Ndoa ya kwanza ya kamaralzamani

NDOA YA HAMU Basi hali ikawa kama hivyo wawili hawa binamu na Kamaralzamani wakaanza kupanga njama ya kuweza kuondoka eneo lile kuelekea nchi za mbali kwa ajili ya kukutana na binti mfalme.

Ndoa ya kwanza ya kamaralzamani

NDOA YA HAMU
Basi hali ikawa kama hivyo wawili hawa binamu na Kamaralzamani wakaanza kupanga njama ya kuweza kuondoka eneo lile kuelekea nchi za mbali kwa ajili ya kukutana na binti mfalme. Basi Kamaralzamani akapanga njama ya kuwa aende kuwinda ili kiruhusiwa hukohuo atoroke. Basi siku hiyo ilifata yule mgeni wa siri wa Kamaralzamani akavaa mavazi ya walinzi ili asijulikane. Kamaralzamani akaenda kumuomba ruhusa baba yake ili aende kuwinda. Mfalme alifurahi sana kuona sasa akili ya mwanae imekaa sawa. Basi msafara mkubwa ukaandaliwa wa kwenda kuwinda.


Walipofika mawindoni Kamaralzamani na mgeni wake walitoroka na kukimbia. Walipofia njia panda wakachukuwa kisu na kumchinja sungura waliyemchukuwa nyumbani. Nguo za kamaralzamani wakazijaza damu ili ijulikane amejeruhiwa na kupotelea msituni. Wawili hawa waliendelea na safari yao msituni huku wanalala. Walihofia kupitia njiani kuwa huwenda wakaonekana na watu. Mwishowe wakafika bandarini. Kamaralzamani alibadili mavazi yake na kuwa ya kawaida. Ili sijulikane akaziba na sura yake. Walipanda kwenye marekebu ya kuelekea nchi za mashariki ya kati.


Baada ya mwendo wa mwezi mmoja hatimaye wakatokea kwenye nchi ya wakina binti sulatani. Katika hali kama ile ya kuziba sura Kamaralzamani aliweza kuingia nchini kwa siri. Hali ya binti sultani ilikuwa bado mbaya na waganha walikuwa wakiongezeka kila siku. Hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kumtibu ukiachilia mbali donge ya kumuoa endapo mtu atafanikiwa kumtibu. Hii yote ni kwa sababu maradhi ya mapenzi hayatibiwi kwa dawa za mitishamba. Sasa ni wakati wa kuona tiba sahihi ya maradhi ya mapenzi. Mipango yote ikawa inapangwa kwa usiri kabisa. Sasa binabu akaenda kwa dada yake na kumpa habari za furaha kuwa muda si mrefu atapona.


Kamaralzamani katika mavari yake ya kiganga akiwa amejichora kigangaganga akawasili mbele ya sultani na kumueleza kuwa atatibu maradhi ya binti yake hata bila ya kumgusa. Basi sultani ilibiti akahudhurie tiba hiyo. Nje ya chumba alicho binti sultani zuri kubwa la rangi ya nyekundu pembeni, nyeusi katikati na madoa meupe yapo kati ya nyekundu na nyeusi. Chetezo kikubwa kikawekwa na ubani mweupe ukachomwa. Mganga akachukuwa pete yake kwa siri na kuiweka kwenye karatasi bila hata ya mtu yeyote kumuona. Akaweza na ubani mule kishaa akaanza kunogesha uwanja. Baada ya kumaliza mbwembwe zake akachukuwa ile karatasi na kuiandika maneno kadhaa na kuivingirisha vyema na kumwambia mmoja ya wajakazi akampe binti Sultani.


Alipoifunguwa ile karatasi binti Sultani moyo ulikaribia kupasuka kwa furaha. Watu wote waliwza kusikia kicheko chake, furaha yake ilienea kwenye bostani la maua. Sultani akasema kuwa sasa mtoto wangu amepona. Sultani ilibidi atimize ahadi yake. Baada ya kuangalia maendeleo ya binti ndani ya mwezi hapo Sultania kajiridhisha kupoana kwa mwanae na harusi kubwa ilifanya baada ya masiku kadhaa. Kamaralzamani mtoto wa pekee sasa amemuoa binti sultani mtoto wa pekee. Wawili hawa walifanana kwa uzuri wao kama vile ni mapacha. Hata hivyo historia za maisha yao pia zilifanana.


Ni miezi 5 sasa imepita toka kamaralzamani aondoke nchini kwake. Kule mfalme alijuwa mwanae kipenzi ndio amefariki tena. Lakini aliendelea kujipa moyo kwa sababu haiwezekani wakose hata kidole chake. Hali hii ilikuwa ikimpa matumaini kuwa kuna siku moja atakuja kumuona. Mawazo haya yalimfanya aanze kuumwa kwa kumuwaza mwanae wa pekee. Kadri siku zilivyokuwazikienda ndipo hali ya mfalme inazidi kuwa mbaya. Taarifa hizi ziliweza kumfikia Kamaralzamani kupitia binamu yao. Hivyo akaamuwa kuwa siku oja arudi nyumbani.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela3 Main: Burudani File: Download PDF Views 564

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰5 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

HADITHI YA NURDINI 05: Rafiki wa Kweli

Mungu ashukuriwe sana, hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya waziri Masoud kugundua siri nzito.

Soma Zaidi...
NURDINI ANARUDI KWAO NA BARUA YA MFALME WA BAGHADAD

Hadithi za Alif lela u lela kitabu cha tatu sehemu ya nane

Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 03: Nurdini na Mtumwa

Siku ya tano Nurdini alipata taarifa kutoka kwa watu wake yaani wafanyakazi wa chumba chake kuwa kuna binti mgeni ameletwa ila ametengewa sehemu yake maalumu.

Soma Zaidi...
Kamaralzaman arudi kwao

SAFARI YA KURUDI NYUMBANI Kamaralzamani siku hiyo akamfuata baba mkwe wake na kmueleza ukweli wa mambo na kuwa yeye si mganga.

Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 03: Mtumwa wa Gharama

Kama wasemavyo waliokula chumvi nyingi kuwa muomba mungu hachoki, basi waziri Faridi aliendelea kuomba Mungu hata siku moja akapata taarifa kuwa kuna watumwa wametokea nchi za Uajemi.

Soma Zaidi...
HADITHI YA NURDINI 04: Mtihani wa Nurdini

Mama aliendelea kugomba sana kisha akamfungia binti ndani na kuweka walinznwa kiume, kisha akawaambia โ€œharuhusiwi kuingia wala kutoka yeyote humu ndnai, hata mbwa Nurdiniโ€ neno mbwa lilimtoka tu mama Nurdini kisha akajilaumu kwa kumfana nisha ...

Soma Zaidi...
Ndoa ya utata ya Kamaralzaman

NDOA YA UTATA KISIWANI Mfalmee wa serendib alipouona msafara ule alivutiwa sana.

Soma Zaidi...