Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

(d)Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)


"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu ni kwangu, hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda." (31:15).



Aya inabainisha wazi kuwa hatupaswi kuwatii wazazi wetu pale watakapotuamrisha kumuasi Allah (s.w). Tukiwatii tutakuwa tumemshirikisha Allah (s.w) kwa kuwafanya wazazi wetu miungu badala yake kama inavyo bainika katika Qur'an.



โ€œMayahudi na Wakristo) wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allah (s.w) โ€ฆ." (9:31)



Iliposhushwa aya hii Adi bin Hatimu (r.a) ambaye alisilimu kutoka kwenye Ukristo, alimtaka Mtume (s.a.w) atoe ufafanuzi kwa sababu alidai kuwa kinadharia hawakuwa wanawafanya watawa wao miungu. Katika kufafanua, Mtume (s.a.w) alimuuliza Adi, "Je hawakuwa watawa wenu wanawahalalishia alivyo viharamisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii?" Alijibu Adi, "Ndiyo" Mtume (s.a.w) akamuuliza tena, "Je watawa wenu hawakuwa wanakuharamishieni alivyo halalisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii? Adi akajibu tena "Ndiyo." Basi Mtume (s.a.w) akasema, "Huko ndio kuwafanya miungu".



Hivyo, kumtii mzazi au kiongozi au yeyote yule katika kumuasi Allah (s.w) ni kumfanya mungu badala ya Allah (s.w). Pia ukitii matashi ya nafsi yako kinyume na amri au makatazo ya Allah (s.w) utakuwa umeifanya nafsi yako mungu badala ya Allah (s.w).


"Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake, (kile anachikipenda), kuwa Mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi na hayo, na hali ya kuwa hataki?). "(25:43).



Lakini, tunaamrishwa katika aya hii (31:15) kuwa pamoja na kutowatii wazazi wetu katika kumshirikisha Allah (s.w), tusiwe jeuri na fedhuli kwao, bali tuzungumze nao kwa upole kwa kauli njema na tuendelee kuwatii na kuwafanyia wema katika mambo yote ya halali.


Wakati mwingine wazazi wanaweza kutishia kuacha laana tutakapowakatalia kwa kauli nzuri kutowatii katika yale yatakayotupelekea kumuasi na kumshirikisha Allah (s.w). Tusiyumbishwe na tishio hili kwa sababu marejeo yetu sote ni kwa Allah (s.w) na ni mjuzi kamili juu ya dhamira (nia) zetu na vitendo vyetu - "โ€ฆkisha marejeo yenu ni kwangu, Hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda" (31:15).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 1995

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 web hosting     ๐Ÿ‘‰2 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰5 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Lengo la kuletwa mitume

Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:โ€œKwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere..

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu

Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)

Soma Zaidi...
Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu

Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).

Soma Zaidi...
Makemeo juu ya Zinaa na Hukumu kwa Wazinifu.

Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.

Soma Zaidi...