Katika somo hili, utajifunza kuhusu pseudo-classes kama :hover, :first-child, na :last-child, pamoja na pseudo-elements kama ::before, ::after, na ::selection. Hizi husaidia kubadili au kuongeza mitindo maalum kulingana na hali ya elementi au sehemu maalum ya elementi.
Pseudo-classes na pseudo-elements ni sehemu muhimu ya CSS ambazo hukuwezesha kubadilisha mwonekano wa elementi kulingana na hali fulani au kuongeza content ya ziada bila kubadilisha HTML. Ni zana muhimu sana kwenye ubunifu wa kipekee na mwingiliano bora wa mtumiaji.
:hoverInatumika kubadilisha style ya element unapoelekezewa pointer ya mouse.
button:hover {
background-color: green;
color: white;
}
💡 Inafaa sana kwa vitufe (buttons), links, na menyu.
:first-childHuchagua elementi ya kwanza ndani ya mzazi wake.
p:first-child {
font-weight: bold;
}
:last-childHuchagua elementi ya mwisho ndani ya mzazi wake.
li:last-child {
color: red;
}
::beforeHuchomeka content kabla ya element kuonekana.
p::before {
content: "👉 ";
}
::afterHuchomeka content baada ya element.
p::after {
content: " ✅";
}
💡 Zinafaa sana kwa kuongeza icons au alama bila kubadilisha HTML.
::selectionHubadilisha mwonekano wa maandishi yanapochaguliwa (highlighted).
::selection {
background: yellow;
color: black;
}
<p>Hii ni paragraph ya mfano.</p>
p:hover {
color: blue;
}
p:first-child {
text-transform: uppercase;
}
p::before {
content: "💡 ";
}
p::after {
content: " 📘";
}
Pseudo-classes na pseudo-elements huongeza nguvu ya CSS bila kuingilia HTML. Zinaruhusu kufanya mabadiliko ya hali (state), kuchagua elementi maalum, na kuongeza content ya ziada kwa ubunifu. Ni nyenzo muhimu sana kwenye urembo na usability ya tovuti.
Tutajifunza jinsi ya kuleta miondoko (motion) kwa kutumia transition, transform, na animation kwenye CSS.
:hover hutumika lini?
a) Wakati wa kubonyeza tu
b) Wakati element inaonekana tu
c) Wakati pointer ya mouse iko juu ya element
d) Wakati element iko mwisho wa HTML
::before hufanya nini?
a) Kubadilisha background ya element
b) Kuongeza content kabla ya element
c) Kuficha element
d) Kuweka margin mpya
Ili kuchagua element ya mwisho ndani ya mzazi, utatumia:
a) :hover
b) :nth-child(1)
c) :last-child
d) ::after
::selection hutumika wapi?
a) Kwenye picha pekee
b) Kubadilisha style ya content inayo-highlightiwa
c) Kubadilisha background tu
d) Kuweka icon
Kipi kati ya vifuatavyo ni pseudo-class?
a) ::after
b) :hover
c) ::selection
d) ::before
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutajifunza kuhusu CSS Timing Functions, ambazo hutumika kudhibiti kasi na mtiririko wa transition na animation. Utaelewa tofauti kati ya ease, linear, ease-in, ease-out, ease-in-out, pamoja na jinsi ya kutumia cubic-bezier() kwa kudhibiti mwendo wa mabadiliko kwenye elementi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza aina tano za kuweka rangi kw akutumia css
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunza aina za css selectors
Soma Zaidi...Somo hili linakuletea ufahamu wa kina juu ya CSS Transitions na Animations, likifafanua vipengele vyake muhimu, matumizi, na namna ya kutumia properties mbalimbali za animation kwa ufanisi katika kurahisisha muonekano na mtumiaji wa tovuti.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria za uandish wa css yaani syntax za css
Soma Zaidi...katika somo hili utajifunza jinsi ya ku install css kwenye ukurasa wa html
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza jinsi ya kudhibiti muonekano wa sehemu ya nyuma (background) ya HTML element kwa kutumia CSS. Utaweza kuongeza rangi, picha, kuweka picha zisirudiwarudiwe, na hata kusogeza picha kwenye maeneo tofauti ya ukurasa.
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza vipengele vya juu zaidi vya Flexbox: flex-wrap, flex-grow, flex-shrink, na flex-basis. Pia tutajifunza jinsi ya kujenga muundo wa safu (rows) na nguzo (columns) kwa kutumia Flexbox layout.
Soma Zaidi...Katika somo hili, utajifunza msingi wa mfumo wa Flexbox unaotumika kupanga elementi kwa usahihi ndani ya kontena. Utajifunza kuhusu display: flex;, pamoja na properties muhimu kama justify-content, align-items, flex-direction, na gap.
Soma Zaidi...Katika somo hili, tutajifunza kuhusu CSS functions muhimu zinazotumika kufanya mahesabu, kuweka vipimo vya kisasa vinavyobadilika kulingana na hali ya kifaa, na kutumia variables. Tutazingatia functions kama: calc(), clamp(), var(), min(), max(), na mwishoni tutajifunza jinsi ya kutengeneza custom function kwa kutumia variables.
Soma Zaidi...