image

Hadithi ya mke na kasuku

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

HADITHI YA MKE NA KASUKU.

Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara, ambaye alikuwa na familia yake na mkewe ambaye alimpenda san. Hakuamini kama atakuja kuachana naye. Kwakuwa yeye ni mfanya biashara alikuwa akisafiri mara kwa mara. Ijapokuwa kuanwatu walikuwa wakimpa maneno kuhusu mkewe alikuwa ahawaamini. Ilifikia wakati sasa aliingiwa na mawazo ya kutaka kuwaamini japo hakufanya hivyo,

 

Sikumoja alipopata safasi alikwenda kwenye maduka yanayouzwa ndege wa kufuga. Alinunuwa kasuku mmoja laiye mzuri sana. Kasuku huyu pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza habari zilizofanyika wakati bwana wake hayupo. Alimnun ua kasuku yule kwa gharama za juu na akamuweka kwenya kitundu chake. Alimpelekea mkewe na kumwambia “mtunze ndege wangu huyu, na umuweke ndandi na katu usimtowe”. Mke alitii ankumchukuwa kasuku yule na kumugifadhi ndani.

 

Mfanya biashara huye alitoka na kuenda mbali ya mji. Huku nyuma mkewe akafanya ya kuyafanya pale ndani. Ulipofika wakati mfanya biashara alirejea nyumbani. Alimchukuwa kasuku wake na kutoka naye nyumbani ili kutafute mahala pa faragha kisha akamuuliza kasuku kilichofanyaka pale ndani wakati hayupo. Kasuku aliyasema yote aliyoyaona na hayakumpendeza yule mfanya biashara. Aliporejea nyumbani aligombana saa na mkewe. Mke alishangaa ni nani alomwambia. Aliwapa adhabu watumishi wake akidhani ndio walovunja siri. Ila baada ya muda akagunduwa kuwa ni kasuku ndiye muongo.

 

Mfanyabiashara laipata safari nyingine ya kibiashara. Alipoondoka yule mkewe alipotaka mufanya anayoyafanyaga aliwaita wajakazi wake watatu. Mmoja akamwambia aweke beseni la maji chini ya tundu la kasuku, na mwengine akamwabia maji juu ya tundu la kasuku na mwinguni akamwambia achukuwe kioo na kwa kutumia mwanga wa mshumaa ammulike kasuku kwa mwanga uloakisiwa na kioo. Akamwambia afanya hivi kulia na kushoto. Wakati mambo yote haya yakifanyika yule mke nae alikuwa akifanya mambo yake anayoyafanyaga wakati mumewe akiondoka.

 

Siku ilofata mfanyabiashara akarudi nyumbani. Akamuuliza kasuku kilichotokea kasuku akamwambia “mmh bwana wangu mvua ilikuwa kubwa pamoja na radi nilishindwa kujuwa kinachotokea.” yule mfanyabiashara alijuwa kuwa hakuna mvua ilonyesha usiku ule. Akaona kuwa kasuku ni muongo hivyo akaamua amchinye. Baada ya siku akaja kugunduwa kuwa kasuku alikuwa mkweli ila alichezewa mchezo, alijilaumu sana lakini lawama zisingemrudisha kasuku.

 

Baada ya kumaliza kuzungumza hadithi hii (mvuvi akamwambia jini maneno aliyoyasema ) mfalme akamwambia waziri “sitakusikiliza kwa hili, nitamshughulikia tabibu na kama nisije nikajuta kama mfanya biashara alivyojuta baada ya kumuuwa kasuku asiye na hatia”. Waziri akajibu “mfalme tabibu anataka kukuuwa, siwezi kumuacha na kama itatokea nimefanya kosa nitakuwa tayari kuadhibiwa kama alivyoadhibia waziri wa mfalme flani” “alifanya nini huyo waziri” ni swali aliodakia mfalme. Waziri akasimulia hadithi ifuatayo;-





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1035


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya kwanza): KIAPO CHA SULTAN
Soma Zaidi...

Binti wa ndotoni
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

KUELEKEA BONDE LA UOKOZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUELEKEA BONDE LA UOKOZI Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi. Soma Zaidi...

Alif lela u lela 1
Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa. Soma Zaidi...

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI
Soma Zaidi...

BINTI WA NDOTONI
Download kitabu Hiki Bofya hapa BINTI WA NDOTONI. Soma Zaidi...

Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

MWANZO WA USALITI
Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Soma Zaidi...

MALIPO YA WEMA NI WEMA
Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MVUVI NA JINI
Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...