UGENI WA DHATI

UGENI WA DHATI


UGENI WA DHATI



Baada ya mazungumzo kukamilika mama Aladini alikwenda nyumbani akiwa na furaha sana. Aliwaza kuwa anakaribia kuwa mkwe na Mfalme. Kwa upande mwingine mfalme alifurahi sana maana aliona sasa anakwenda kumkomoa aladini na kupata nafasi ya kumuoa mama Aladini. Aliamini kuwa aladini hataweza kulipa mahari hiyo. Waziri naye alifaurahi kwa sababu mfalme alifanya kama alivyomshauri. Waziri aliamini naasi nyungine kwa mwanaye inakuja kwani Aladini katu hataweza kulipa mahari kubwa kiasi kile. Binti mfalme pekee ndiye aliyekuwa na huzuni. Binti mfalme alitambua hata kwa ushawi gani Aaladini hatoweza kulipa mahari kubwa kiasi kile.


Mama alimkuta aladini akiwa anaotea moto baada ya kuoga maji yabaridi. Mama akahitaji kikombe cha maji ili alainishe koo lake tayari kumpatia habari za furaha mtoto wake kipenzi. Hali hii ilikuwa sawa pia kwa Mfalme ambaye aliomba maji kwa binti yake ili ampe habari za furaha za kukubali posa, huku akiwaza pia kuwa atampatia mama wa kambo mama aladini endapo Aladini mambo yatamshinda. Kwa upandewake mama Aladini alipopata funda la maji aliketi kwenye kiti cha miguu mitatu na kumuangalia mwanaye kipenzi kwa ukaribu kabisa huku akimthaminisha na kuwaza kuwa huyu ndiye mkwe wa mfalme. Mama aliendelea kumthaminsha mwanaye kama anafaha kweli mumchukuwa mtoto wa mfalme.


Baada ya muda mchache mama alitabasamu, tabasamu lilomuacha Aladini kubakia na mshangao. Kijana Aladini umri wa miaka 27 ambaye sasa masharubu ndio kwanza yanaanza kuota kama mbegu ya mpunga. Aladini hakutaka kumuacha mama atabasamu peke yake naye akafatiza kwa tabasamu la kijanja, tabasamu kafu lilojawa na udadisi. Mama alimuangalia tenda kijana wake alipokuwa akitabasamu, loo! Sura ya mfalme ikamjia mbele ya mtoto wake. Mama alifananiza visharubu vidogo vya mwanaye na yale ya mfalme. Mama akachukuwa sekunde kadhaa kumkumbuka mume wake marehemu kisha akajisemea 'wote hawamfikii mume wangu'. mama alipiga funda lingine la maji na kumuita mwanaye kwa jina.


'mwanangu aladini, pokea habari za furaha, kwa hakika mfalme amekubali posa yake' Aladini alicheka na kurukaruka kwa furaha. Siku hiyo aladini aliitumia kula, kunywa na kufurahi na mama yake. Hata kale kaduka kao kadogo ka kuuza vijiguo hawakukafunguwa. Kisha ilipofika jioni mama ikabidi amueleze mwanaye kuhusu mahari aliyotakiwa ailipe. Mwanangu mfalme amekuridhia kwa mahari inayolingana na hadhi ya mtoto wake, nayo ni mabeseni 10 ya dhahabu safi, mabeseni 10 ya lulu, mabeseni 10 ya madini ya almasi. Mapambo ya wanawake yaliyotengenezwa kwa dhahabu, almasi, shaba na fedha kila moja mabeseni 10. majora 20 ya hariri safi laini, na viatu vizuri vya ngozi ya kifaru pea 30. pia ametaka wajakazi 100 wa kiume na 200 wa kike, na wote waje wakiwa na beseni la dhahabu kila mmoja. Mama akaongeza kwa kusema kuwa mahari hii imetakiwa kutolewa ndani ya wiki 2'.


Aladini hakuonekana kuwa na mshangao hata kidogo. Aladini aliamini mshumaa wa ajabu utafanya haya yoye ndani yakauli moja tu. Ilipofika alfajiri aladini kama kawaida alisugua mshumaa, na jini lilipotokea akaliambia kila kitu, jini likaahidi kutekeleza ifikapo asubuhi. Basi mambo yakawa kama ivyo asubuhi ilipoingia aladini aliona msitari wa wajakazi 50 wakiwa na mabeseni ya dhahabu, mbele yao kuna mikokoteni 5 ya kuburuza na ngamia, yote imejawa na mizigo ya mahari. Aladini alimpa mama maelekezo na safari ya mama kupeleka mahari ikaanza. Falme alishangaa sana kuona mahari imepatikana na mapema hivi, tena kwa ubora zaidi ya alivyotamka. Mfalme moyo ulikufa ganzi kuona sasa hataweza tena kumpata mama Aladini.


Habari hizi za furaha zilimfikia binti mfalme ambaye hakuweza kuhimili furaha yake, alitoka mbia na kwenda kumkumbatia mkwe wake mtarajiwa, binti hakuishia habo alimbusu paji la uso la mkwewe na kumpeleka kwenye chumba kingine. Binti mfame aliamuwa kufunguw moyo wake kwa mkwe waeke. Binti akaagiza wajakazi wake wampeleke bafuni na wamsugue vyema na kwa upendo wa hali yajuu. Hali ilikuwa hivyo maji safi yaliyochanganywa na miski iliyonukia vyema. Mauwa na mjasmini yalichanganywa kwenye maji hayo yalio na uvuguvugu. Maji yalipendeza vyema kwa muogaji na hata muogeshaji. Haya hakuwahi kuyawaza mama aladini kama kuna siku yatatokea.


Visugulio vya hariri vinavyokwaruza kwa mbali kama vinatekenya. Mama aladini hakuweza kuumilia furaha yake hata kidogo. Muda wote alikuwa akitabasabu na kuchek. Wajakazi waliendelea mumsuguwa mama vilivyo, kisha wakampeleka chumba kingine. Chumba chenye mapazia ya rangi ya kijivu yaliyoandikwa maandishi ya kiarabu, maandishi yaliyoonekana kama ni maua mazuri. Mikunyo ya herufi na mfangilio utadhani yameandikwa na mchoraji. Maneno yalisomeka 'mrahaban bikum' yaani 'karibu'. katikati ya chumba kikubwa kulikuwa na kitanda kikybwa kilichokuwa na mito mitatu yote ni ya rangi ya kivivu yaliyochorwa picha ya kichwa cha ndege. (huyu ni ndege aliyewakutanisha Aladini na binti mfalme).


Kitanda kilikuwa na shuka kubwa la rangi ya buluu iliyochanganyika na hudhurungi, shuka ilioonekana kuwa na michirizi ya vijivu katika mapindo yake. Katikati ya shuka kulikuwa na picha ya ndege mzuri sana aliyetaka kufanana na tausi, ila ni mdogo. Mwenye rangi za mchanganyiko zilizopangiliwa vyema. Ndege huyu alionekana amechanua mabawa yake. Kichwa cha ndege kinafanana na picha ya kwenye mito. (ndege huyu ni yule ambaye aliwaunganisha wapendanao hawa). mama Aladini alibakiwa kuduwaa katikati ya chumba akishangaa uzuri ulioje wa chumba kile. Alizidi kuangalia juu yake, taa kubwa ya karabai ilikuwa imening'inia, ilikuwa imezungushiwa kwa waya maalumu ulioonekana kung'aa sana. Mama alijiwaza uzuri wa mwanga wa taa hii ifikapo usiku.


Viatu vya kike vya ngozi iliyoonekana kuwa ni madhubuti vilipangiliwa vyema kwenye kameza kadogo. Mama Aladini aliendelea kuangalia vyema kile chumba akagunduwa kuwa kuna midolo mitatu. Mmoja ni wa kiume na miwili ni ya kike. Midoli yote ya kike ilivalishwa nguo za kupendeza sana. Mama alistaajabu alipouona ule mdoli wa kiume Loo! Ulikuwa na sura ya mwanae kipenzi Aladini. Mama hakuelewa kabisa maana ya yote anayoyaona kwenye chumba hiki. Uzuri wa chumba ulimfurahisha sana lakini alistaajabu sana kwa aliyoyaona. Sakafu ya chumba hiki ilikuwa ni kama kioo, aliweza kujiona vyema kwenye sakafu. Mama Aladini hakufikiri kuwa ip siku ataingia sehemu kama hii, 'kweli kuzaa raha, lakini kupendwa ni raha zaidi' ni maneno aliyojisemea mama Aladini kwa sauti.


Baada ya punde binti mfalme akaja akiwa na nguo nzuri zilizofumwa na fundi maridadi wa ikulu. Gauni refu lililoburuzika chini, likiwa na rangi zilizofanana na mkia wa tausi. Gauni lilikuwa ni la kupendeza sana, mama akajikuta kama ndio binti wa makamo. Mama alimuwaza sana marehemu mume waka laiti kama angelimuona ama angeliiona siku kama ya leo. Wasusi mahodari wa warembaji waliletwa na kutengeneza mwili wa mama Aladini. Mama alijiwazia na kuamini kuwa kweli ana mtoto wa iume. Kweli nguvu ya mapenzi haiwezi kufaannishwa na kitu. Baada ya maandalizi yote kukamilika binti mfalme alianza kumpa mama stori nzima ya aladini na yeye kumueleza maana za kila kilihopo ndani.




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 183


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME. Soma Zaidi...

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 08
20. Soma Zaidi...

KIFO CHA AJABU
Download kitabu Hiki Bofya hapa KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SULTAN. Soma Zaidi...

SAFARI YA PILI YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA PILI YA SINBAD Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Kiapo Cha Mfalme
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

DARSA ZA DINI YA KIISLAMU KAMA QURAN, FIQH, SIRA, AFYA, TAJWID NA TAFSIR ZA QURAN
Soma Zaidi...

IDGHAAM KATIKA LAAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Hadithi za Sinbad
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI YA TABIBU NA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Soma Zaidi...

Kuangamizwa Firauni na Majeshi Yake
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 24
13. Soma Zaidi...