picha

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat

"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat

1. Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat (49:15)


"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi." Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tuliyowapa. Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa". (8:2-4)


"Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kweli kweli." (49:15)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli ni wale wenye sifa zifuatazo:
(i)Wana yakini kuwa Allah (s.w) yupo
Waumini wa kweli huwa na yakini nyoyoni mwao juu ya kuwepo Allah (s.w) na Mtume wake. Yaani wanashuhudia kwa dhati nyoyoni mwao kuwa Allah (s.w) ni Mola wao pekee na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake wa mwisho na katika matendo yao yote huishi kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na daima hukumbuka msisitizo wa aya ifuatayo:



“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao. na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa)." (33:3 6)



(ii)Humcha Allah (s.w) kwa kutekeleza amri zake
Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa. Hufanya hivyo kwa kukhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu na kutarajia radhi zake.



(iii)Huongezeka Imani yao kwa Kusoma na kufuata Qur-an
Wanaposoma aya za Mwenyezi Mungu huwazidishia imani kwa maana nyingine, waumini wa kweli hufuata mwongozo wa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Hawako tayari kufanya jambo lolote kinyume na mwongozo wa Allah (s.w). Imani huongezeka kwa kutenda inavyostahiki kwa mujibu wa maelekezo ya Allah (s.w).



(iv)Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Wanamsimamo thabiti na hawayumbishwi na yeyote katika kutekeleza wajibu wao kwa Mola wao. Wanayakini kuwa aliyenusuriwa na Allah (s.w) hakuna wa kumdhuru na aliyeandikiwa kupata dhara na Allah (s.w) hakuna wa kumnusuru.


(v)Husimamisha Swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Huswali swala zote za faradhi na swala za Sunnah kwa kadiri ya uwezo wao kwa khushui (unyenyekevu) huku wakizingatia masharti na nguzo za swala. Na kwahiyo hufikia lengo la swala kwa kutojihusisha kabisa na mambo machafu na maovu. Pia husimama kidete kuondoa maovu na machafu yaliyopo katika jamii.



(vi)Husaidia wenye matatizo katika jamii
Huwa wepesi wa kutoa msaada wa hali na mali kwa wanaadamu wenzao wanaohitajia msaada. Pia hutoa mali zao na nguvu zao kwa ajili ya kuendeleza Uislamu na kuusimamisha katika jam ii.



(vii)Hupigania Dini ya Allah (s.w)
Wanafanya jitihada za makusudi kwa kutumia mali zao na kujitoa muhanga nafsi zao ili kuhakikisha kuwa dini ya Allah inasimama katika jamii. Yaani wanajitahidi kwa jitihada zao zote ili kuzitafanya sharia za Allah (s.w) ziwe ndizo zinazotawala harakati zote za maisha ya jamii. Lengo lao kuu la maisha ni kuutawalisha Uislamu katika jamii.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1472

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 ai web app    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Mtazamo wa uislamu juu ya dini

Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Soma Zaidi...
KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu

Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu

Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)

Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?

Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura

“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).

Soma Zaidi...
Mambo ya lazima kufanyiwa maiti ya muislamu

Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...