Katika somo hili utajifunza aina tano za kuweka rangi kw akutumia css
Tumesha jifunza katika masomo ya nyuma jinsi ya kuweka rangi. Rangi inaweza kuwa ni kwa ajilia backround ama kwa ajii ya text. Kama tulivyojifunza huko awali, property background hutumika kwa ajili ya ku set rangi kwa ajili ya background, na propert ya color hutumika ku set rangi ya text
p{
background: black;
color: blue;
}
Tofauti na hizo mbili kuna nyingine ya kuweka rangi kwenye borders. Hii inaitwa border
Mfano:
p{
border: solid #d00c0c;
}
Namna za uwekaji warangi
Katika css kuna aina tano za kuweka rangi kwenye faii la html. Njia hizo ni :-
Kwa kutumia jina la rangi ni kama tulivyofanya hapo juu. Utaitaja rangi hyo kwa jina. Jambo la msingi ni kujuwa tu majina ya hizo rangi kwa ufasaha. Mfano red, blue, black, yellow, green, purple n.k. Nikama tulivyofanya hapo juu.
p{
background: black;
color: blue;
}
2. Kwa kutumia Hex color
Kuna baadhi ya rangi majina yake huyajui, saa utatumia thamani zake za hex color. Hex color zipo katika namna mbili ambzo ni kwa kutumia herufi ama kwa kutumia namba. Njia yeyote utakayotumia utaanza na alama ya reli yaani hash #. Baada ya kuandika # itafuatiwa na character 6 kama ni herufi ziwe 6 na kama ni namba ziwe 6.
Mfano:
p{
background: #000000;
color: #160ee7;
}
Unaweza kuzi generate mwenyewe kwenye text editor. Ama w3schools wanayo system ya ku generate hex color free.
3. Kwa kutumia RGB
RGB ni kifupisho cha maneno Red, Green, Blue. kwa hiyo ni kitendo cha kuchanganya rangi hizo tatu ili kupata rangi nyingine. Kwa mfano ukicanganya rangi nyekundu, ya kijani na buluu kwa uwiano sawa utapata rangi nyeupe.
p{
background: rgb(255, 255, 255);
color: rgb(0,0,0);
}
Kwenye css editor itaonekana hivyo
...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKatika somo hili utakwenda kujifunza maana ya CSS, pia nitakujulisha kazi zake. Mwisho utatambuwa historia ya CSS toka kuanzishwa.
Soma Zaidi...katika somo hili utajifunza jinsi ya ku install css kwenye ukurasa wa html
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria za uandish wa css yaani syntax za css
Soma Zaidi...