Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini!
(f) Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumba zenu mpaka muombe ruhusa, (mpige hodi) na muwatolee salamu waliomo humo. Hayo ni bora kwenu; huenda mtakumbuka (mkaona ni mazuri haya mnayoambiwa).
Na kama hamtamkuta humo yeyote, basi msiingie mpaka mruhusiwe . na mkiambiwa "Rudini," basi rudini; hili ni takaso kwenu. Na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyaatenda. Si vibaya kwenu kuingia majumba yasiyokaliwa, (yasiyofanywa maskani: kama mahoteli, maktaba), ( bila kupiga hodi), ambamo humo mna manufaa yenu; na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyadhihirisha na mna yoyaficha. (24:27-29)
Kutokana na aya hizi tunajifunza adabu za kuingia katika nyumba za watu kama ifuatavyo:
(i)Hairuhusiwi mtu kuingia nyumba ya mtu bila ya kubisha hodi. Hata kama utaukuta mlango uko wazi, huruhusiwi kuangaza macho ndani. Hivyo wakati wa kubisha hodi unatakiwa uwe pembeni mwa mlango, kiasi kwamba hata kama mlango umefunguliwa usiweze kumuona mtu au vitu vilivyomo ndani. Vile vile hairuhusiwi kubisha hodi kupitia mlango wa uani au madirishani. Hekima ya amri hii ya kubisha hodi, ni kulinda haki ya faragha (privacy) ambayo ni haki ya msingi kwa binaadamu katika mambo mema.
(ii)Hata baada ya kuruhusiwa kuingia katika nyumba za watu,hatutaingia mpaka kwanza tuwatolee salamu waliomo ndani.
(iii)Kama mtu atabisha hodi mara tatu bila ya kuitikiwa, hata kama atakuwa anawasikia watu wakiongea ndani, asiingie bali aondoke aende zake bila kinyongo.
(iv)Iwapo mtu ataitikiwa baada ya kubisha hodi na badala ya kukaribishwa ndani akaambiwa arudi, hanabudi kurudi kwa moyo mkunjufu bila ya manung'uniko yoyote.
(v)Hatuhitajiki kubisha hodi kwenye nyumba zenye kutoa huduma za kijamii kama vile hoteli, maktaba, msikiti, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 ai web app 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu
Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ?
Soma Zaidi...Shahada mbili
Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...Kujiepusha na maringo na majivuno
Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri.
Soma Zaidi...Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?
Soma Zaidi...