Hadithi ya Kaka wa sita wa kinyozi


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani


HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI

Kaka yangu wa sita amekatwa mdomo wa chini. Nitakusimulia kisa hiki kwa ufasaha na kwa ufupi. Habari ni kuwa kaka yangu wa sita hakuwa ni mtafutaji sana wa mali ila alikuwa ni mcheshi na mpenda utani sana. Alikuwa na hali ya kipato cha chini na ilitokeaga siku nyingine anakosa hata cha kukila. Kaka yangu wa sita naye ni kama wenzie hakuwa na mke wala mtoto na hakupatapo kuoa. Hakuwa na makazi ya kudumu kwamuda mrefu hivyo alizoea sana kutanga tanga. Jambo ambalo lilikuwa linampatia sifa kaka yangu huyu ni kuwa alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri. Alikuwa akipendwa sana na wabinti na hata wake za watu. Nadhani hali hii ndiyo iliyomfanya asiwe na makazi maalumu ili kuepuka mitihani na wake za watu na watoto za watu.

 

Ilitokea siku moja kaka hakupata kula toka asubuhi mpaka mwishoni mwa mchana. Katika hali hiyo hakupatapo kutia kitu mdomoni iwe kinywaji ama chakula. Katika hali kama hiyo kaka alidhoofu sana kwa ghafla ndani ya siku moja tu. Katika kutembea kaka akafika kwenye nyumba moja pembeni kidogo na mji. Kaka alikwenda kuomba walau apate hata tunda moja la kufunguwa kinywa chake. Alikuatana na mlinzi wa geti. Kaka akaeleza shida yake kwa mlinzo aliyeonekana mwenye busara sana na mwenye huruma. Mlinzi alimueleza kuwa aingie ndani na atakutana na mwenye nyumba.

 

Kaka akaingia ndani, huko akakutana na bostani kubwa na la kifahari. Matunda yaliyowiva yalikuwa yakining’inia kama taa za fanusi zilizotengenezwa Misri. Maembe machungwa na midizi iliyopangiliwa kwa mistari kwa pamoja ilipendeza vyema. Kaka njaa ndio ilizidi baada ya kuona minanasi iliyokatika sura njema. Kaka hakujuwa ni wapi atamuona mwenye nyumba. Aliendelea mbele huku akiona vitu vizuri na vya kupendeza. Hatimaye alianza kuona kiti kizuri chenye miguu ya kumeremeta. Mzee wa makamo alikuwa akisoma kitabu kikubwa sana. “Asalaamu Alykum” “waalykumsalaam habari yako kijana” “Nzuri tuu” yalikuwa ni salamu kati ya kaka na mzee wa makamo.

 

Baada ya salamu kaka akaeleza shida yake. Mzee alionekana kufurahi sana na alionyesha tabasamu la udadisi. Mzee akamchukuwa kaka hadi kwenye baraza ya nyumba na kukete wakiwa wanaangaliana. Mzee naye akasema kuwa hata yeye ana njaa sana. Alikuwa akisubiri mtu wa kukaa na kula naye, kwani yeye hakuzoea kula akiwa pekeyake hata siku moja. Kaka alifurahi na kuona kuwa nitakula na mwenye nyumba kubwa na ya kifahari. Bila shaka aliamini kuwa leo atakula vitu vya utamu sana.

 

Mzee akaagiza vijana wake walete viliwa. Mmoja akaleta birika la kunawia maji. Cha kushangaza birika lilikuwa tupu, na katika hali hiyo akafanya kama anamnawisha mzee na mzee akafanya kama ndio ananawa. Alipomaliza kunawa alifanya kama anakung’uta mikono. Ukweli ni kuwa hakuna alichonawa ila ilikuwa tu ni utani. Mzee huyu alizijuwa vyema sifa za kaka kuwa anapenda utani. Lakini leo kaka mpenda utani ana njaa sana. Na anafanyiwa utani kwenye chakula. Leo uvumilivu wa kaka unakwenda kupimwa. Baada ya kijakazi kumnawisha mzee alienda kwa kaka naye akafanya vile vile kama anamtirizia maji. Kaka naye akafanya kama mzee vile ananawa kisha akakung’uta mikono yake. Kijakazi akaondoka.

 

Kijakazi mwingine akaja, mzee akamwambia tuwekee nyama ya kuoka na mikate pamoja na mchuzi wa kuchovyea. Kijakazi akafanya kama anatenga. Alipomaliza akaondoka. Ukweli ni kuwa alitenga hewa tu. Mzee akamwambia kaka waanze kula. Mzee akajifanya kama anakata kipande cha nyama huku anaminyana kwa taabu. Akamwambia kaka akamate kipande kile wavutiane. Kaka akafanya kama anakamata kipande kisha kikakatika na wakaendelea kula. Hapa walikuwa hawalikiuhalisia ila kila kitu kilikuwa ni hisia tu. Kaka akagunduwa kuwa stiki za kuchokole meno hazipo. Hapo akajifanya kana kwamba nyama imemkwama kwenye meno yake.

 

Mzee akamuita kijakazi alete stiki, punde ikaletwa na kaka akaanza kuchokowa meno. Kisha akaendele akula kawaida. Nmzee alikuwa akionyesha tabasamu la udadisi muda wote. Kaka akajifanya anakula kwa pupa maana ana njaa sana. Haukupita muda kaka ndipo akapaliwa na kipande cha mkate. Mzee kwa shauku akamkamata kaka na kuktia ngumi mgongoni, ngumu iliyoingia vyema mgomgoni mwa kaka aliyekuwa ana njaa kali sana. Kaka alikasirika sana na alitamani amrudishie ila alivumilia. Kaka akasema kimoyoni huyu mzee nitamlipa masikhara yake leoleo hii na atajuta kufanya utani na mimi.

 

Mzee akajifanya ameshiba hivyo akaagiza vinywaji viletwe. Kaka alitaka aletewe mvinyo uliotemgenezwa kutoka nchi ya uhabeshi. Mzee akaagiza mvinjo wa tende na zabibu. Wote kwa pamoja waliagiza kwa sauti. Punde kijakazi akafanya kama anatenge bilauri na birika mbili akaweka mbele yao ili waweze kujitilia wenyewe. Ukweli ni kuwa kaka alikuwa na njaa sana lakini alijitahidi kuvumulia yote haya huku akitafuta nafasi ya kulipa huu utani. Nafasi aliyoitafuta kaka sasa ndipo imepatikana maana sasa ameanza kujifanya amelewa.

 

Katika hali kama hiyo mvinyo wa kihabeshi ulionekana mkali sana. Sasa kaka amelewa na ameanza kutapika. Akajifanya amemtapikia mzee. Na mzee akajifanya kama anafuta matapishi kwenye kanzu yake. Haukupita muda kaka akamtandika kofi kubwa mzee kwenye shingo. Akamuongeza tena kwenye uso, hadi mzee akaona nyotanyota. Mzee tabasamu likaondoka na akahamaki na kuuliza mbna unaniadhibu? Kaka alifurahi baada ya kuvunja utani wa mzee. Kaka ndipo akajifanya anaongea kwa kulewa, na kumwambia mzee “unataka lingine, wanasema kofi na mlevi zito, na kulewa huku niliko nako nataka nikuongeze lingine”. hapo mzee akacheka sana na kutamka “umeshinda kijana”.

 

Kumbe muda wote mzee alikuwa anamjaribu kaka na sasa kaka ameshinda majaribu. Mzee akajitambulisha vyema kwa kaka, na kaka akjitambulisha. Japo mzee alikuw akimfahamu kaka, maana mzee alikuwa ni rafiki na baba. Baada ya hapo mzee akaagiza chakula cha ukweli kiletwe, na hapo ilikuwa ni kula na kunywa kiukweli. Baada ya hapo mzee alimtaka kaka waishi pale kwa pamoja. Waliishi pamoja kwa muda wa miaka 20, kisha mzee akafariki. Ndugu za mzee wakazichukuwa mali zote na kaka wakamuhisabu kuwa ni mtumwa wa mzee na wakamuuza kwenye biashara za utumwa.

 

Kaka alinunuliwa na mzee mmoja hivi. Kwa kuwa kaka alikuwa na sura nzuri, mke wa mzee alikuwa akimtamani kaka. Siku moja walikutwa wakiwa wamekee kwa pamoja kwa ukaribu sana. Mzee alikasirika na kumkata kaka mdomo, akamtandika na kwenda kumtupa mbali maeneo ya milimani. Wapitanjia walimuokota kaka na kumtibu kumpatia mavazi na chakula. Nilipozipata habari hizi nilikwenda kumtafuta kaka na kumchukuwa.

 

Baada ya kumaliza masimulizi haya haya ya kaka sita pamoja na yeye mwenyewe mkinyozi akamueleza kadhi je umeamini kuwa mimi si mtu wa maneno mengi, bali nazungumza ukweli?. kadhi alifurahi sana na kuniruhusu niondoke pale. Kisha kinyozi akaendelea kusema kuwa katika pirika pirika ndipo nikakutana na baba wa huyu kijana wakati huo kijana huyu akiwa ni mdogo. Niliweza kuishi na baba wa huyu kijana kwa muda mrefu, na kabla ya kufariki alinitaka niendelee kumlinda kijana wake. Niliendelea kufanya hivi kwa siri kwa muda mrefu. Hivyo sikuwa nikimtakia maomvu huyu kijana kama yeye alivyofikiria.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    2 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Download App zetu hapa ujifunze zaidi    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Hasara za wivu na kutokuwa wazi (sehemu ya 3)
Posti hii inahusu zaidi hasara za kuwa na wivu na kutokuwa wazi, sehemu hii inahusu zaidi maendeleo ya Lisa shuleni yanakuwa mabaya zaidi na lina anaendelea kumtunzia siri lengo lake lina ni kuendelea kuwa wa kwanza darasani. Soma Zaidi...

image Ndani ya jumba la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)
Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani. Soma Zaidi...

image Safari ya tano ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 2
Post hii ni mwendelezo wa hadithi ambayo Kwa jina inaitwa wakati wa Kufumbuka, ni mwendelezo wa pale maria anawekwa mbele ya wazee Ili akili kwamba John sio mtoto wa Mzee maganga ila maria akikumbuka wazi kwamba John ni mtoto wa Mzee maganga anakataa kukiri na anaangua kilio na watoto pia wanaangua kilio na pia wanaamua kumpeleka Mari kwenye mizimu Ili iweze kuamua. Soma Zaidi...

image NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)
Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank Soma Zaidi...