU

Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa.mkewangu nilimpenda sana. Niliamini ananipenda sana pia. Bila ya kujua kinachoendelea kumbe alikuwa anajiiba na kuzini na moja ya watumwa wangu pale ndani. Ilichukuwa muda mrefu mpaka nilivyogundu tabia hii mabya ya mkewangu.

 

Basi siku moja nikaaga safari ya dharura lakini lengo langu nilitaka nimtegee ili nimkamate. Niliondoka nyumbani vizuri lakini nikarejea nyumbanni usiku ule na kumkuta mke wangua na yule mtumwa wakiwa wanafanya madhambi. Hali ile iliniumiza sana. Lakini mkewangu hata bila ya aibu akachukuwa maji na kuyasemea maneno ya kichawi na kunimwagia usoni. Hapo nikaanza kuunguwa mwili mzina na hatimaye nikabadilika kuwa mbwa.

 

Basi nilipojiona nimekuwa mbwa nikaondoka pale ndani na kuenda kwenye duka la mfanya biashara mmoja. Yule mfanya biashara akawa ananionea huruma kulikuwa na mbwa wengine wanataka kunipiga basi yule mfanya biashara akawa ananigombea. Ulipofika muda wa mchana binti yake mfanya bishara akaja kumletea chakula baba yake. Ghafla tu macho yangu na ya yule binti yalipo kutana nikahisi hali flani ya mabadiliko usoni kwa yule binti.

 

Baada ya mfanya biashara kual akanipatia mabaki yale ya chakua na kunipatia. Yule binti akamuuliza baba yake “baba umepata wapi mbwa mzuri huyu?”. “hapana amekuja mwenyewe hapa”. Basi binti akamwambia baba yake “baba uanjuwa huyu sio mbwa wa awaida, huyu ni binadamu aliyegeuzwa mbwa” niliposikia maneno yale nikawa natingisha kichwa isara ya kuyaunga mkono maneno yale. “sasa unaweza kumrudisha katika hali ya kawaida?” aliuliza mfanya bishara. “ndio baba naweza” ni majibu ya binti.

 

Basi binti akachukuwa maji na akayasemea maneno yasiyo eelweka na kunimwagia usoni. Palel aple nikawa katika umbo la kawaida. Kisha akamwendea mke wangu na kumgeuza kuwa mbwa kama alivyonifanya mimi. Kisha akanielekeza sehemu ya kukutana nae itakapofika miaka 10. Hivyo miaka 10 sasa imefika ndio niko safarini kukutana nae ili amrudishie mke wangu umbo lake mwenyewe. Ndio nikakutana na nyinyi hapa. Basi waztu wote wanne wale wakaachana pale na kila mmoja akaenda na safari zake.

 

Baada ya kumaliza hadithi hii Schehra-zade akamwambia mdogo wake “vip unaionaje hadithi hii” “mmmmhmmh … Ni nzuri sana dada, ila ni ipi hadithi ya yule mzee wa tatu”? Ni maneno ya Dinar-zade. “hata mimi sijui ila naamini ni nzuri zaid, lakini haiwezi kushinda hadithi ya mvuvi na jini” alisikika Schehra-zade akimweleza mdogowake. Sultani akadakia “ooh, kama hii nzuri hivi vp hiyo ya mvuvi na jini, natamani kuisikiliza,”

Schehra-zade akaongea “kama utanipa siku nyingine zaidi naamini utaflaiya hadithi hii”. Basi siku ile Schehra-zade hakuuliwa na siku ilofata mfalme akamuleza asimulie hadithi ya mvuvi na jini. Schehra-zade bila ya kuchelewa kaanza kusimulia kama ifuatavyo

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 2101

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA SAFARI SABA ZA BAHARIA SINBAD

SAFARI SABA ZA SINBADKatika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo.

Soma Zaidi...
SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME.

Soma Zaidi...
Safari ya sita ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Kuelekea bonde la uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...