image

Kifo cha mtoa burudani wa sultani

Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan

KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN.

Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Kijana huyu alizoeleka sana na mfalme kiasi kwamba mfalme hakuwea kumkosa hata kwa siku moja. Siku moja kijana huyu akiwa kwenye dimbwi kubwa la mawazo alitembea maeneo kadhaa katika mji huu na akakutana na Mshona nguo. Alikaa sana kwenye eneo hili nje ya ofisi ya mshona nguo.

 

Muda wa kufunga ofisi ulipofika mshonanguo alimchukuwa kijana huyu na kwenda naye nyumbani kwa lengo la kufurahi nae na kula chakula. Alipofika nyumbani mkewake alimpokea kwa ukarimu kijana huya. Na kwa ufundi na uwezo wa kutoa burudani alio nao kijana huyu aliweza kuchangamsha nyumba hii. Mke wa mshonaji alianza kuandaa chakula kizuri sana na nyama ya samaki. Aliandaa ndizi na vyakula vizurivizuri kwa ajili ya mgeni wao.

 

Huku burudani zikiendelea mke wa mshonaji aliendelea kupika. Mshonaji alikwenda kuchukuwa vinywaji kadhaa na kuvileta pale nyumbani kwao. Muda wa chakula ulipofika walikusanyika na kuanza kula. Katika kufanya manyonjo na furaha mke wa mshonaji akachukuwa nofu la nyama na kuliiweka kwenye mdomo wa kijana yule na kumwambia meza. Kijana alimeza na kwa bahati mbaya kwenye nofu lile kulikuwa na mwiba mkubwa sana. Mwiba ule ukamkaba kijana yule na kupoteza maifahamu.

 

Mshonaji baada ya kuangalia hali ile akagunduwa kuwa kijana amekufa. Kuona hivyo akaogopa sana maana ataambiwa amemuuwa kijana wa watu. Wakashauriana na mkewake nini wafanye. Baada ya muda wakaamuwa kumchukuwa marehemu waendenae kwa tabibu ili wamuachie msala wote tabibu. Hali ikawa hivyo na wakambeba hadi mlangoni kwa tabibu kisha wakamlaza pale.

 

Waligonga hodi akatoka kijana wakamueleza amuite abibu harakwa kuna mgonjwa ana hali mbaya. Alipoingia ndani yule mtto kwenda muita tabibu mshonaji na mkewe wakakimbia. Tabibu alitoka na kiza cha usiku ule na akamkanyaga huyo aloambiwa mgonjwa. Ikawa tabibu akafikiri yeye ndo alomuuwa mgonjwa. Akanza kushauriana na familia yake wajue namna ya kujinusuru na janga lile. Mke wake akamshauri mumewe kwa kumwambia kuwa wamueke kwenye ukuta wa jirani yao.

 

Jirani yao alikuwa ni muuza nyama hivyo kulikuwa na wezi wanakuja kuiba nyamma pale kwake. Hivyo walifikiria huenda akampiga na kujuwa amemuuwa yeye. Basi wakamfunga kamba karehemu yule na kumpenyeza kwa nje ya nyumba yao kupitia paani. Aliposimama sawa kwenye ukuta wa jirani yao kwa nyuma wakaitowa kamba ile. Ilipofika usiku sana yule muuza nyama alirudi nyumbani na alipoona mtu kasimama kwenye ukuta wake akajuwa ni mwizi amekuja. Hivyo akachukuwa fimbo kubwa na kuanza kumtandika sawasawa. Hatimaye mtu yule alianguka na alipomgusa akahisi ameshakufa.

 

Kwa woga akafikkiria kuwa ameuwa mtu. Akaanza kushauriana na familia yake namna ya kujinusuru na mkasa huu.wakaamuwa wambebe maiti yule kisha wakamsimamishe kwenye moja ya kuta za sokoni, huenda akakumbana na walinzi wakampiga na hapo itakuwa ameuliwa mwizi na esi itaishia hapo. Wakafanya hivyo na baada ya muda mmoja katika walevi akapita eneo lile na alipoona mtu kajibanza akajuwa ni wale watu wanaomnyemelea siku zote na kumuibia pindi akilewa.

 

Mlevi yule alinyata pale karibu na kumpiga chupa ya mgongoni mtu yule. Hatiumaye kwa pigo moja la mlevi mtu yule akaangunga na m;evi kuangalia vile akajuwa kuwa ameuwa. Palepale walinzi walifika na kumkamata mlevi yule kwa kosa la kuuwa mtu. Basi kesi ile ikapelekwa kwa kadhi ili hukumu itolewe, na hukumu ikapita kuwa mlevi ni muuwaji hivyo naye auliwe. Mlevia akapelekwa katika uwanja wa mauaji na kuwekwa tayari kuuliwa.

 

Wakati hukumu inataka kupitishwa ghafla akatokea yule muuza nyama na kusema “ewe ndugu hakimu tafadhali niuwe mimi kwani ndiye nilomuuwa huyo kijana na si huyo mlevi” basi pale pale akaondolewa mlevi na muuza nyama akatiwa kitanzi tayari kwa kuchinjwa. Kabla hajachinjwa akatokea tabitu na kusema yeye ndiye muuwaji hivyo achinjwe yeye. Na alipotaka kuchinjwa tabibu alikuja mshona charahani na kusema yeye ndiye muuwaji halisi na wote hawa hawahusiki. Kitanzi kilipokuwa kwa mshona charahani. Kabla ya kufanya zoezi hakimu akaanza kushauriana na wenzie nini wafanye maana muuwaji halisi hawamjui.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1344


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU
Soma Zaidi...

UPENDO ULIOTAFASIRIWA KWA MICHORO
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa sita wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndani ya jumba la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Upendo uliotafsiriwa kwa michoro
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ujio wa wageni wa baraka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi mwenyewe
Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaa wa tatu
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...