Dalili za ugonjwa wa macho.

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa macho, ugonjwa huu kwa kawaida una dalili kuu tano kadri ya maambukizi yanavyoongezeka na madhara yake kwa hiyo tunapaswa kujua dalili hizo Kama ifuatavyo.

Dalili za ugonjwa wa macho.

1. Dalili ya kwanza ni pale mdudu anapotua kwenye jicho na jicho hilo kwa kawaida uanza kuwa jekundu,kuwashwa, kuwa maji maji yanayotoka kwenye jicho yanaweza kuwa yote mawili au Moja na pengine kadri siku zinavyoenda jicho linaweza kuwa na mayongo to go kila mara , kwa hiyo kama ni mtoto mdogo wazazi wanapaswa kuwa macho Ili kuweza kumsaidi kwa kumpatia matibabu mapema.

 

2. Dalili ya pili ni pale maambukizi yanavyozidi ndivyo yanaendelea kuwa na uvimbe kwenye jicho ambao kwa kitaalamu huitwa oedema, uvimbe huh unaweza kuwa juu ya jicho na pengine unatoa usaha au maji maji kwa hiyo ikitokea uvimbe huu ukapsuliwa na maji maji yakagusa kwenye jicho la mtu ambaye Hana maambukizi ndio mwanzo wa maambukizi kuanza 

 

3. Katika hatua hii ya tatu maambukizi uzidi na kusababisha uvimbe ulipokuwa kwenye jicho kutengeneza kofu kwenye jicho na kukaribia kufunika jicho Ilo kovu kwa upande mwingine linaweza kuwa na maumivu au kutokuwepo kwa maumivu kwa hiyo kwenye hatua hii ugonjwa unaweza kutibika ni vizuri kabisa kutibu maana ukizidi hapa ni hatari.

 

4. Hatua hii ya nne ni pale maambukizi yakizidi zaidi ambapo kovu lililotengenezwa kuwa kubwa na kuongezeka kwenye jicho na kukaribia kufunika jicho na sehemu mbalimbali za jicho ubadilika kwa hatua hii mtu uanza kuona kwa shida, hatua hii upasuaji ni wa lazima kwa sababu kupona ni vigumu.

 

5. Hatua ya tano na ya mwisho ni pale ambapo mtu anashindwa kuona kabisa yaani makovu yanafunika jicho na pia kabla ya hapo mtu uanza kuona maluwe luwe hatimaye jicho Linaziba kabisa ndo upofu unatokea, kwa hiyo tunapaswa kuelewa kuwa ugonjwa huu unatibika sana na dawa zipo kwa wingi hospitalini kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka wagonjwa wetu hospital Ili waweze kupata huduma inayofaa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/04/23/Saturday - 06:18:39 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1650


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-