Menu



Safari ya nne ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

SAFARI YA NNE YA SINBAD

Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Tulianza safari ile usiku hata ikafika asubuhi tukiwa katikati ya maji. Njia ya safari hii sikuwa na uzoefu nayo na niliona mambo mapy. Niliweza kuona majabali yalofanana na watu, wanyama na vitu mbalimbali. Pia tuliweza kuona mawe ya ajabu ambayo huwa hayapati maji sikuzote. Tukiwa karibu ya kuingia kwenye kisiwa chetu cha kwanza kwa ghafla tulivamiwa na majiwatu makubwa na yenye nguvu sana.

 

Watu hawa walifanikiwa kututeka sote tuliokuwa mule ndani ya jahazi lile. Walitukamata wote na kutufunga kamba na kutuziba macho yetu kwa vitambaa hata tusione wapi tunakwenda. Walitupeleka tusikokujuwa na kwa kuelewa tu niliona kama tunarudinyuma. Waliturudisha nyuma kwa muda wa takribani masaa matatu kisha tukaelekea upande wa kushoto na kukiwacha kile kisiwa tulokuwa tukikiona kuliani. Tulikwenda kwamuda wa takribani masaa sita. Nikiwa nachukuwa hisia juu ya safari ili niligunduwa kumbe wanatuzungusha tuu lakini tunatupeleka pale kwenye kisiwa kile tulichokiona.

 

Hatimaye tukawasili na wakatufungua machoyetu na hapo nikapata tena kuona ardhi nzuri yenye udongo mweupe wa kupendeza. Wale watu wakawa wanagawana kila mmoja kucukuwa watu kadhaa katika sisi. Waligombaniana watu wote na kubakia mimi. Walichelea kunichagua kwa sababu nilikuwa nimekonda sana. Basi akatokea mzee mmoja wa heshima katika wao akanichukuwa. Basi wote tuliingizwa kwenye jumba moja na kuletewa chakula kilichofanana na machicha ya nasi. Bila ya kuchelewa wenzangu wakaanza kula chakula kile ila mimi nikachelea kukila hata kikaisha.

 

Baada ya muda tukaletewa majani mithili ya majani ya miwa lakini haya yana maji mengi na ni matamu sana. Mimi sikuyala kwa kuhofia usalama wangu. Niliweza kugunduwa ladha yake kwa kuhadithiwa na wenzangu. Nilikaa na njaa kwa muda wa siku mbili hata nikakosa nguvu. Yule mzee akamiletea samaki wa kuchoma pamoja na mayai ya kasa. Nilikula sana hata nikashiba. Nilipopata nduvu ziku ya tatu nikaona mabadiliko kwa wenzangu. Walikuwa wakinenepa sana kwa ghafla kila walipokula vyakula vile. Kitu cha kushangaza wakawa wanapoteza kumbukumbu na kuwa na akili ya kinyama kinyama.

 

Hali iliendelea hivi kwa muda wa wiki tatu hata akawa mmoja kati ya wenzangu hawezi kupita kwenye mlago kwa unene. Basi wale watu wakawa wanamchukuwa mtu mmojammoja kila wiki na kuondoka nae na asirudi. Nikawa nafatilia nini kinaendelea hata nikagunduwa kuwa wanakwenda kumchinja na kumuuza nyama kwenye kisiwa kingine. Niolijaribu kuwaeleza wenzangu lakini wamekuwa wanyama hakuna walijualo zaidi ya kula tu. Mimi niliendelea kula vyakula kwa kuiba na hali yangu ikazidi kudhoofu.

 

Yule mzee akaamuwa kunitoa bandani mule kwa kuamini nikiwa huru naweza kunenepa. Hali iliendelea hivyo hata nikapewa funguo ya kuwalinda wenzangu. Waliendelea kuchinjwa hata wakabakia watu kumi na mbili. Kuna siku kulikuwa na sherehe na watu wakaondoka na kuniacha mimi na yule mzee. Basi nilitoroka pale peke angu kwani ningemhukuwa yeyote asingekubali na kwa unene na uzito alonao asingeweza kukimbia hata kidogo. Basi nilitoroka kwenda mbali zaidi.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views 917

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

BINTI WA NDOTONI

Download kitabu Hiki Bofya hapa BINTI WA NDOTONI.

Soma Zaidi...
Usuluhishaji wa walio dhurumiwa

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Safari ya majibu juu ya maswali mawili

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
KISIWA CHA UOKOZE CHA PILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.

Soma Zaidi...
SAFARI YA TANO YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TANO YA SINBAD Baada ya watu kukusanyika siku ilofata sinbad akaanza kusimulia stori ya safari yake ya tano.

Soma Zaidi...
KISIWA CHA UOKOZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli.

Soma Zaidi...
KIAPO CHA SULTANI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KIAPO CHA SULTANI.

Soma Zaidi...
Safari ya pili ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...