الحديث التاسع والعشرون
"تعبد الله لا تشرك به شيئا"
عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ)) .ثم قال: (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: {تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ} - حتى بلغ - {يَعْمَلُونَ} السجدة: 16-17 .
ثم قال: ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال: (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).
ثم قال: (( ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت : يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ, وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ )) أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ ألسِنَتهم))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Mu'aadh Ibn Jabal رضي الله عنه amesema:
Nilisema: Ewe Mtume صلى الله عليه وسلم , niambie kitendo ambacho kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto. Akasema : Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambae Mola anaemsahilishia. Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zaka, funga Ramadhani, nenda kuhiji (Makka). Kisha akasema: Je? Nikuonyeshe milango ya kheri? Saumu ni ngao, sadaka inazima dhambi kama vile maji yanavyozima moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma {Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda}
Sura As-Sajda 32: 16 na 17
Tena akasema: Je, nikwambie kilele cha hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa? Nikasema : Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akasema: kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swala na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad. Kisha akasema : Je, nikwambie muhimili wa yote haya? Nikasema: Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu. Akaukamata ulimi wake na akasema; Uzuie huu. Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu; yale tunayoyasema tutahukumiwa kwayo? Akasema: mama yako akuhurumie ewe Mu'aadh! Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si mavuno ya ndimi zao?
Imesimuliwa na At-Tirmidhi na ni hadithi Hasan.