Navigation Menu



image

Historia ya pango, aladini na kitabu

HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU

Aladini alipofika kwake alikuwa na mawazo sana, maana ilibakia kidogo aingie majaribuni. Aladini sasa alikuwa na mawazo kuwa muda wowote asipokuwa makini anaweza kupoteza kila kitu. Kwa mawazo yote aliamua akalale. Katu usingizi hakuweza kupata hata lepe la usingizi. Aladini akiwa kwenye fikra na mawazo haya ghafla aliwaza kile kitabu. Aladini alifikiri hasa ni nini chanzo cha lile pango na ni kitu gani kimeandikwa kwenye pango lile. Aladini akapatwa na hamu kubwa ya kusoma, ijapokuwa Aladini hakukulia katika mazingira ya kupenda kusoma. Aladini alifikiri ili aweze kuelewa vyema akaoge. Pia huenda alikwenda kuoga kwa sababu Aladini aliamini kuwa kitabu kile kitakuwa ni kitabu kitukufu hivyo si vyema kukigusa bila hata kuoge.

 

Baada ya kumaliza usafi wa mwili Aladini akakamata kitabu akiwa yupo kitandani kwake. Hata mkewake alishangazwa sana na tabia ya mumewe leo kusoma. Kwa hakupatapo kumuona akisoma hata. Gamba a juu la kitabu lilikuwa ni la ngozi iliyokunnwa vyema. Gamba la juu lilikuwa ni chakavu na halikuweza kuonyesha chochote katika picha wala maandisi. Lakini mshangao mkubwa ni pale Aladini alipofunua ukurasa wa kwanza wa kitabu ambapo alikuta picha ya pete aliyovaa, mshumaa wa ajabu, yule ndege wa ajabu, vile vijiwe vya pangoni, vile vijiko pamoja na kit kama yai. Lakini kitu hiki kumeandiwa juu na nyuki kadhaa wa dhahabu. Picha hizi hazikuwa na majina. Hapa Aladini akaanza kupatwa na mshangao na kuanza kufikiri kuwa huwenda mambo yote aliyokutana naye yalishatabiriwa kwenye kitabu hiki.

 

Aladini alizidiwa na ushawishi na madukuduku. Aladini hakuridhishwa na zile picha alitaka sasa kuona nini maana ya picha zile. Ndipo akafunguwa ukurasa unaofata. Loo! Aladini alistaajabu zaidi kuona kuna mchoro wa sura yake, mkewe, baba yake na pia kulikuwa na sura mbili za watu ambazo ni ngeni sana kwa Aladini. Watu hawa alikuwa ni babau yake na mchawi wa pili. Aladini alianza sasa kuamini kuwa kitabu kile kuna familia yake, hivyo kuna uwezekana wa uhusikaji wake katika pango lile. Chini ya ukurasa huu kulikuwa na maandishi ya lugha asiyoijuwa. Lakini maandishi hayo yalifanana sana na maandishi ya majini.

 

Ukurasa uliofuata ulikuwa na rangi nyeusi tupu na maandishi ya rangi nyeusi yaliyoweza kuonekana kwa mbali sana, kama vile jongoo kwenye usiku wa kiza. Maandishi yaliweza kusomeka kwa mbali sana. Aladini akabaki kukodoa mimacho tuu. Baada ya kutazama kwa muda mrefu maandishi yale yakaanza kubadilika taratiibu kuwa meupe na kuanza kusomeka vyema. Mambo haya yalimshangaza sana Aladini. Muda wote Aladini alikuwa akisoma kitabu akiwa amelala kichalichali. Basi akajigeuza upande wa kulia. Wakati anajigeuza kwa bahati mbaya alikifunga kitabu. Alipokuja kukifungua kila alichokisoma na kukiona kwenye kitabu kile hakikuweza kuonekana tena. Zilibaki kurasa tupu. Dah aladini alistaajabu sana, na alitambuwa kuwa hakuna kinachobakia kwenye kitabu hiki baada ya kukisoma.

 

Kwa kuwa Aladini hakuweza kusoma yale maandishi yaliyokuwa yakisomeka baada ya kukodoa macho kwa muda maandishi yakaanza kurudi tena. Maandishi hayakuwa mengi sana ila yalisomeka kama ifuatavyo

 

“Salamu nyingi zikufikie mchaguliwa wetu ewe Aladini, bila shaka ndiwe unayesoma hiki kitabu kwa sasa. Kwani asingeweza yeyote kusoma ila wewe. Siri nzito ya familia yako na pango ili inapatikana humu. Tumekilinda kitabu hiki kwa miaka zaidi ya 85 sasa, na baada yako hakuna atayeweza kuisoma katu, kwani maandishi tutakuwa tumeshayachukuwa. Kumbuka siri za kwenye kitabu hiki hutamueleza yeyote. Tambua pia kuwa kurasa zijazo utatakiwa kufumba macho ndio uweze kusoma kitabu hiki. Hakikisha upo peke yako katika sehemu tulivu, mwisho ninakutakia mafanikio mema na binti mfalme”

 

Aladini sasa maswali mengi yakazidi kuzunguka kichwani mwake hasa pale alipotakiwa mafanikio mema yeye na binti Mfalme. Inamaana maisha ya Aladini yalishaandikw akuwa atamuoa binti Mfalme. Aladini alijaribu kufungua kurasa zijazo lakini hakuona maandishi. Alijaribu kukodoa macho kwa muda mrefu lakini wapi. Aladini sasa akawaza kuwa njia pekee ya kuendelea kusoma kitabu kile ni kufumba macho na kuwa katika sehemu nzuri na tulivu. Aladini akafikiri kuwa chumba cha stoo ambapo kulikuwa kukitoka mwangaza hajawahi kuingia, wala kuchunguza mwangaza ule ulitokea wapi. Aladini akawaza kule ndio sehemu pekee iliyo tulivu ambapo hatoweza kusumbuliwa katu.

 

Aladini akabeba kitabu chake na kuelekea kwenye chumba kile. Loo! Harufu nzuri ya marashi yaliyonukia vyema ilimkaribisha. Aladini alistaajabishwa kuona kuwa chumba kile kina vijiwe vinavyotoa mwangaza kama vya kule pangoni. Vijiwe vilikuwa kwenye kaboksi kadogo ka vioo. Chini ya kiboksi kulikuwa na karatasi iliyoandika “zawadi kwako Aladini mjukuu wangu”. Aladini alikuta kwenye chumba kile kuna kiti kikubwa kizuri sana. Kiti kilichofanana na cha mfalme ila tu hiki kilikuwa kinauwezo wa kukilaza na kuwa kile kiti cha uvivu. Aladini alikaa pale na kujiandaa tayari kwa kusoma ujumbe wa siri kwenye kitabu cha maajabu.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1164


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya mjakazi wa Mfalme
HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Soma Zaidi...

NDANI YA JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Mtihani penzini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Nje ya jumba la kifahari la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndoa ya siri
NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

Sababu ya kukatwa vidole gumba
KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA? Soma Zaidi...