Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu

Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu

"Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za s

Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu

(g) Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu.


"Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za wale mliowashikia funguo zao, au rafiki zenu. Si vibaya juu yenu kama mkila pamoja au mbali mbali. Na mnapoingia katika majumba toleaneni salamu; (maamkio haya) ni zawadi itokayo kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka, na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyokubainishieni Aya (zake) ili mpate kufahamu." (24:61)



"Enyi mlioamini! Msiingie nyumba za Mtume ila mpewe ruhusa kwenda kula, pasipo (kwenda kukaa) kungojea kiivie. Lakini mtakkapoitwa ingieni, na mnapokwisha kula tawanyikeni. Wala msiweke mazungumzo, maana jambo hili linamuudhi Mtume, naye anakuoneeni haya; lakini Mwenyezi Mungu Haoni haya kusema haki. Nanyi mnapowauliza (wakeze) waulizeni nyuma ya pazia. Kufanya haya kutasafisha nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikupasieni (haitakikani) kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wala kuwaoa wake zake baada yake; kabisa. Hakika jambo hilo ni (dhambi) kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. (33:53)
Tukizingatia aya hizi tunapata maelekezo ya kimaadili yafuatayo:



(i) Pamoja na kwamba Uislamu unahimiza ukarimu, haumuhusu kwa pande mmoja, kuingia na kula katika nyumba za watu pasi na mwaliko rasmi. Kuvamia chakula katika nyumba za watu ni kuvuruga utaratibu wa familia na kuleta kero, jambo ambalo halikubaliki katika Uislamu. Kwa upande mwingine, katika mafundisho ya Uislamu, akija mgeni asiyerami (mgeni wa kupita) asitoke bila ya kumkirimu chochote, angalau maji ya kunywa; naye apokee lakini ahakikishe kuwa hawakalifishi wenyeji wake.



(ii)Wanaoruhusika kula chakula watakacho kikuta ni wanafamilia wenyewe na jamaa wa karibu kama walivyotajwa katika aya (24:61). Marafiki walioainishwa katika aya hii ni wale marafiki wa ndani walioshibana na familia (rafiki ndugu).



(iii)Wengine wanaoruhusika kula chakula katika nyumba za watu bila mwaliko rasmi ni wagonjwa, vilema, na wengine walioathirika kiuchumi wanaotambulika kisheria na wanaohitajia msaada wa Waislamu.



(iv)Waislamu watakapopata mwaliko wa kwenda kula katika nyumba za watu, waje pale kwa wakati uliopangwa na baada ya kula waombe ruhusa ya kuondoka ili kuwapa wenyeji wao uhuru wa kufanya mambo yao mengine ya faragha (yanayohusu familia).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views: 1748

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰2 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰5 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Muombe Allah wakati unapokuwa na furaha.

Amesimulia Abuuhurairah ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… amesema "โ€ ู…ูŽู†ู’ ุณูŽุฑู‘ูŽู‡ู ุฃูŽู†ู’ ูŠูŽุณู’ุชูŽุฌููŠุจูŽ ุงู„ู„ู‘ูŽู‡ู ู„ูŽู‡ู ุนูู†ู’ุฏูŽ ุงู„ุดู‘ูŽุฏูŽุงุฆูุฏู ูˆูŽุงู„ู’ูƒูุฑูŽุจู ููŽู„ู’ูŠููƒู’ุซูุฑู ุงู„ุฏู‘ูุนูŽุงุกูŽ ูููŠ ุงู„ุฑู‘ูŽุฎูŽุงุกู โ€" โ€ โ€œmwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa rahaโ€. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).

Soma Zaidi...
Dua sehemu 03

Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa.

Soma Zaidi...
KUINGIA KWA WAGENI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUINGIA KWA WAGENI Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie.

Soma Zaidi...