Aladini na binti wa mfalme


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya mshumaa wa ajabu


ALADINI NA BINTI WA MFALME.

Baada ya pango kuziba Aladini alianza kupata taabu sana. Wale nyuki walikuwa wakimuuma, kale kamwanga kadogo ka pete hakakuonekana tena. Ukweli ni kuwa yule mzee alikuwa ni mchawi aliyesoma kuhusu uajiri wa eneo hili, alitambuwa kuwa ukipata mshumaa tu utakuwa na nguvu ya ajabu sana. Hakuna mchawi wala mganga atakayekutia mkono. Kulingana na maelezo ya hiko kitabu huwezi kuuchukuwa huo mshumaa mwenyewe, lazima upokee kutoka kwa mtu mwingine vinginevyo ni kifo. Pia atakayeuchukuwa hatakiwi kutoka humo ni lazima afie humo, vinginevyo ni kifo. Hatahivyo atakayeuchukuwa anatakiwa awe ni kijana wa kiume asiyemjuwa mwanamko hata (yaani hajawahi ku ……) hivyo ndio maana Aladini alikuwa ni chaguo pekee.

 

Sasa mzee mchawi alivyoona Aladini hataki kumpa mshumaa alijuwa kuwa vinginevyo ni kifo chake. Alichofanya ni kuziba shimo ili Aladini afe kabisa iiwe ni kafara yeke. Ila jambo la hatari ni kuwa mchawi alisahau kuchukuwa pete yake kwa Aladini. Na hiki ndio kitu pekee sasa kinachoweza kumtoa Aladini. Ndani ya pango Aladini aliendelea kulia sana. Aladini alijuta na akatamani kula lakini hakuna cha kukila. Nyuki kadhaa waliweza kumuuma na kumuongezea maumivu badala ya njaa aliyo nayo. Siku ya kwanza ilipita ola bila Aladini kuliona jua wa la kula kitu, siku ya pili nayo ikabita. Aladini sasa amechoka sana, kiu na njaa vinamsumbuwa, kiza na joto yote yanampa taabu.

 

Aladini aliendelea kuomba dua kwa Mungu mlezi na aliendelea kutubu. Aladini alitambuwa madhambi yake yote na kuahidi kutokurudia endapo Mungu atamtoa salama kwenye pango lile la kifo. Machozi ya aladini yaliweza kutotesha mavazi yake kwa siku ya kwanza, lakini sas aAladini hakuweza tena kulia kwa machozi. Maana hana maji ya kutosha kuzalisha machozi mwilini. Hakika Aladini yupo katika hali ngumu sana. Kwa upande mwingine mama aliamini kuwa Aladni yupo hatiani, na hii ni baada ya kukumbuka kuwa shemeji yake aliambiwa kuwa na kovu kubwa la jeraha kwenye paji la uso wake. Lakini shemeji huyu hana hilo kovu.

 

Mama aligundua kuwa mwanae yupo hatariri. Mama aliendelea kuomba dua na kumtafuta mwanaye kila alipojuwa. Kwa upande wa mchawi baada ya kuondoka pale alipotea kabisa, alipokumbuka kuwa pete ya ajabu hana, alishindwa kurudi. Kwa mujibu wa kitabu alichosoma ni kuwa alitakiwa kurudi pale baada ya kiaka 3, kila jaribio likifeli anatakiwa angoje miaka mitatu. Na tayari hili sasa ni jaribio la 5. na kila alipofeli kijana alipoteza maisha, na saa ni zamu ya Aladini. Habari ya Aladini ni tofauti kidogo na wenziwe, maana wenziwewaligoma kutoa mshumaa lakini walirudisha pete baada ya kulaghaiwa. Lakini Aladini alibakiwa na pete ya mchawi.

Katika kiza cha pango Aladini hakutambuwa muda, kuwa ni asubuhi ama jioni. Wakati alipokuwa akiomba dua alikuwa akisuguwasugwa ile pete, ghafla lijini kubwa likatokea. Pango zima likawa na mwangaza. Lijini likasea kuwa “mimi ndiye mtumwa wa hiyo pete, nambie unataka nini nikusaidie” Aladini kwa ujasiri akatamka kuwa “nitoe hapa kwenye pango” punde Aladini akajikuta yupo nje. Alikimbia sana na alipofika nyumbani ilikuwa ni majira ya asubuhi. Aladini alipofika mlangoni kwao Aliangka na kupoteza fahamu. Ama yake akampepea na kumpahuduma ya kwanza. Alipozinduka Aladini alihitaji kitu cha kula. Mama akamueleza “mwanangu hapa sina hata pesa, ila kuna nguo hizi niende sokoni nikauze tupate pes”

 

Aladini aliposikia kuwa ndani hakuna pesa ya kula alikumbuka kuwa mfukoni anamshumaa ule aliochukuwa kule pangoni. Aladini akamueleza mama yeke kuwa kuna mshumaa amekuja nao atakwenda kuuza wapate pesa. Aladini akauchukuwa ule mshumaa na kuanza kuusafisha na maji maana ni mchafu sana hivyo usingenunuliwa. Wakati anausuguwa ghafla harufu ya manukato ikazagaa ndani kwao Aladini, mwangaza hafifu ukatokea ukutani na binti membo akatokea kisha ananena “mimi ndiye mtumwa wa huo mshumaa, nitume chochote nitakutekelezea” Aladini bila woga akamueleza niletee chakula cha kula mimi na mama”

 

Punde masinia mawili ya dhahabu yaliyofunikwa wa makawa yenye rangi nzuri. Vishikizo vya juu vya makwa vilikuwa ni sanamu la huyu jini wa kike. Aladini alipofunua kila sinia lilikuwa na sahani moja, bilauri za dhahabu, birika moja na vikombe viwili. Kikombe kimoja kilikuwa na asali ya dhahabu, kikombe kingine kilkuwa na juisi ya matunda. Aladini hakujuwa ni matunda gani maana ilikuwa na mchanganyiko wa rangi utadhani mikia ya tausi wa uhabeshini.bilauri ya maji ilikuwa ni ya madini ya fedha. Visahani vidogo vya kuwekea vikombe vilikuwa ni vipande vya lulu vyenye rangi nzuuri. Haya yote yaliendelea kumsataajabisha Aladini. Aladini alistaajabu zaidi alipoona kijiko, kwani kilikuwa ni cheusi, jambo ambalo hakulitarajia.

 

Aladini aliposhika kijiko, kilianza kuangaza chumba kizima mwangaza huu ulimkumbusha ule wa kwenye lile pango. Aladini akaanza kukumbuka kila alichokiona kwenye lile pango. Na kila alipokumbuka vilikuwa vikionakena ukutani. Punde alipokichia kile kijiko mambo yalitulia. “mmmh” aliguna Aladini, mguno ambao ulimshitua mama aliyekuwa anajiandaa kwenda sokoni kuuza vingui alivyoshona wapate cha kukila. “una nini Aladini” ni swali la mama kwa mwanaye kipenzi. Mama alipotoka alikuta mambo yamebadilika, harufunzuri ya vyakula. Kufunua alikuta chakula kizuri, chakula ambacho huwa kinaliwa na wafalme na mawaziri.

 

Aladini aakamkaribisha mama na kumwambia asiulize zaidi ya kula maswali baadaye. Aladini alizungumza maneno hayu huku paja la kuku wa kuoka likiwa mdomoni. Kwa njaa alifundia na kunywa juisi na kulamilizia na asali. Alipomaliza alimsimulia mama kila kitu. Kisha aladini akachukuwa vitu vyote vile na kwenda kuviuza. Pesa laiyoipata aliweza kuitumia kwa muda wa miezi kadhaa.

 

Maisha ya Aladini yakarudi kawaida, na Aladini hakutaka kutumia nguvu zile kwa muda mrefu. Na aliamuwa kuishi kama alivyoishi zamani. Hakukuwa na mabadilio yeyote zaidi ya kuwa alikuwa ni mtiifu na mwenye kusaidia kazi mzazi wake. Aladini aliweza sasa kushona nguo kwa umaridadi mkubwa kama baba yake. Siku moja mfalme wa nchi alitangaza kuwa watu wote wasitoe ndani maana binti mfalme atapita mtaani kwenda bwawani kuoga. Ilikuwa ni kawaida yake kila miezi sita anakwenda kuoga bwawani. Hivyo siku hiyo hakuna anayeruhusiwa kutoka.

 

Aladini alitaka kujuwa sura ya binti mfalme. Alichofanya ni kwenda bwawani na kujificha juu ya mti. Baada ya muda binti mfalme akaja bwawani. Aladini alitaka kuziba sura akiamini kuwa binti mfalme amekuja kuoga hivyo atavua nguo. Ukweli ni kuwa binti mfalme hakuwa akioga ila ni kuchezea maji na wadogo zake na kuchezea mchanga mweupe wa bwawani. Aladini alishuhudia kila alichokiona, aladini alipendezwa ghafla na sura ya binti. Katika kucheza alikuja ndege mzuuri na kumtua binti kwenye kichwa chake. Binti alitabasamu na kufurahia, ndege yule alipuruka na kuelekea juu ya mtu ambapo Aaladini amejifucha. Macho ya Aladini yakakutana na binti, “mmmmh huyu kaka nzuri sana” ni maneno yaliyotoka moyoni mwa binti..



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Hadithi ya Khalid mwenye kuneemeshwa na Jalid
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)
Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani. Soma Zaidi...

image Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...

image Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti wa kwanza na mbwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi iliyosimuliwq na mlevi mbele ya sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi iliyosimuliwa na mlevi mbele ya sultan Soma Zaidi...

image Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Hadithi ya binti wa pili mwimba mashairi mwenye makovu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...