Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria za uandish wa css yaani syntax za css
Sheria za uandishi wa css yaani syntax za css.
Css ni moja katika lugha za ki kompyuta (computer language) ambayo ina sheria zilizo rahisi sana na ni chache. Ukishazijuwa hizo basi mabo yote yatakuwa sawa.
Sheria za kuandka css zimezama kwenye mambo makuu mawili tu ambayo ni selector na declaration. Yaani code zote za css unaweza kuzigawa kwenye sehemu kuu hizi mbili ambazo ni selector na declaration.
Selectors: hii ni sehemu ambayo yenyewe inahusisha element za html. Yaani hapa ndipo tunakwenda kujuwa je hizo code za css zinahud element gani. Mfano ukisema
haloo
katika code hizi selector ni
ambapo inaonesha kuwa tuna target paragraph.
Declaration: hii ni sehemu ambayo inakwenda kuweka code za css. Declaration yenyewe imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni property na value. Kwa mfano katika mfano niliotoa hapo juu declaration ni color:yellow ambapo tunapata color ni property na yellow ni value.
Kwa ufupi selector ina kuwa na tag husika ya html na declaration inakuwa na protery pamoja na value. Declaration inakuwa kwenye mabano ya {} kama utatumia internal css ama external css.
Selector inaweza kuwa zaidi ya moja na declaration pia inawezakuwa zaidi ya moja. Jambo la kuzingatia nikiwa unapotumia selector zaidi ya Moja utatakiwa kuzitenganisha kwa alama ya koma (,). Na unapotumia declation zaidi ya Moja utatenganisha kwa kutumia semicolon (;). Angalia mfano hapo chini
p, h1, u, i, b{
color:blue;
font-size:200%;
background: red;
}
Katika code hizi selectors ni p, h1, u, i na b hizi zinatarget tag za html. Tag hizo ni <p>, <h1>, <u>, <i> na <b>. Kwa pamoja element hizo zote zitafuata style hiyo popote zitakapotumiwa.
Pia ha">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download Nowkatika somo hili utajifunza jinsi ya ku install css kwenye ukurasa wa html
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza aina tano za kuweka rangi kw akutumia css
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya CSS, pia nitakujulisha kazi zake. Mwisho utatambuwa historia ya CSS toka kuanzishwa.
Soma Zaidi...