Chemsha bongo 07

imageimage
22.Busara za mfalme
Hapo zamani kulikuwa na mfalme. Mfalme huyu hakuwa hata na mtoto wa kumrithi. Na alishakuwa amezeheka sana. Hivyo akaamuwa kutowa mbegu mbalimbali za miti kuwapa watoto wa nchini na akasema yeyote atakayeotesha mti mzuri kuliko wenzie kutoka katika hizi mbegu ninazotoa atkuwa ndiye mrithi wangu.

Baada ya miezi mitatu maelfu ya watoto wakaja ikulu kuleta miti yao waloiotesha kwenye makopo na mitungi. Mtoto mmoja tu yeye alikuja na kopo tupu ambalo halikuwa na mti, bali lilikuwa na udogo tu. Mwisho mfalme alimshagua huyu mtoto kuwa ndiye mrithi. Umadhani ni kwa nini?
Jibu.
Ni kwa sababu mfalme aliwapa mbegu feki. Na huyu mtoto hakufanya udanganyifu wa kuotesha mbegu nyingine tofauti na ile alopewa na mfakme.