Haki na Wajibu wa mume kwa mkewe na familia

Haki na Wajibu wa mume kwa mkewe na familia

Wajibu wa Mume kwa Mkewe



Katika jamii za kikafiri, mwanamke alifanywa kama mtumishi au kama mtumwa. Katika baadhi ya jamii hizo, mwanamke aliangaliwa kama kifaa kingine cha nyumbani. Kwa upande mwingine, mwanamume katika jamii hizi hakuwa na wajibu wowote kwa mkewe, bali mkewe ndiye tu aliyelazimika kuwajibika kwa bwana wake. Mpaka hivi leo, katika jamii nyingi uhusiano wa mume na mke ni ule wa "Bwana" na "Mtumwa" wake. Uhusiano wa mume na mke katika Uislamu ni ule wa mtu na mwenzie au mtu na mpenzi wake. Tumeshaona kuwa uhusiano huu wa mume na mke ndio lengo kuu Ia ndoa. Kama tunavyojifunza katika Qur-an:


"Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu iii mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu " (30:21).
Mapenzi na huruma baina ya Mke na Mume vitakuwepo tu endapo kila mmoja atatekeleza wajibu wake kwa mwenziwe kwa kadiri ya uwezo wake na kwa upendo na huruma. Mume anawajibika kwa mkewe:



(i)Kumlisha, kumvisha na kumpatia makazi
Mwanamume na amgharimie mkewe kwa kadri ya uwezo wake.


Mwenye wasaa agharamike kadri ya wasaa wake, na yule ambaye amepungukiwa riziki yake, atoe katika idle alichopewa na Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu hamkalflshi mtu yeyote ila kwa kadri ya alichompa. Atajaalia Mwenyezi Mungu baada ya dhikifaraja. (65:7).


(ii)Kumtendea wema, kumhurumia na kumpenda


Na kaeni nao kwa wema; na kama mkiwachukia basi (msiwawache) kwani huenda mkachukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake. (4:19).
Katika hadithi iliyosimuliwa na Aisha (r.a), Mtume (s.a.w) amesema:



Mbora miongoni mwenu ni yule aliye mbora katika (kuwatendea wema) familia yake na ni mbora wenu katika familia yangu... (Ibn Majah).
Pia Abu Hurairah (r.a) kasimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Muislamu aliyekamilika kweli kweli miongoni mwenu katika imani ni yule aliye mbora wao katika tabia, na wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao. (Tirmidhs, Abu Daud).



Katika Qur-an na hadithi wanaume wamesisitizwa sana kuwafanyia wema wake zao, na kuwaonyesha upendo na huruma. Iii kuzidisha mapenzi, inapendekezwa kwa mwanamume kuwa, pamoja na kumpatia mkewe mahitaji muhimu, mara kwa mara amletee zawadi kila atakapopata wasaa. Vile vile, mume ameshauriwa mara kwa mara apate muda wa kucheza na kutoka na mkewe kwa matembezi. Tunajifunza katika hadithi nyingi kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akicheza na wakeze na kufanya maskhara nao.



(iii)Kujizuia na kumchukia mkewe
Chuki ni kinyume cha upendo. Kumchukia mke ni doa kubwa katika nyumba, hivyo mwanamume anatakiwa ajitahidi kujiepusha na kumchukia mkewe, kwa kuyabeza maudhi madogo madogo yasiyo ya msingi kama Mtume (s.a.w) anavyotushauri katika hadithi ifuatayo:


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Mwanamume aliyeamini asimchukie mwanamke aliyeamini. Kama anachukia kipengele kimoja cha tabia yake, atafurahishwa na kipengele kingine kizuri katika tabia yake. (Muslim).



Hadithi hii inasisitiza kuvumiliana kwa kuyaangalia mazuri ya mtu na kuyafumbia macho mabaya yake. Kwani ni muhali mwanaadamu kukosa mabaya, angalau kidogo. Hakuna binaadamu aliyekamilika



(iv)Kujizuia kumpiga au kuwa mkali sana kwake:
Mwanamume haruhusiwi kumpiga mkewe kwa makosa madogo madogo. Haruhusiwi kumpiga fimbo au kofi Ia usoni bali anaruhusiwa kumpiga kwa nguo au mti wa mswaki kiasi cha kumpa onyo. Kabla ya kufikia hatua hii ya kuwapa onyo Ia kipigo hiki hafifu, tumeambiwa katika Qur-an tuwaonye kwa mawaidha na tuwahame katika vitanda mpaka watakapojirekebisha (4:34). Mtume (s.a.w) ametushauri katika hadithi mbali mbali kuwa, tuwe na subira na ustahamilivu juu ya wake zetu, kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



ilyas bin Abdullah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Msiwapige v/akazi vya Mwenyezi Mungu (wanawake). Kisha Umar(r.a) alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Wanawake wanawakalia (hawawajali waume zao sasa. Kwa hivyo (Mtume) aliwaruhusu wawapige. Kesho yake (baada ya ruhusa hii) wanawake wengi wakawa wanaranda randa katika mazingira ya nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu wakilalamika dhidi ya waume zao. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: "Wanawake wamerandaranda nyumbani kwa Muhammad wakilalamika dhidi ya waume zao. Wanaume hao sio bora miongoni mwenu." (Abu Dawud, Ibn Majah).



Hadithi hii inatuweka wazi kuwa, japo kupiga kunaruhusiwa, lakini kisiwe kipigo kikubwa cha kuumiza. Hata hicho kipigo hafifu si jambo linalopendeza mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake. Mtume (s.a.w) ambaye ni kiigizo chetu, hatuoni popote alipothubutu kumnyoshea mkono, yeyote katika wake zake, japo baadhi yao walikuwa wakorofi. Tunajifunza kuwa kutokana na ukorofi wa wakeze, aliwahi kuwahama kwa kipindi cha mwezi mmoja. Iii tuweze kuishi vizuri na wake zetu, hatuna budi kuwavumilia na kuwachukulia kuwa ndilo umbile lao, kama Mtume (s.a.w) anavyotushauri katika hadithi zifuatazo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Kuweni wema kwa wanawake, kwani wameumbwa kutokana na sehemu ya juu ya ubavu, na sehemu iliyopinda kuliko zote katika ubavu ni sehemu yajuu. Kwa hiyo kama utataka kuinyoosha utaivunja, na kama utaiacha hivyo hivyo itaendelea kupinda. Kwa hiyo wawaidhini wanawake (waonyeni) kwa kadri iwezekanavyo. (Bukhari na Muslim).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Hakika mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu ambao kamwe hautakunyookea unavyotaka (kupinda ndio umbile lake). Kama unamfurahia mkeo, utamfurahia pamoja na kupinda kwake, kama utataka kunyoosha, utamvunja, na kuvunjika kwake ni talaka. (Muslim).
Hadithi hizi zinatuthibitishia kuwa, hapana mtu atakayedumu na mkewe, kama hapatakuwa na kuvumiliana. Mwanamume asimtegemee mkewe kuwa na msimamo kama ule wake, ajue kuwa kila mmoja, kulingana na nafasi yake ana umbile tofauti. Hivyo ni lazima wanaume wawe wavumilivu sana kwa wake zao ili papatikane amani, upendo na furaha katika familia.



(v)Kutunza Sin za Unyumba:
Ni jambo baya sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) mtu kutoa sin za nyumbani kupeleka nje hasa zile zinazohusu unyumba. Utoaji wa sin za unyumba unaondoa uaminifu kati ya mke na mume, unaondoa upendo kati yao, na unatoa mwanya kwa maadui kuwaingilia na kuvunja nyumba yao.


(vi)Kuwa Muadilifu:
Mwanamume akiwa na mke zaidi ya mmoja, awe muadilifu na kuwagawia haki zao pasina upendeleo wowote. Ikitokea kuwa kuna kitu ambacho hakiwezekani kugawanyika itabidi wake zake wote waamue kwa pamoja kuwa nani kati yao apate kitu hicho kwa niaba ya wengine Ia sivyo itapigwa kura, na kitu hicho kitakuwa ni cha yule atakayeangukiwa na kura. Mtume (s.a.w) ambaye ni kiigizo chetu, alikuwa muadilifu mno na mwenye kugawa haki sawa kwa wake zake kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akigawanya ngono kwa wake zake kwa usawa. Alikuwa akisema: "Ee Mwenyezi Mungu huu ndio mgawanyo wangu kulingana na uwezo wangu. Hivyo usinipatilize kwa idle ulicho na mamlaka nacho, ambacho mimi sina. (Tirmidh, Ahmed, Nisai).



Mtu kupendelea baadhi ya wakeze katika kuwapa haki zao, ni jambo baya mno, ambalo linaweza likawa ndio sababu ya mtu kuingia motoni kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mtu mwenye wake wawili akawa anampendelea mmoja kati yao, atakuwa siku ya Kiyama na upande mmoja unaoning 'inia chini. (Tirmidh, Abu Daud, Nisai).



Mwanamume akijitahidi kumpa mkewe haki zake na akawa muadilifu kwake, akajitahidi kuonesha mahaba kwake na akawa mvumilivu na mwenye subira juu ya udhaifu wake, kwa vyovyote vile atapendana na kushikamana vilivyo na mkewe endapo mkewe atakuwa ni Muumini na mcha-Mungu.



(vii) Kusimamia maadili ya kiislamu na ucha-Mungu
Ni wajibu wa mwanamume wa Kiislamu kuhakikisha kuwa mkewe/wakeze wanaujua Uislamu kwa usahihi wake na kujitahidi kuwa wacha-Mungu katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kibinafsi, kifamilia na kijamii. Pamoja na jitihada za wanaume wa kiislamu katika kusimamia maadili ya wake zao, ikiwa ni pamoja na kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu, hawanabudi kuomba msaada wa Allah (s.w) kwa kuleta dua aliyotufunza:


"... Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho (yetu) na utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu "(25:74).
Uamrishaji mema na ukatazaji mabaya kwa wake zetu hautakuwa na athari yoyote kama hatutakuwa kiigizo chema katika kufanya mema na kuacha maovu.
Mwanamke anapovunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake, mumewe amuonyeshe ubaya alioufanya na amuhimize kuleta toba ya kweli kama Allah (s.w) anavyotuamrisha:


Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli; huenda Mola wenu akakufutieni maovu yenu na kukuingizeni katika Pepo zipitazo mito mbele yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Mtume wala wale walioamini pamoja naye; nuru yao itakuwa inakwenda mbele yao na pande zao za kulia (na kushoto); na huku wanasema: 'Mola wetu! Tutimizie nuru yetu, na utughufirie, hakika wewe ni Mwenye uwezajuu ya kila kitu". (66:8).


Mke akirudia kosa Ia kumuasi Allah (s.w) na Mtume wake, mumewe amuase kwa mawaidha makali akionyesha kutoridhika kwake kutokana na uasi wake na akirudia tena kukaidi mume ajitenge naye kitandani kama kiashiria cha mwisho wa kumvumilia. Talaka itakuwa hainabudi kama mke huyo atazidi kukaidi kwa kuzingatia aya ifuatayo:


"Sema: Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu, ni vpenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania Dini yake, Basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu waasi" (9:24)




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 352

Post zifazofanana:-

Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake
Kwa nini unapata maumivu makali wakati wa kuingia hedhi, je unajuwa sababu za maumivu makali ya tumbo la chago. Soma Zaidi...

Nataka nijue siku ya kubeba mimba mwanamke
Soma Zaidi...

DUA YA MUUMINI NA DUA YA KAFIRI
DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI. Soma Zaidi...

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza
Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili. Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa 'Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili. Soma Zaidi...

NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

fangasi wa kwenye Mdomo na koo
Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

Matatozo katika choo kidogo, maradhi ya figo na dalili zake pia namna ya kujikinga na madhradhi ya figo
MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili. Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Soma Zaidi...