image

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI


JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI



Siku moja Aladini alipokwenda kuwinda yeye na wafanyakazi wa Mfalme nyuma alikuja yule mchawi aliyemtelekeza Aladini kule mapangoni. Ukweli ni kuwa mchawi aliyekutana na waziri mkuu kule nchi za Afrika alikuwa ni yule mchawi aliyekutana na Aladini na kujifanya ni Baba mdogo na Aladini. Mchawi yule alitambua fika kuwa Aladini hawezi kutembea na ule mshumaa kwa ni ni kitu cha thamani sana. Alikuja mchawi yule katika sura ya mfanya biashara na kujifanya anabadili vitu vya zamani kwa vipya. Alipokuja kwa Aladini akajifanya anabadili mishumaa ya zamani kwa mipya. Ukweli ni kuwa alikuwa na vipande vya mishumaa vilivyo vizuri.


Alikuwa na mishumaa yenye rangi ya samawadi iliyo ang’avu sana, mishumaa ya rangi nyeusi na myeupe. Pia alikuwa na mishumaa ya madoamadoa. Alinukia miski mishumaa hiyo kama vile udi uluotengenezwa Yemeni. Mchawi huyu alipofika kwa Aladini akanadi sana na kuwasha mishumaa ile na kueneaharufu nzuri ya mishumaa. Hapo akasema kama ndani kuna vitu vya zamani ama mishumaa ya zamani isiyotumika mimi nabadilisha na mipya. Pale binti Mfalme kwa kuwa alishalewa na harufu ya mshumaa wa rangi wa mchawi. Mshumaa ambao haukuwaka moto ila yalikuwa ni mazingaombe. Kilevi hiki kilmfanya binti sultani kuingia nda wenda tafuta mhumaa.


Hatmaye akaja na kipande cha mshumaa wa ajabu. Mshumaa wa Aladini alioupata mapangoni. Yule mchaw alipoushika tu mshumaa ule kiza kinene kilitokea pale na ndani ya sekunde chache hapakuwa na chochote kile. Ilikuwa ni kana kwamba hapakuwa na kitu toka mwanza. Mchawi hauweza kuacha alama yeyote ile. Mfalme akiwa ikulu alkuwa akchungulia kwa dirishani jumba la Aladini. Lakini leo alishangaa hakuweza kuoa chochote. Muda huo huo mfalme hakuamn kumuna wzir wake. Mfalme alisalimiana na waziri kwa furaha. Lakini waziri kwa kuwa alijuwa kila kitu akaanza kumkandia Aladini kuwa ni mchawi sana na kumzulia mengineyo.


Mfalme akaagiza Aladini aletwe sasa hivi. Aladini alishangaa kundi la askari kumtia mbaroni na kumpekeka kwa Mfalme. “nieleze mwanangu yupo wapi, umemfanya nini na ipo wapi nyumba yako”yalikuwa ni maswali ya haraka ya mfalme. Aladini alishindwa kujibu maswali yote alioangalia hakuweza kuona jumba lake. Kwa hasira mfalme akaagiza kichwa cha Aladini kikatwe. Hapo aladini akamuomba msamaha Mfalme na kumuomba angalai siku tatu aweze kumrudisha mkewe. Na kama akishindwa akatwe kichwa. Mfalme akakubali kmpa Aladini siku saba.


Aladini alifika kwake na kuanza kulia sana. Kulia hakuku saidia akaenda kwa mama yake na kumueleza kila kkitu. Kisha aladini akamuita jini wa kwenye pete yake na kumuuliza kama anaweza kurudisha nyumb na mke. Jini wa pete kaeleza kuwa hawezi kurudisha chochote kilichofanywa na jini wa mshumaa. Hivyo Aladini akamtaka jini wa pete ampeleke mahali nyumba yake ilipo. Punde aladini akawa yupo dirishani kwenye nyumba yake huko maeneo ya Afrika. Masiini mke wake alikuwa akilia. Alladini alipojiridhisha kuwa yule mchawi hayupo ndani akamuita mkewe na kuzungumza naye.


Ladini akampatia mkewe maelekezo juu ya nini afanya na pia akamueleza vyocyote kuwa kuna mshumaa ulimpatia. Mwanamke akakiri ni kweli. Hapo aladini akamueleza mkewe siri nzima ya mshumaa. Lengo hasa la mchawi ilikuwa ni kumuuwa Aladinni na amchukuwe binti mfalme kuwa wake. Mchawi alikuwa akimsisitizia binti mfalme kuwa Aladini ameshakufa hivyo hana bidi kumkubali yeye.


Siku hiyo binti mfalme akaoga na kujipamba vizruri. Kisha akaweza glasi mbili za vinywaji huku akimsubiri mchawi aje. Mchawi alipokuwa alistaajabishwa na urembo wa mtoto. Mtoto akamkumbatia mchawi na kumwambia “nimekata shauri kuwa aaladini amekufa, hivyo nipo kwa ajili yako sasa, naomba tufurahie leo”. mchawi aliruka kwa furaha. Hapo binti mfalme akafukuwa bilauri ya kinywaji na kumpatia mchawi kisha wakaanza kunyweshana. Haukupita muda mchawi kakakata roho. Kumbe kinywaji kile kilikuwa na sumu.


Aladini alipojiridhisha kifo cha mchawi akachukuwa mshumaa, kisha akamzika mchawi. Aladini kwa kutumia jini wa mshumaa haikuchukuwa muda jumba la Aladini likarudi pale lilipo. Mfalme alifurahi sana na kwenda kumsalimia mwanaye na kumpa pole aladini. Aladini akamueleza mfalme kila kitu kuhusu mshumaa na pete. Basi maisha yakaendelea vizuri hatimaye miezi kadhaa ikapita bila ya tukio lolote.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 340


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Siri ya wageni wale
SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

Jaribio la pili la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa kwanza wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

BINTI MZURI ASIYETAMBULIKA
BINTI HUYU NI NANI? Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kwanini vidole gumba vilikatwa
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

HADITHI YA MLEVI
Soma Zaidi...